Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Binafsi naiunga mkono CHADEMA lakini si kama Kipofu. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba CCM si mama yake wala si dini yake. Hata mimi CHADEMA si mama yangu wala si dini yangu lakini ni chama ninachokiunga mkono toka moyoni mwangu.


Hii ya kada Wa CHADEMA aliitoA JANA....nI MATUMAINI YANGU SIKU YA KUPIGA KURA ATAKUWA CCM baada ya kusikia hili la Wafuasi wa chadema kumwalibia mpigakura wa nchi hii,chama kinachohubiri demokrasia hakikubali kushindwa ndipo napo shakaaa.
CCM kinabaki chama bora,kinachoheshimu matakwa ya watu wengi...

Kuishi kwingi kuona mengi. Sasa huyu anazungumzia nini?? nimemsoma tangu mwanzo mpaka mwisho simuelewi!!
 
Du nawahurumia, dalili za ccm kufulia kisiasa ndo hizi, nilitegemea wataandika habari za kujinadi na kueleza kwa nini mtu mchafu [fisadi] Rostam amekuwa lulu kwa sasa wakati walimtimua kwa uhujumu wa uchumi wa nchi.
 
imedihirisha si utaratibu wao. Wamekuwa mstari wa mbele kutoa maneno mengi, kashfa na propaganda nyingi

Mi nashangaa sana hili gazeti lao la Uhuru, hivi tangu lini Chadema wamekuwa mstari wa mbele kwa hayo hilo gazeti la kishenzi lililoandika? ni ukweli usiopingika kuwa ccm ndio jibwa linalobweka hovyo! Hivi walikuwa na sababu gani kumleta fisadi lao Ben kwenye uzinduzi wa kampeni kama sio mbinu ya kuwahadaa watanzania kuwa ccm inapendwa kwa kujaza umati wa watoto na kuonyesha picha kwnye uozo wao wa tbc..eti watanzania waseme kuwa magamba wanakubalika..Huu ni ujuha wa ccm na gazeti lao. Hatudanganyiki.
 
"Kama alivyonena Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, kwamba ‘hivi karubuni, siku zote mbwa anayebweka sana, huwa haumi,’ hivyo hilo limekuwa haliumizi kichwa CCM ambayo imeenda katika matendo zaidi."

Kama haliwaumizi kichwa andiko hili ni la nini? CCM mmeshikwa pabaya msijidanganye kuwa kichwa hakiumi sababu ya CDM, hayo ni maneno ya mfa maji.

Na bila shaka mbwa anayebweka sana huko igunga ni magamba. Mwenye mbwa amegundua kwamba mbwa wake haumi pamoja na kubweka sana kwahiyo ameamua kumsaidia mbwa wake kubweka. I think you know what i mean,......!!
 
Wajameni: Alisikika Mkapa akisema 'Na nyie Takukuru tunaomba mtuache tugawe mahindi kwa kuwa ccm ni chama sikivu, na hii sio rushwa mmesikia'? Hii ilitokea kwenye ufunguzi wa malumbano yao Igunga, na utafiti tumefanya na kugundua mahindi yanagawiwa mchana kweupe. Hayo ndio maendeleo anayosema Ben yanampa faraja kabisa. Lami toka Dar hadi Mwanza, chakula kaputii... Nchi hii bwana.

Sasa hapo napenda kusema Takukuru walijibu 'Sawa mkuu, na sasa mtagawa viroba vingapi?. Yaani hii ni sawa na Mkweree alipoambiwa na Marekani, 'Hey hebu ruka juu' Yeye alijibu 'Sawa mkuu, sasa niruke hadi wapi - nipimie wewe'.

Wisdom: Tulipitisha sheria ya uchaguzi ambayo sina hakika kama huyu Ben aliipitia kwa ukamilifu. Tunamuomba Tendwa atoe tamko vinginevyo ccm inagawa rushwa njenje. Yaani hii inakera sana. Wana JF, nawasilisha.
 
safari hii ni mpaka kieleweke na hizo ni mvua za rasharasha tu.Don,t give up CHADEMA!
 
Mimi kinachonishangaza Gazeti la Uhuru lina toa habari nyeti kama hizi lakini hawamuweki Mhariri wa habari hii kwa Jina? Kuna tatizo gani? atauawa?

Hapa sio kama Russia, be out and defend your means of information.

