Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Ngoja atakuja hapa kukanuasha na matusi kibao........

Nape kijana anayezidi kuporomoka kisiasa, Rostam aliziita siasa za uchwara, na huko aliokokuwa hatakiwi akaenda tena isitoshe katibu wake mkuu anamchimba biti, sasa ukiwa na akili ambayo haina gamba unaendelea kushikamana na hao watu mpaka lini, ila kutambua hili ni mpaka gamba la ufahamu lidondoke!!!!!!!!!!!!!!
 
Ndio hadithi za kujiliwaza wana CDM. Kama ndio zinawapa raha endeleeni nazo tu. Ndio maana chama chenu kinagawa konyagi huko igunga, hizi stori zinaendana na tungi ile mbaya.
 


Hii taarifa ni ya kishabiki zaidi. Tumezoea kupata kila aina ya takataka kila uchaguzi ukijitokea. Huu ni wakati wa ujio wa kila aina ya NABII.
 
Sasa hapo mbona huo ugumu wa hali hauonekani. Nilidhani utasema watu hawahudhurii mikutano yao, au kura ya maoni ya REDET imeonyesha hivyo kumbe ni porojo tu za kutumia masaburi kufikiria uonekane upo. Mgombea wa CUF ameishawaambia wana igunga wasimpigie kura kwani kuna chama kimeleta maendeleo MAKUBWA toka uhuru wakipigia, huku hao waliopata hayo '' Maendeleo Makubwa'' huko Igunga wanahitaji chakula cha msaada, na CCM inatumia hizo njaa zao kujinufaisha
 

uko dunia ipi Nape hatakiwi Igunga, anatibua maslahi ya mafisadi, wenye ccm yaani mafisadi wanadai chanzo cha rostam kuachia ngazi ni Nape wala si uzito wa GAMBA. Nikuulize nani muhimu kwa JK na Mkama ni Rostam au Nape, usijibu leo!!!!!!!!
 

YAWN YAWN YAWN!!!!

 
Hata wapigania haki wengi walipata uzushi wa kipuuzi ili kuwakatisha tamaa, Mandela alikuwa akiitwa gaidi lakini leo hii ni hero, time will come utajuwa CDM ni hero na liberal wa nchi hii nawe nawe mzushi utageuka kupiga makofi na kuwapongeza ufisadi wa RA muulize Msemakweli ana nyaraka zake za Kagoda
 
Kwa kiasi kikubwa Nape hafiti kwenye hiyo timu alichaguliwa bahati mbaya kwa sababu ya hali ya 'upepo' akielewa hili atakaa 'nao' vizuri.Kwa misimamo aliyoonyesha toka lile sakata la ujenzi wa jengo la UVCCM ni wazi hakufaa kuwa kwenye hii timu ya sasa ya hiki chama ikiongozwa na watu walewale, afu eti anataka kuja na spidi mpya ni ngumu sana kupenyeza chochote kizuri lakini kikiwa kina madhara kwa 'wenye' chama na ubaki salama.Wacha tuvute subira tuone hizi sarakasi za mara gamba,siasa uchwara na sasa hii mikwara inaishia wapi..
 


Upumbavu hauna bei!
 
Hivi ninyi watu wa CDM mnataka tu successful stories from CDM tu? Mbona mnakuwa kma sio wasomi? Msomi wa kweli ni yule anaetazama pande zote mbili, kusikiliza na kuchambua maoni ya pande zote mbili...wengi wenu mliochangia kwenye hii thread hamkuchukua hata dk 2 kuprove kama kuna ukweli katika taarifa hii badala yake mnakurupuka kuponda habari hii!

Mimi co wa CDM wala nini wala siko Igunga lakini nashangaa kila inapoletwa habari mbaya kuhusu CDM mnang'aka lakini ikiletwa habari mbaya kuhusu CCM na vyama vingine mnafurahia.

Hii inaonyesha wazi kuwa wengi wenu sio positive thinkers bali ni washabiki wa vyama vya siasa TENA Chadema!!!! Kwa bahati nzuri hatuombi tickets kuchangia mada hapa...so mtegemee critizism kutoka upande mwingine na sio habari ya kufurahisha CDM pekee!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…