Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
tumetenganishwa na milima, mabonde, wilaya na mikoa, mlioko igunga tupeni hali halisi uwanja kujinadi, chenkapa yu hali gani, tunasikia baadhi ya watu waliobebwa na kuletwa igunga kwa mafuso wamekosa chakula, eti mwigulu amekalia fungu, alikuwa bize kwenye kikao na chenkapa, je ni kweli?
 
Inaonesha jinsi gani chadema hawakurupuki kama nyie magamba wanaongea fact tupu,nabado
 
Sasa nyinyi mlitaka ajivunie kushona magwanda?
 

tawi la UDOM lililofunguliwa na NAPE hili, hahahaaa...!
 
Ndege ilipoanza kuruka juu jamaa akalia Mama yangu...iliporuka tena juu zaidi akasema Mungu wangu..Ilipopaaaa zaidiiiiiiiii na zaidiiiiiii jamaa asema MAWEEEEEEEE....Sasa Chadema inapaaa na mtasema Maweeeeeeeee.....PEOPLES POWER
 
<br />
<br />
Kweli cdM Balaa, kazi ya polisi wafanye wao!
Kwa kutumiwa kwake na kufanywa kipofu na Vijisenti vya Nape itafika mahali atawalaumu CDM kwa kushindwa kumfunga Rostam Azizi mpaka sasa hivi!
 
huko ndiko kumpigia kampeni kafumu? kweli huyu mukapa hajui kupiga kampeni ndiyo maana alikuwa akiuzwa kama ndizi na Mwalimu Nyerere mwaka 1995.
Yaani Jamii forum members in kiboko cha njia hata kama ulikuwa na msongo wa mawazo kwa kukosa lishe na maisha magumu utacheka tuu,ilike this comment
 
Jifanye wewe ni Mkapa na kampeni umemaliza kwa kujidai na Chadema wameshinda.Utajisikia je???
 
Sasa nyinyi mlitaka ajivunie kushona magwanda?
Magwanda manake saa ya ukombozi ni sasa sasa Mkapa bin Kiwavi,bin mchwa,bin komba,bin panya maliza vyote wananchi watatjijua wenyewe atafanyaje
 
dah,
watu kweli wabunifu,
hiyo kitu imetulia sana.
Watu wana vipaji sana,
sema basi tu serikali yenyewe ndio hii isiyojali raia wake kwa kuweka mazingira mazuri kwa watunzi kama hao.

bendera yako ya kula na kurarua...nimeipenda..chama chako nataka kadi....
 
CCM wameshajichokea. Wanatapatapa tu. Nimemdharau sana Mkapa, amekubali kulazimishwa kwenda kujidhalilisha bure! Inabidi waandae Malori ya kutosha kuwabeba watu na pesa za kuwalipa wapanda baiskeli na Pikipiki vinginevyo yanaweza kumkuta ya Rungwe kujikuta anahutubia Matairi.
Namwonea huruma sana huyu baba.
 
Itakumbukwa kuwa Mkapa alitua jana Igunga, huku matangazo yakipita kote Mjini Igunga kuhamasisha watu kwenda kumpokea. Nilikuwa najaribu kujiuliza, je hii ilikuwa ni kimkakati kuwagawa watu au ni coincidence tu?

Kama siyo hivyo je kulikuwa na ulazima wa yeye kutua jana? Kama ni ndio, je kwa kuwa Mkapa ni Rais mstaafu wetu sote (ukiondoa ile kuwa ameenda kama mpiga debe mkuu wa mgombea wa chama shindani na kile kilichokuwa kinazindua kampeni jana), na kwa kuwa taratibu zinasisitiza kutoingiliana kwenye maeneo ili kuwapa muda na fursa watu wa maeneo husika kusikiliza sera na makusudio ya wagombea wao, je huoni kuwa CCM walikuwa na nia mbaya ili kudivert attention ya watu ili wasiende kwenye mkutano wa CHADEMA? Lakini tukiacha hayo, unadhani walifanikiwa kwa kiasi gani? Na kama sivyo hii inaashiria nini kwa wana CCM na mgombea wake?

Naomba tujadili
 
ni nani Timamu wa kusimama mbele ya CDM pale ccm ?
 
Baada ya kumaliza madili yao ya kuuza migodi na madini yetu bure kwa wazungu sasa wanasaidiana kutafutiana ulaji bungeni siyo?? Nafikiri jitihaza za Mkapa siyo bure. Labda anataka aende huko ili akaongeze nguvu iwapo mambo yataibuliwa bungeni huko mbeleni.

Naomba kuuliza, hivi Mkapa alishawahi kumpigia nani mwingine kampeni zaidi ya JK?? So what is so special about this man??? Is he doing this for CCM, Igunga, himself or this guy???
 
kweli debe tupu haliachi kutika

karibu marwa
 
Tumia akili kidogo, Chadema walimwambia nani kwamba wanakwenda Igunga kuzungumzia Kagoda? Hata kama ni muhimu kulizungumzia, je ilikuwa lazima kulizungumzia kwenye ufunguzi wa kampeni?
Wewe ndiye uliyetaka lizungumziwe lakini zingatia kuwa akili yako wewe si ya Chadema.
 
Najiuliza hivi uchaguzi wa jimbo la Igunga,CCM wanapeleka majeshi kiasi hicho ni nini wanachoogopa,Manake according to CCM 'maendeleo waliyoyafanya' wananchi wanaona sasa nguvu yooote hiyo ya nini??

Napata majibu ya haraka-haraka mawili kwamba hawana uhakika wa hilo jimbo kurudi CCM au hakuna walichofanya Igunga(kama Chama/Serikali) kiasi cha kujivuna.Acheni kupoteza rasilimali nyingi kwa ajili ya uchaguzi elekezeni hizo fedha kwenye shughuli za maendeleo muone kama mtahitaji kuita wastaafu wasaidie kampeni za kajimbo kamoja.Wana Igunga mmepewa nafasi ya kuamua kuanza safari ya kupiga hatua mbele kuelekea kwenye maendeleo au kupiga hatua nyuma kuelekea kwenye umaskini.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…