Na hili gazeti linasafirishwa kweli Mikoani nilishaliona kule Ngudu Mwanza na Wananchi wanalinunua bei nusu lakini wanasoma unadhani wanapata matinki gani kuona kichwa hiki cha habari?

Tusiidharahu hii MIpango ya Serikali ya CCM; kwa kutumia Gazeti ambalo hakuna analolisoma Mjini lakini wapiga kura wengi vijijini na nadhani hata Igunga bado wanasoma
 
hawa ndio wale watu ambao huwa wanakurupuka asubuhi bila hata kupiga mswaki na kuchana nyele
 
Hivi hili gazeti linajiendeshaje?au ndo matumizi mabaya ya kodi zetu na habari za kupikia ofisin, lishindwe.
 
mwandishi wa habari hii naomba awe wa kwanza kuisaidia polisi kwani inaonekana ana ushahd tosha kabisa ..sasa naomba awawasilishie polisi ili madai haya yathibtke na chadema waweze kupoteza jimbo....vinginevyo hz ni propaganda za kawaida za magamba....kwani hata bashe hakuwa raia wa nchi hii...ila kwa ss ni raia..ccm huwa tayari hata kutoa fedha nying kwa propaganda kama hz ili zienee lakini wananchi wa ss c wajinga kias hicho
 
Nyie si mlitaka UHURU isifie CDM ndio lionekane gazeti la maana, wamesema ukweli kabisa. CDM ni chama cha wahuni na wavuta bangi.

Mimi nadhani kwa suala la kuzungumzia CHADEMA, Uhuru sio objective source hata kidogo, suala sio kusifia hapa. Halafu ndugu hata kama CAHDEMA wana makosa yao mbona lugha uliyotumia ni kali sana, unadhani kwa mtazamo huu tutaijenga Tanzania ya amani, utulivu, kuheshimiana na demokrasia ya kweli? TAFAKARI
 
Sijui kama ni mzima kweli! au unamatatizo ya akili mgando, magwanda ya CHADEMA si kitu kipya duniani na hata Tanzania. WAMAGAMBA walianza kuvaa magwanda na kuwavisha hata watoto wa shule za msingi wakiwaitwa CHIPUKIZI. Sasa washangaa nini kama huna sehemu ya kujipatia umaarufu nenda hata BIG BROTHER utafahamika tu, kijana.
 
Kweli wanaIGUNGA mtakubali, ANGALIENI SANA HISTORIA ITAWASULUBU KWA MIAKA 5?!!
 
Du!!!!!!!!!!!!
Ndugu zangu kwa kinachoendelea Igunga ndio kitakuwa kipimo kizuri cha akili za wa-Tanzania. Yaani waliyemvua gamba kwa kashfa mbalimbali ndie anapandishwa kumuombea kura Kafumu? Tena alisema amechoshwa na siasa uchwara za CCM! DUUUUUUUUUUUUUUU. Ama kweli kumekucha. Hilo ni gamba lingine.
 
Regardless of the source ya hii habari..inabidi tukubaliane kuwa..chadema wamekuwa chanzo cha vurugu na vifo vingi vya watu wasio na hatia
Kama maandamano ya kudai haki ni fujo basi na haya matembezi ya jazba yaliyoandaliwa na sheikh Ponda pia ni chanzo cha vurugu.
 
Nyie si mlitaka UHURU isifie CDM ndio lionekane gazeti la maana, wamesema ukweli kabisa. CDM ni chama cha wahuni na wavuta bangi.
Kama kufanya maandamano ya amani na kutoa elimu ya uraiya ni kitendo cha kihuni na cha kivuta bangi basi Sheikh Ponda anavuta bangi na anahamasisha wahuni wenzake kuandamana kupinga hotuba ya JK kuhusu kadhi.
 
Mimi, kama 'President Elect', niko tayari kuvaa gwanda endapo CHADEMA kitafanikiwa kushinda uchaguzi mdogo, jimbo la Igunga.

Hii ni changamoto kwa CHADEMA na wapambe wao hapa JF, ambao macho na masikio yao yanafuatilia uchaguzi wa Igunga.

Jimbo la Igunga ni karata dume, ambayo CCM wanayo mikononi mwao. Kazi kwenu CHADEMA kuwapokonya, na kama mtafanikiwa, basi na mimi nitavaa gwanda, kama ilivyo kwa mh. Freeman Mbowe au mh. Zitto Kabwe. Nasema tena, kazi kwenu CHADEMA!

