Hawa CCM wamezidwa hawawezi hata kupumua ukweli Mkapa akihutubu kuna vijana na T-shirt za njano toka sehemu mbalimbali za Igunga ndio walikuwa wanaingia,wananchi waliondoka soma chini Mwananchi katueleza Sinema nzima
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Mkapa awaponda wapinzani
[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Sunday, 11 September 2011 11:17
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0diggsdigg
Boniface Meena na Daniel Mjema, Igunga
RAIS Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amevishangaa vyama vya upinzani vinavyodai kuwa Serikali ya CCM haijafanya chochote, wakati wanaujua kuwa chama hicho. kimefanya mengi yaliyoiletea maendeleo Tanzania.
Mkapa alisema katika Uwanja wa Sokoine, mjini Igunga wakati akizindua kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo na kumnadi mgombea wa chama hicho, Dk Peter Kafumu.
Alisema vyama hivyo vilianza mwaka 1992 kutokana na kutofautiana na sera za CCM, lakini hadi leo havijawahi kueleza hitilafu hizo zilitokana na nini na badala yake vimekaa kukishambulia chama kilichopo madarakani bila kuangalia wanachokisema.
"Tuwakanyagekanyage kwa kuwa walioko upinzani walihitilafiana na CCM kisera na ningependa waeleze hitilafu ilitokana na nini," alisema.
Alisema baadhi ya vyama hivyo vinasema kuwa alipokuwa madarakani hakufanya kitu, lakini wanashindwa kueleza kama barabara walijenga wao au ni Serikali yake ndiyo iliyofanya hivyo.
"Wana Igunga msidangaywe CCM imejenga shule za kutosha na suala la afya kazi imefanyika, anayesema hatukufanya chochote anaishi dunia ya wapi? alihoji Mkapa.Alisema wakati anaingia madarakani kulikuwa na benki moja ya biashara ambayo ni NBC, lakini ilikuwa inaomba ruzuku Serikalini kitu ambacho kilikuwa siyo sawa.
"Tuliona tuibinafsishe kwa kuwa huwezi kuwa na benki ya biashara inayoomba ruzuku, tukaibinafsisha, lakini siyo yote tukabakia na asilimia za Serikali," alisema na kuongeza."Wanasema nimeuza benki yetu, siyo hivyo nimeuza madeni yetu na kuisaidia nchi. Tumejaribu, tunaweza na tunasonga mbele."
Mkapa alisema vyama hivyo vinavyoishambulia Serikali ya CCM vinakwenda nje kwenda kuomba ruzuku, lakini CCM ikienda kushughulikia suala la maendeleo wanalalamika."Sera za CCM ndiyo nambari one, kazi yao ni kusema tu, kaiba hili, kafanya lile, demokrasia…," alisema Mkapa.Alisema kuwa kama kweli wapinzani wanafanya mazuri basi wawaeleze wananchi sera zao mbadala ni zipi na si kuzungumza tu bila utaratibu.
"Wapinzani wana sera mbadala zipi? Mkapa alihoji.
Alisema Serikali ya CCM imesaidia ukombozi wa nchi nyingi za Afrika na maeneo mbalimbali katika kuleta amani, huku akitoa mfano wa yeye na Rais Jakaya Kikwete walivyolishughulikia suala la Kenya baada ya kutokea vurugu za uchaguzi uliopita.
Aliwaambia wananchi wa Igunga kuwa Serikali ya CCM inashughulikia mradi wa maji kutoka Nzega hadi Igunga ili kutatua suala hilo la maji kwa eneo la Igunga.
"Jamani tunafanya kazi kwa utaratibu hata Roma haikujengwa kwa siku moja, nashangaa viongozi wengine wa upinzani walisoma huko, lakini hawakujifunza kuwa Roma haikujengwa siku moja," alisema.
Alisema kuwa, sera za CCM ndizo zitakazoimarisha Uhuru wa Tanzania na jukumu la maendeleo ya nchi ni la Watanzania wote.
Alisema sera za upinzani ni za kupinga kila kitu, na kuangusha serikali.Aliwataka wananchi wa Igunga, kumchagua Dk Kafumu kwa kuwa ni mpambanaji na anajua mfumo wa serikali ulivyo.
Kabla Mkapa alisema kuwa hajahutubia mkutano uliohudhuriwa na watu wengi kama huo kwa miaka sita iliyopita.
"Sijahutubia mkutano wa hadhara kama huu kwa miaka sita kwa hiyo mkiniona legelege mnisamehe," alisema.
Rostam aibuka kwenye uzinduzi
Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz jana aliibuka kwenye uzinduzi wa kampeni hizo na kuwaeleza wananchi wa Igunga kuwa amesimama kama mkazi mwenzao, mbunge mstaafu na mwanachama wa CCM.
"Nimesimama hapa kama mkazi wa Wilaya ya Igunga, mbunge mstaafu na mwanachama wa CCM na ninaomba mmpe Kafumu kura zenu zote," alisema Rostam.
Nchemba aikandia Chadema
Mratibu wa Kampeni za jimbo hilo, Mwigulu Nchemba aliishukia Chadema akieleza kuwa wamefika Igunga kutafuta jimbo ili waongeze ruzuku na kuendelea kufanya maandamano zaidi nchini.
Alisema Chadema kimeipinga Serikali kupandisha bei ya pamba katika mkoa wa Tabora kwa madai kuwa itawaharibia katika uchaguzi wa Igunga.
Vijana wamwagwa mkutanoni
Vijana waliokuwa wamevalia fulana za njano walimwagwa mjini Igunga wakitokea vijiji mbalimbali vya jimbo hilo ili kuhudhuria mkutano huo wa uzinduzi.
Vijana hao ambao walikuja wakati matangazo ya mkutano yakiendelea walitinga wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali baadaye kutakiwa kukaa kwa utulivu.
Vijana hao walitanda kila kona ya mkutano wengine wakiwa wamekaa mbele ya jukwaa na kumshangilia Mkapa alipokuwa akihutubia.
Wengine waondoka mkutanoni
Wakati Mkapa akiendelea kuhutubia, baadhi ya watu wakiwa kwenye makundi walianza kuondoka kwenye mkutano huo.
Wengi waliohojiwa na Mwananchi Jumapili walisema hakuna jipya katika hotuba ya Mkapa na kuongeza kuwa, waliyokuwa wakiambiwa na wapinzani yalithibitishwa na Mkapa mwenyewe.
Walitoa mfano kuwa Mkapa alipoingia madarakani, makusanyo ya Serikali kwa mwezi yalikuwa ni Sh28 bilioni, lakini hadi anaondoka, makusanyo hayo yalikuwa ni Sh400 bilioni na kuongeza kuwa ni wazi Serikali ina fedha, lakini hazitumiki kwa shughuli za maendeleo.
Maandalizi ya uzinduzi
Kuanzia juzi CCM imekuwa ikihamasisha wafuasi wake waweze kufika kwenye ufunguzi wa kampeni zao, huku magari ya chama hicho yakionekana kupita kona mbalimbali za Igunga.
Jana kuanzia asubuhi mashangingi ya viongozi wa ngazi za juu ya CCM yalionekana yakipita sehemu mbalimbali katika mji wa Igunga na baadhi ya wananchi wakiwa kuvaa nguo za rangi za kijani na njano. Bendera za CCM zilikuwa zinapepea kila kona ya mji wa Igunga.