Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.

Kuishi kwingi kuona mengi. Sasa huyu anazungumzia nini?? nimemsoma tangu mwanzo mpaka mwisho simuelewi!!
 
Du nawahurumia, dalili za ccm kufulia kisiasa ndo hizi, nilitegemea wataandika habari za kujinadi na kueleza kwa nini mtu mchafu [fisadi] Rostam amekuwa lulu kwa sasa wakati walimtimua kwa uhujumu wa uchumi wa nchi.
 
imedihirisha si utaratibu wao. Wamekuwa mstari wa mbele kutoa maneno mengi, kashfa na propaganda nyingi

Mi nashangaa sana hili gazeti lao la Uhuru, hivi tangu lini Chadema wamekuwa mstari wa mbele kwa hayo hilo gazeti la kishenzi lililoandika? ni ukweli usiopingika kuwa ccm ndio jibwa linalobweka hovyo! Hivi walikuwa na sababu gani kumleta fisadi lao Ben kwenye uzinduzi wa kampeni kama sio mbinu ya kuwahadaa watanzania kuwa ccm inapendwa kwa kujaza umati wa watoto na kuonyesha picha kwnye uozo wao wa tbc..eti watanzania waseme kuwa magamba wanakubalika..Huu ni ujuha wa ccm na gazeti lao. Hatudanganyiki.
 

Na bila shaka mbwa anayebweka sana huko igunga ni magamba. Mwenye mbwa amegundua kwamba mbwa wake haumi pamoja na kubweka sana kwahiyo ameamua kumsaidia mbwa wake kubweka. I think you know what i mean,......!!
 
Wajameni: Alisikika Mkapa akisema 'Na nyie Takukuru tunaomba mtuache tugawe mahindi kwa kuwa ccm ni chama sikivu, na hii sio rushwa mmesikia'? Hii ilitokea kwenye ufunguzi wa malumbano yao Igunga, na utafiti tumefanya na kugundua mahindi yanagawiwa mchana kweupe. Hayo ndio maendeleo anayosema Ben yanampa faraja kabisa. Lami toka Dar hadi Mwanza, chakula kaputii... Nchi hii bwana.

Sasa hapo napenda kusema Takukuru walijibu 'Sawa mkuu, na sasa mtagawa viroba vingapi?. Yaani hii ni sawa na Mkweree alipoambiwa na Marekani, 'Hey hebu ruka juu' Yeye alijibu 'Sawa mkuu, sasa niruke hadi wapi - nipimie wewe'.

Wisdom: Tulipitisha sheria ya uchaguzi ambayo sina hakika kama huyu Ben aliipitia kwa ukamilifu. Tunamuomba Tendwa atoe tamko vinginevyo ccm inagawa rushwa njenje. Yaani hii inakera sana. Wana JF, nawasilisha.
 
safari hii ni mpaka kieleweke na hizo ni mvua za rasharasha tu.Don,t give up CHADEMA!
 
Mimi kinachonishangaza Gazeti la Uhuru lina toa habari nyeti kama hizi lakini hawamuweki Mhariri wa habari hii kwa Jina? Kuna tatizo gani? atauawa?

Hapa sio kama Russia, be out and defend your means of information.

Na hili gazeti linasafirishwa kweli Mikoani nilishaliona kule Ngudu Mwanza na Wananchi wanalinunua bei nusu lakini wanasoma unadhani wanapata matinki gani kuona kichwa hiki cha habari?

