issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,788
- 5,217
Siipendi CCM na viongozi wake. angalieni uongo wa gazeti la uhuru
Mkapa atikisa jimbo la Igunga
Friday, 09 September 2011 12:15 newsroom
WAKATI ujio wa Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa, ukitikisa wilayani Igunga, vyama vya CHADEMA na CUF vimezidi kuingia kwenye mgogoro. Msafara wa Mkapa uliwasili wilayani hapa jana kwa njia ya barabara na kupata mapokezi makubwa, huku wananchi wakiacha shughuli zao na kujitokeza kumlaki.
Awali, Mkapa ambaye ujio wake umekuwa mwiba kwa wapinzani, alipokewa na viongozi wa CCM, wanachama na wananchi katika kijiji cha Makomero, nje kidogo ya Igunga. Baada ya kuwasili katika kijiji hicho, msafara wa Mkapa ulisimama kwa muda ili asalimiane na wana-CCM na wananchi waliojitokeza.
Mkapa aliwaeleza amekwenda Igunga kukamilisha kazi moja tu, ambayo ni ushindi kwa CCM. Mkapa atazindua kampeni za mgombea ubunge wa CCM, Dk. Peter Kafumu, kesho kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Rostam Aziz, aliyejiuzulu.
"Nimewasili Igunga na wana-Igunga kazi iliyopo mbele yetu ni moja, ni ushindi tu," alisema huku akishangiliwa. Alisema anaona fahari kubwa kufika Igunga kwa njia ya barabara, tena ya lami na kwamba, mara ya mwisho alipita ikiwa ya vumbi. "Nafarijika kufika hapa kwa kutumia barabara, haya ni maendeleo makubwa jamani," alisema.
Mkapa aliwaasa wananchi wa Igunga kujitokeza kwa wingi Oktoba 2, mwaka huu, kumpigia kura mgombea wa CCM, Dk. Kafumu. Alisema kwa kufanya hivyo, wananchi watakuwa wamechagua maendeleo na kuachana na wapinzani, ambao hawana sera. "Kuna mengi ya kuwaeleza tutakapokutana kwenye mikutano yetu ya kampeni, lakini mfahamu kuwa kura zote kwa Dk. Kafumu," alisema.
Baada ya kusalimiana na wana-CCM hao, msafara wa Mkapa uliingia mjini ukiongozwa na waendesha pikipiki na baiskeli, zilizopambwa kwa bendera za CCM. Msafara huo ulizunguka katika mitaa mbalimbali ya mjini wa Igunga na kuzidisha hofu kwa wapinzani, ambao wamekuwa wakimhofia kiongozi huyo mwenye historia nchini. Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika katika viwanja vya Kumbukumbu ya Samora, ambapo leo Mkapa atakuwa na shughuli mbalimbali za kichama.
CHADEMA, CUF ‘watoana roho'
Wakati kivumbi cha kampeni kikianza kutimka jimboni humu, vyama vya upinzani vinavyopambana na CCM, vimeanza kuingiwa na kiwewe huku CHADEMA kikiwasilisha malalamiko polisi ya kufanyiwa fujo na wafuasi wa CUF na kutaka hatua za haraka zichuliwe kabla hali haijawa mbaya.
Kupitia barua yenye kumbukumbu namba CDM/W/IG/UCH/VOL.5/2011, Katibu wa CHADEMA wilayani Igunga, Christopher Saye, aliiomba polisi kuichukulia hatua CUF kwa madai kitendo hicho kikirudiwa kinaweza kuvuruga amani.
CHADEMA imedai Jumanne iliyopita wafuasi wa CUF waliwafanyia fujo wakiwa katika harakati za kurejesha fomu za mgombea wao.
Walidai wakiwa katika msafara wa kurejesha fomu, magari ya CUF yaliyokuwa yameegeshwa jirani na ofisi za CHADEMA yalianza kupita katikati ya msafara wao.
Kutokana na madai hayo, juzi Msimamizi wa Uchaguzi huo, Magayane Protace, alilazimika kuwaita wawakilishi wa CHADEMA na CUF na kuwakemea kutokana na vurugu hizo.
Kwa upande wao, CUF wamedai shutuma zilizotolewa na CHADEMA kwamba CUF ndiyo waanzilishi wa vurugu ni za uongo na zenye lengo la kuupotosha umma.
Last Updated ( Friday, 09 September 2011 12:57 )