Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Mie nawaomba watu wa Igunga, wachukue mahindi na siku ikifika wao ndio waamuzi.
Tatizo la Watanzania wengi hawana uelewa kama wa kwako. Wengine wanapogawiwa mahindi ndio wanaona kwamba huyo anayewagawia ndiye chaguo la Mungu na ametumwa kuja kuwakomboa, Hawana uwezo wa kujiuliza kwamba muda wote walikuwa wapi mpaka ifike kipindi cha kampeni ndio wagawe hayo mahindi!
Mungu Okoa kizazi hiki!
 
Mitanzania bana!
Mahindi kilo ishirini halafu linaishi kwa tabu miaka minne! Pambafu kabisa!
 
Wana-Igunga, chukueni kila kitu; mahindi kwa CCM, Ubwabwa kwa CCM na fedha nazo toka CCM ila kura zote kwa CDM kuuchinja rasmi ufisadi nchini kwa kuanzia hapo Igunga.

Hizo zote ni kodi zetu walizokwapua huko serikali hivyo ni halali zetu toka kwa wanamagamba hao. Hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Mie nawaomba watu wa Igunga, wachukue mahindi na siku ikifika wao ndio waamuzi.
Naomba nikuwekee maneno mdomoni Mkuu. Yaani siku ikifika wawapige chini ccm, wachague chama kingine. Shida ya njaa ilikuwepo siku nyingi kwanini hawakugawa hayo mahindi. Hiyo ni rushwa moja kwa moja, inabidi tuwahurumie PCCB kwakuwa mazingira yao ya kazi ndo hayo sasa. Kiongozi ambaye PCCB inawajibika kwake (Kikwete) ndio kabariki kugawa rushwa, unless ajitokeze Kikwete (kama anaweza lakini), akanushe maneno yaliyotamkwa na mtangulizi wake (Che Nkapa). Binafsi naamini kinachofanywa na ccm Igunga kina baraka zote za Kikwete (M/kiti).
 
Unapogawiwa mahindi baada ya kunyonywa kwa muda mrefu na majizi kama RA halafu unatoka unacheka kama zuzu unapiga kura ya "ndiyo" ni upuuzi mkubwa sana na udhalilishaji
 
wangelazimisha kugawa msaada wa chakula iramba magharibi kwa mwigulu, jairo na nape ningewaelewa kidoogo. tena yapo maeneo nchini yana njaa kuliko igunga,mbona hawapeleki hiyo misaada ya chakula inayohitajika sana huko. ccm inaharibu ufahamu wa watanzania.
 
Kwani mmesahau enzi za Mkapa Takukuru haikuweza kukamata hata mtuhumiwa mmoja wa rushwa? Alikuwa akiwapa kiuzibe....Mkapa is corrupt. Period!
 
Mi nahisi CCM wameshaona wamepoteza mvuto kabisa kwa waTZ kwa sasa wameanza kufanya ubabe. Ona, Ile hali ya Mkapa kufanya kampeni igunga walidhani watu wangeamka lakini wakakuta mwitiko ni ndogo sana. Sasa wameanza ubabe na wamemtumia Mkapa kwa kuwa yeye ana asili ya ubabe. Ona sasa kauli zake. Pata picha kama CDM wangefanya kile kitendo cha kupita mtaani wakiwahamasisha watu kuhudhuria kampeni siku moja kabla ingekuwaje?

Mimi nasema vurugu zitaanzishwa na CCM wenyewe!! Moja ni hii ya tindikali, kwani kwa mji mdogo kama igunga polisi wanaweza kushindwa kufanya uchunguzi kweli wa kujua nani kasababisha au tunafanyana mambumbumbu? Hili tendo lingekuwa limefanya na wafuasi wa CDM real tayari watu wangekuwa wanahisiwa, kuhojiwa ama kuwekwa mahabusu kabisa. Ila ukweli wa jambo hili ni aibu. Na Yule kijana wanaweza wakamuua kupoteza ushaidi. Hiyo nawapa. Inauma sana ila watanzania na nyie amke jamani.
 
mahindi kwa ccm kura kwa chadema itapendeza sana. ni kweli ccm walijua siku nyingi watu wa Igunga wana njaa, ndiyo maana wanatumia udhaifu huo kuwa rubuni masikini wana Igunga. juzi tu watu wamekula mchele mpaka wakasaza.
 