Hapa hawapati kitu. CHADEMA imekufa na inaendelea kufa.

Kwa kuthibitisha hayo ni pale ambapo 'Mode' amezibana Thread zangu zaidi ya 5 nilizoeleza KUPANDA NA KUSHUKA KWA CHADEMA NA MH SLAA. Alipokataa kuzirusha hewani nikajua ujumbe umemfikia MODE, kwani alifikiri kuwa ukweli hatuujui kumbe siri imefichuka. Kama mimi si mkweli aziachie hizo THREAD ili nijibu maswali.

Huu ndio mwisho wa CHADEMA, NA Igunga haipati kitu.
 
UCHAGUZI IGUNGA:




Kura zikipigwa leo
*CCM kupata asilimia 39
*CHADEMA asilimia 37
*CUF kupata asilimia 18
*Vyama vingine asilimia 6
Na Waandishi Wetu, Igunga na Dar
Katika utafiti huo ambao umefanyika katika kata 20 za jimbo hilo, wastani wa watu 50 wenye umri kati ya miaka 20 hadi 50 walihojiwa katika kila kata na kutoa maoni yao.
Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa, kama uchaguzi huo ungefanyika wiki hii, basi matokeo yangekuwa kwamba CCM ingepata asilimia 39, CHADEMA asilimia 37, CUF asilimia 18 huku vyama vingine vilivyosalia vikigawana asilimia sita.
Kata zilizohusika kwenye utafiti huo ni Igunga, Itumbi, Bukoko, Isakamalwa, Nyandekwa, Mbutu, Kining'ila, Mwamashinga, Choma, Kinungu, Ntobo, Igurubi, Hundwa, Mwashiku, Ziba, Ndembezi, Nkinga, Ngulu, Sungwi na Mwisi.
Wagombea katika uchaguzi huo ni Mwalimu Joseph Kashindye (CHADEMA), Dk. Peter Kafumu (CCM), Leopold Mahona (CUF), Hemed Dedu (UPDP), Said Cheni (DP), John Maguna (SAU) na Stephen Makingi (AFP).
Utafiti huo umeonesha kuwa wanaokiunga mkono CCM wanajivunia mtandao wa wanachama wake katika maeneo mbalimbali jimboni, ingawaje wanakiri moja kwa moja kuwapo kwa mgawanyiko na kuwapo kwa makundi.
"Sisi wana-CCM tunao uwezo wa kuwakabili vilivyo wapinzani wetu, kwa sababu watu tunao, sera zetu zinaeleweka, lakini tatizo letu ni kutoelewana wenyewe kwa wenyewe, hili linaweza kutuangusha.
"Sasa hivi baadhi yetu wanawaona viongozi wa kitaifa kama wasaliti na watu wasiolitakia mema jimbo letu, hasa baada ya aliyekuwa Mbunge wetu Rostam Aziz kujiuzulu kutokana na siasa chafu ndani ya chama.
"Tatizo ni kubwa zaidi, kwa sababu baadhi ya wenzetu wameshasema wazi kuwa hawatapiga kura, na kuna uwezekano wengine wakawapigia wapinzani ili kulikomoa kundi au watu fulani, hii hali si nzuri kwa chama chetu," alisema Mwenyekiti wa moja ya matawi maarufu ya CCM Igunga Mjini.
Kwa upande wa CHADEMA, utafiti umebaini kuwa kinaungwa mkono na makundi ya vijana na wafanyabiashara, makundi ambayo yanaonekana kuwa na kiu ya manadiliko.
Kutokana na ukweli huo, chama hicho ambacho kinatarajiwa kutoa upinzani mkubwa kwa CCM na CUF, kinatarajia kupata kura nyingi katika maeneo ya mjini, ambako umaarufu wake umekuwa ukikua kwa kasi tangu kuanza kwa vuguvugu la uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu.
Pia wananchi wengi ambao walihojiwa na kuonekana kukiunga mkono CHADEMA, ni wale ambao wanakabiliwa ugumu wa maisha unaotokana na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu kwa ajili ya matumizi ya kila siku.
Kundi hili linaonekana kufurahishwa na sera ya chama hicho (CHADEMA) ya kupambana na umasikini kwa kuhakikisha rasilimali za nchi zinanufaisha wananchi husika, pamoja na kupigania bei bora za mazao ya biashara, ikiwamo pamba inayolimwa kwa wingi jimboni huo.
Kwa upande wa CUF, wananchi wengi waliohojiwa ambao wanaonekana kukiunga mkono wanaweka karata yao zaidi kwenye idadi ya kura 11,000 alizopata mgombea wao katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
"Sisi tayari tuna kura zetu zaidi 10,000i, kwa hiyo tunahitaji kuweka nguvu zaidi kuziongeza, sera zetu zinafahamika Igunga, mgombea wetu ni mtoto wa hapa hapa, kwa hiyo tunachosubiri ni ushindi wa kishindo, labda tuhujumiwe," alisema mfanyabiashara mmoja katika soko la Igunga, aliyejitambulisha kwa jina la Doto Maganga.
Matatizo ya wananchi wa Igunga
Wakati kampeni zikiingia siku ya pili leo, uchunguzi umebaini matatizo kadha wa kadha yanayowakabili wapigakura wa Igunga, matatizo ambayo wanatarajia Mbunge wao mpya atayapatia ufumbuzi.

