Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
<br />Mkapa huwa anatumia neno moja tu linalowakilisha wapinzani, KOKOTO. Huyu mzee namkubali sana.
Boniface Meena na Geofrey Nyang'oro, Igunga
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimewawekea pingamizi wagombea ubunge kupitia vyama vya Chadema na CCM kwa madai kuwa hawakurudisha fomu kwa kufuata kanuni na sheria za uchaguzi. Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Msimamizi wa Uchaguzi, Magayane Protas alisema ametupilia mbali pingamizi hilo."Mgombea wa CUF, Ndugu Mahona amewasilisha pingamizi dhidi ya wagombea wa Chadema na CCM akidai kuwa walirudisha fomu kinyume cha sheria. Lakini nimeangalia sheria inavyoeleza na kuona hawakufanya kosa lolote wakati wakirudisha fomu hivyo, nimelitupilia mbali pingamizi hilo."
CHADEMA Kuzindua Kampeni Igunga Leo
Chadema kinatarajia kuzindua kampeni zake rasmi leo. Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa chama hicho, Waitara Mwita alisema kuwa watawapokea viongozi wa kitaifa kwa maandamano kuanzia saa 6:00 mchana ili kuelekea kwenye eneo la mkutano katika Uwanja wa Sokoine.
"Tutaanza maandamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa na wajumbe wa kamati kuu pamoja na wabunge na mkutano utaanza saa 8:00 mchana na kumalizika saa 12:00 jioni," alisema
Chanzo: CUF yakwama kuvizuia CCM, Chadema Igunga
Ningekuwa sina akili ningepata GPA ya 4.0?
Mkapa huwa anatumia neno moja tu linalowakilisha wapinzani, KOKOTO. Huyu mzee namkubali sana.
<br />Magwanda kama kawa, siasa za maji taka. Kumbe wanaenda Igunga kuongelea watu na si sera!
wakiongozwa na katibu mkuu wa chama hicho Seif Sharif Hamad wakiwa na magari zaidi ya 30 na pikipiki zaidi 100 na umati wa watu waliotembea kwa miguu, huu ni mwanzo wa kuashiria kuanza kwa kampeni hapo kesho.
Leo igunga imezizima japo police walimwagwa kila kona lakini wanainchi wamejitokeza, kweli wanainchi wanataka mabadiliko, macho na masikio yetu tunasubiri hapo tarehe 2/10/2011 tuone ni nana atakaye nyakua kiti hicho.
Mtoaji wa habari ni mgeni ambaye nipo hapa igunga kwa shughuli ya kikazi
al jamaacuf_al_ islam
polisi wanafungua jalada la malalamiko (RB) katika kituo chao wenyewe cha polisi .. duh hii kali