Kwa kweli tunatakiwa kuwa serious. kwa kauli moja tukubaliane kuto-kuburuzwa. Hivi aliyefanya biashara ikulu (ANNBEN) ndio kikosi kazi kampen ccm-igunga, RA ndio anatu-asure kuwa Kafumu ni mgombea makini kama yeye alivyokuwa mbunge kabla hajajivua gamba kwa siasa uchwara. Na madudu mengine mengi. Hivi baada ya kujiuzulu karibuni, siasa za ccm zimekuwa safi (sio uchwara tena?) tena? kama ndio hivyo kwanini nguvu kubwa itumike kuwashawishi wana-igunga kuhusu ccm (maana kuna msemo-kizuri chajiuza kibaya chajitembeza)? nawewe kijana unayeshabikia ccm kana kwamba unaishi peponi umerogwa? Na kama ni msomi kwa kweli ninamashaka na elimu yako. Hebu tupime maendeleo yetu kwa kutumia indicators zinazo-reflect uhalisia wa maisha ya mtanzania na sio orodha au tarakimu za miradi, majengo nk. ni aibu Pombe kuongoza kwenye pato la taifa ili hali nchi ina madini lukuki yasiyokuwa na tija kwa taifa letu. Hivi tunaandaa taifa la walevi au productive nation interms of capital goods and consumer goods zenye tija au blablablabla. Tafakali.
 
Yan Mkapa hakomagi...na hashindwi kumlazimisha msimamiz wa uchaguz amtangaze kafumu ndo mshndi kama alivofanya zanzibar kaz ipo aisee
 
Kama wana akili watajua kwamba hii sio sawa kabisa wenzao wa Busanda waliwekewa magunzo ya umeme mpaka leo mwaka wa tatu hawajaona umeme ha ha ha CCM ni kiboko cha njia
 
wanakuaje na njaa..wakati mbunge aliyepita alikuwa jembe?...tena jembe la nchi ati?...au alikua hajui matatizo ya jimbo lake bw RA....maana nackia hata Bungeni hakuwahi kuchangia mijadala
 
................Mara zote watu wanapodai haki na ustawi wao,watawala juha uwa wanamaneno yafuatayo...."Hao ni wavunja amani na wahuni,tazama maneno ya Gaddafi na wengine wengi" Tujiulize,kama kuna haki na watu wanapewa uhuru wa kufanya mambo yao bila kuminywa na kudharauliwa nani ataleta vurugu? Haya yanayotekea Igunga si CHADEMA...Wananchi wamechoka na akili zao zimechoka jamani...Nimepost maoni yangu hapa JF kwenye thread moja nikasema...Watanzani wamepoteza uzalendo kwa kila nyanja,si michezo,utamaduni,siasa,elimu,utu nk...na hili ni zao la kuchoka na kupoteza matumaini mtu anaamua lolote na liwe....CHADEMA haiwezi kumtuma mtu akammwagie mwenzie tindikali,huo ni uchochezi wa CCM na vyombo vyake vya habari....Lakini nakubalia kuwa yawezekana ni watu waliochoka na CCM au wanaCCM wenyewe maana wamezoea kutoana kafara,mifano ipo tena mingi.......Kama hamjui muulizeni Mrema atawaambia alivyokoswakoswa pale ukumbi wa CHIMWAGA chini ya chumba ambacho sasa hivi UDOM wanakitumia kama Computer Laboratory ya Staff....Matukio ya vifo katika siasa katika nchi zote ni zao la wananchi kukosa imani na viongozi wao....
 
hacha ujinga wako wewe ni nani kwanza, kwanza usivae gwanda zetu utazitia nuksi....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom