................Mara zote watu wanapodai haki na ustawi wao,watawala juha uwa wanamaneno yafuatayo...."Hao ni wavunja amani na wahuni,tazama maneno ya Gaddafi na wengine wengi" Tujiulize,kama kuna haki na watu wanapewa uhuru wa kufanya mambo yao bila kuminywa na kudharauliwa nani ataleta vurugu? Haya yanayotekea Igunga si CHADEMA...Wananchi wamechoka na akili zao zimechoka jamani...Nimepost maoni yangu hapa JF kwenye thread moja nikasema...Watanzani wamepoteza uzalendo kwa kila nyanja,si michezo,utamaduni,siasa,elimu,utu nk...na hili ni zao la kuchoka na kupoteza matumaini mtu anaamua lolote na liwe....CHADEMA haiwezi kumtuma mtu akammwagie mwenzie tindikali,huo ni uchochezi wa CCM na vyombo vyake vya habari....Lakini nakubalia kuwa yawezekana ni watu waliochoka na CCM au wanaCCM wenyewe maana wamezoea kutoana kafara,mifano ipo tena mingi.......Kama hamjui muulizeni Mrema atawaambia alivyokoswakoswa pale ukumbi wa CHIMWAGA chini ya chumba ambacho sasa hivi UDOM wanakitumia kama Computer Laboratory ya Staff....Matukio ya vifo katika siasa katika nchi zote ni zao la wananchi kukosa imani na viongozi wao....