Miongoni mwa matatizo hayo ni uhaba wa chakula unaolikabili jimbo hilo kutokana na uhaba wa mvua, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa limeathiri shughuli za maendeleo hasa maeneo ya vijijini.

Aidha, kuna hali ya umasikini wa kutisha kama ilivyo kawaida katika sehemu nyingi nchini ikichochewa na mfumuko wa bei, kupanda na kushuka kwa bei za mafuta na kudorora kwa shughuli za uchumi kama vile biashara na kilimo.

Vile vile kuna kuporomoka kwa bei ya pamba, zao kuu la biashara kwa wakazi wa jimbo hilo kumezidisha ukali wa maisha, ingawaje kumekuwapo juhudi za kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri sokoni.

Jimbo la Igunga pia linakabiliwa na tatizo sugu la miundombinu ya barabara, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa limeathiri mawasiliano kati ya sehemu moja hadi nyingine.

Taarifa zaidi zimesema kuwa, pamoja na Mbunge aliyejiuzulu kujitahidi kutatua matatizo yaliyopo kwenye sekta za afya na maji, bado nguvu kubwa inahitajika kukidhi mahitaji wa wana-Igunga.

Wagombea wa CCM, CHADEMA, CUF wanavyotazamwa
Mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, amewahi kugombea mara kadhaa, ambapo mara ya mwisho alianguka kwenye kura za maoni, wakati Mbunge aliyejiuzulu, Rostam Aziz, akiibuka mshindi.

Kwa sasa yeye ni Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, na ni msomi aliyebobea katika masuala ya madini akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Madini.

Lakini uchunguzi umebaini kuwa, kwa wakazi wengi wa Igunga, Dk. Kafumu anaonekana si mwanasiasa, si mkazi wa Igunga na pia ni mtu ambaye ni vigumu kujichanganya na watu, ingawaje anatajwa kuwa anaweza kuukwaa uwaziri kama atashinda, ikiwa yatafanyika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Kwa upande wake, mgombea wa CHADEMA, Mwalimu Joseph Kashindye, yeye ni Mkaguzi wa Elimu wa Wilaya ya Igunga, pia ana historia ndefu katika Sekta ya Elimu.

Alianza kazi ya ualimu akiwa kama Mwalimu wa UPE, lakini amekuwa na bidii kubwa katika kujiendeleza, na hivi sasa ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika masuala ya elimu.

Kwa wakazi wengi wa Igunga, anaonekana kuwa ni mkazi mwenzao, anafahamu matatizo ya siku hadi siku ya Igunga, pamoja na yale yanayowakabili walimu na wanafunzi.

Kuhusu mgombe wa CUF, Leopold Mahoma, Rai haikuweza kupata taarifa zake kwa kina, lakini kama alivyo mgombea wa CHADEMA, yeye pia ni mkazi wa Igunga, na katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alishika nafasi ya pili nyuma ya mgombea wa CCM, ambapo alipata kura 11,000.

Acha kuficha ukweli, Eleza pia juu ya mgombea wa CUF. Utawezaje kupata maelezo ya mgombea wa CHADEMA ambaye hata hakushika nafasi yeyote katika uchaguzi uliopita na ushindwe kupata maelezo hata hatua moja juu ya mgombea aliyeshika nafasi ya pikli katika uchaguzi uliopita? Ni bora usingeandika kitu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom