Hata mimi Lazima ningejitahidi kuhudhuria mkutano huo, lau nisikie maajabu haya makubwa, Rais mstaafu ambaye nakumbuka katika utawala wake wote wa miaka 10, hajawahi kulala Igunga hata siku moja, mara zote amelala Tabora au Nzega ikitokea, sasa leo kapiga kambi kabisa.. hiki ni kituko namba moja.. kama nakosea wadadisi msisite kunisahihisha.. kituko cha pili nakumbuka kipindi cha kampeni zake mara nyingi amezungumzia ujenzi wa "Daraja la Mbutu"ambalo mpaka leo ni wimbo, pamoja na ujenzi wa brabara inayounganisha Tabora na igunga kupitia Ipuli kwa kiwango cha changarewe safi hatimae Lami, kisha ujenzi wa barabara ya Tabora hadi Nzega kwa lami, ahadi ambazo hazijatimizwa hata moja, Barabara zote hizi hazipitiki, hazina mashimo bali mahandaki, Tabora Igunga ni mwendo wa KM 203, ila utachukua zaidi ya masaa matano au sita kwa gari ndogo. sasa natarajia kusikia kaka Benja ataongea nini Leo juu ya haya, na LAZIMA AJIBU MAANA WAPIGAKURA WANA DATA ZOTE, UKIWALAGHAI WATAKUSTAHI ILA WATAONYESHA HASIRA ZAO TAREHE 2 oCT.
Zaidi ya yote maskini ya Baba wa watu sijui atasema nini juu ya jamaa aliyejiengua..Rostam, sijui atamsifia au kumsilibia, sipati picha.. aa sijui atasemanini juu ya mafisadi , sijui atajibuje hoja za wapinzani juu ya meremeta na mengineyo. Kwa kweli kazi ipo. au sijui atajidanganya kwamba watanzania bado ni walewale mambumbumbu kwamba wanaendeshwa kwa nguvu za Pesa na ubabe.. au anadhani atawahadaaa wananchi asiwape majibu yaliyojaa shibe na mantiki wamuelewe kwa kunyoosha dole gumba juu.. ah labda aendE na "ILE KITU", Watanzania wa sasa Wadadisi, wanasikiliza redio, wanasoma magezeti, wanaangalia tv..(kupitia cm za kichina).. sijui kama watadanganyika kirahisi tena..
Kama Hakuna Hoja zenye shibe stahiki kwa wakazi wa Igunga, nashauri mzee wetu bora usithubutu kuongea, sikukatishi tamaaa, bali nakwambia kweli manake unaweza kuambulia aibu. kampeni si muwaachie walioko madarakani wanaochakachua mambo kila kukicha. Endapo CCM Itashindwa, tafsiri yake ni kwamba wewe Mzee wetu Mkapa utakuwa umeshindwa, watanzania wamedhihirisha hasira za maumivu yao kwa kipindi chako cha utawala, na utachujika sana, hata ile sifa yako ndogo ya kubana matumizi ya serikali itayeyuka.
Ni mtego wamekuwekea wenzako, ushindwe uaibike..STUKA!!