Tusiidharahu hii MIpango ya Serikali ya CCM; kwa kutumia Gazeti ambalo hakuna analolisoma Mjini lakini wapiga kura wengi vijijini na nadhani hata Igunga bado wanasoma
 
hawa ndio wale watu ambao huwa wanakurupuka asubuhi bila hata kupiga mswaki na kuchana nyele
 
Hivi hili gazeti linajiendeshaje?au ndo matumizi mabaya ya kodi zetu na habari za kupikia ofisin, lishindwe.
 
mwandishi wa habari hii naomba awe wa kwanza kuisaidia polisi kwani inaonekana ana ushahd tosha kabisa ..sasa naomba awawasilishie polisi ili madai haya yathibtke na chadema waweze kupoteza jimbo....vinginevyo hz ni propaganda za kawaida za magamba....kwani hata bashe hakuwa raia wa nchi hii...ila kwa ss ni raia..ccm huwa tayari hata kutoa fedha nying kwa propaganda kama hz ili zienee lakini wananchi wa ss c wajinga kias hicho
 
Nyie si mlitaka UHURU isifie CDM ndio lionekane gazeti la maana, wamesema ukweli kabisa. CDM ni chama cha wahuni na wavuta bangi.

Mimi nadhani kwa suala la kuzungumzia CHADEMA, Uhuru sio objective source hata kidogo, suala sio kusifia hapa. Halafu ndugu hata kama CAHDEMA wana makosa yao mbona lugha uliyotumia ni kali sana, unadhani kwa mtazamo huu tutaijenga Tanzania ya amani, utulivu, kuheshimiana na demokrasia ya kweli? TAFAKARI
 
Sijui kama ni mzima kweli! au unamatatizo ya akili mgando, magwanda ya CHADEMA si kitu kipya duniani na hata Tanzania. WAMAGAMBA walianza kuvaa magwanda na kuwavisha hata watoto wa shule za msingi wakiwaitwa CHIPUKIZI. Sasa washangaa nini kama huna sehemu ya kujipatia umaarufu nenda hata BIG BROTHER utafahamika tu, kijana.
 
Kweli wanaIGUNGA mtakubali, ANGALIENI SANA HISTORIA ITAWASULUBU KWA MIAKA 5?!!
 
Du!!!!!!!!!!!!
Ndugu zangu kwa kinachoendelea Igunga ndio kitakuwa kipimo kizuri cha akili za wa-Tanzania. Yaani waliyemvua gamba kwa kashfa mbalimbali ndie anapandishwa kumuombea kura Kafumu? Tena alisema amechoshwa na siasa uchwara za CCM! DUUUUUUUUUUUUUUU. Ama kweli kumekucha. Hilo ni gamba lingine.
 
Regardless of the source ya hii habari..inabidi tukubaliane kuwa..chadema wamekuwa chanzo cha vurugu na vifo vingi vya watu wasio na hatia
Kama maandamano ya kudai haki ni fujo basi na haya matembezi ya jazba yaliyoandaliwa na sheikh Ponda pia ni chanzo cha vurugu.
 
Nyie si mlitaka UHURU isifie CDM ndio lionekane gazeti la maana, wamesema ukweli kabisa. CDM ni chama cha wahuni na wavuta bangi.
Kama kufanya maandamano ya amani na kutoa elimu ya uraiya ni kitendo cha kihuni na cha kivuta bangi basi Sheikh Ponda anavuta bangi na anahamasisha wahuni wenzake kuandamana kupinga hotuba ya JK kuhusu kadhi.
 

Hapa hawapati kitu. CHADEMA imekufa na inaendelea kufa.

Kwa kuthibitisha hayo ni pale ambapo 'Mode' amezibana Thread zangu zaidi ya 5 nilizoeleza KUPANDA NA KUSHUKA KWA CHADEMA NA MH SLAA. Alipokataa kuzirusha hewani nikajua ujumbe umemfikia MODE, kwani alifikiri kuwa ukweli hatuujui kumbe siri imefichuka. Kama mimi si mkweli aziachie hizo THREAD ili nijibu maswali.

Huu ndio mwisho wa CHADEMA, NA Igunga haipati kitu.
 

Acha kuficha ukweli, Eleza pia juu ya mgombea wa CUF. Utawezaje kupata maelezo ya mgombea wa CHADEMA ambaye hata hakushika nafasi yeyote katika uchaguzi uliopita na ushindwe kupata maelezo hata hatua moja juu ya mgombea aliyeshika nafasi ya pikli katika uchaguzi uliopita? Ni bora usingeandika kitu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…