Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Kubeba watu kwenye malori utafikiri ng'ombe wanapelekwa mnadani au buchani!!!!

Kama wana wathamini wapiga kura basi wakodishe mabasi yenye heshima.

Ajali ikitokea lori likianguka jee, itakuwa maangamizi.

Watu wa igunga, msikubali kupanda malori, ni hatari

Hata mimi Lazima ningejitahidi kuhudhuria mkutano huo, lau nisikie maajabu haya makubwa, Rais mstaafu ambaye nakumbuka katika utawala wake wote wa miaka 10, hajawahi kulala Igunga hata siku moja, mara zote amelala Tabora au Nzega ikitokea, sasa leo kapiga kambi kabisa.. hiki ni kituko namba moja.. kama nakosea wadadisi msisite kunisahihisha.. kituko cha pili nakumbuka kipindi cha kampeni zake mara nyingi amezungumzia ujenzi wa "Daraja la Mbutu"ambalo mpaka leo ni wimbo, pamoja na ujenzi wa brabara inayounganisha Tabora na igunga kupitia Ipuli kwa kiwango cha changarewe safi hatimae Lami, kisha ujenzi wa barabara ya Tabora hadi Nzega kwa lami, ahadi ambazo hazijatimizwa hata moja, Barabara zote hizi hazipitiki, hazina mashimo bali mahandaki, Tabora Igunga ni mwendo wa KM 203, ila utachukua zaidi ya masaa matano au sita kwa gari ndogo. sasa natarajia kusikia kaka Benja ataongea nini Leo juu ya haya, na LAZIMA AJIBU MAANA WAPIGAKURA WANA DATA ZOTE, UKIWALAGHAI WATAKUSTAHI ILA WATAONYESHA HASIRA ZAO TAREHE 2 oCT.
Zaidi ya yote maskini ya Baba wa watu sijui atasema nini juu ya jamaa aliyejiengua..Rostam, sijui atamsifia au kumsilibia, sipati picha.. aa sijui atasemanini juu ya mafisadi , sijui atajibuje hoja za wapinzani juu ya meremeta na mengineyo. Kwa kweli kazi ipo. au sijui atajidanganya kwamba watanzania bado ni walewale mambumbumbu kwamba wanaendeshwa kwa nguvu za Pesa na ubabe.. au anadhani atawahadaaa wananchi asiwape majibu yaliyojaa shibe na mantiki wamuelewe kwa kunyoosha dole gumba juu.. ah labda aendE na "ILE KITU", Watanzania wa sasa Wadadisi, wanasikiliza redio, wanasoma magezeti, wanaangalia tv..(kupitia cm za kichina).. sijui kama watadanganyika kirahisi tena..
Kama Hakuna Hoja zenye shibe stahiki kwa wakazi wa Igunga, nashauri mzee wetu bora usithubutu kuongea, sikukatishi tamaaa, bali nakwambia kweli manake unaweza kuambulia aibu. kampeni si muwaachie walioko madarakani wanaochakachua mambo kila kukicha. Endapo CCM Itashindwa, tafsiri yake ni kwamba wewe Mzee wetu Mkapa utakuwa umeshindwa, watanzania wamedhihirisha hasira za maumivu yao kwa kipindi chako cha utawala, na utachujika sana, hata ile sifa yako ndogo ya kubana matumizi ya serikali itayeyuka.
Ni mtego wamekuwekea wenzako, ushindwe uaibike..STUKA!!

Gazeti la mwananchi limeeleza kwa kirefu leo kuhusu maandalizi makubwa yaliyofanywa na ccm jana kuhusu kufanikisha uzinduzi wa mgombea wao leo.Waandishi wa gazeti hilo wameenda mbali zaidi na kutabiri mkutano wa ccm leo utavunja rekodi ya mikutano yote kuwahi kufanywa ktk uwanja wa sokoine.Kama vile haitoshi waandishi wa gazeti pendwa la mwananchi pia wamerudia taarifa ya mapokezi ya mkapa juzi ambapo wamesema alilakiwa na umati mkubwa wa watu kuwahi kushuhudiwa.Source habari kuu Mwananchi leo.

kwa sasa chanzo changu cha kuaminika cha habari kuhusu chama changu cha chadema ni JF

Wakati mwingine siasa za Kiafrika zinachusha (Boring) hadi inafikia wakati unaona ni bora turudi kwenye enzi zile za Kisultani na Kitemi au tuwe na madikteta wanaotutawala.

Igunga kuna uchaguzi mdogo unafanyika. Tangu CCM walipopost CV za mgombea wao hakuna la maana nililoambua litakalonisaidia kuelewa kinagaubaga ni nini hasa wagombea wa vyama vyote wanataka kuwafanyia wana Igunga. Marekani Obama na wapinzani wake wanashindana ni jinsi gani wanavyoweza kuongeza ajira na kuondokana na naksi ya kibajeti (Budgetary Deficit) hapa kwetu tunashindanisha kujaza watu kwenye mikutano hata kama kwenye mikutano hiyo hakuna la maana linaloongelewa.

Nilidhani CCM ni chama kikongwe kitaonyesha tofauti na vyama vingine lakini nacho hakuna kitu. CDM nayo pamoja kujaza wasomi sijaona ni nini wanachosimamia huko Igunga. Cha ajabu nguvu ya wagombea wote haitokani na hoja zao bali nguvu ya kuvungavunga (manipulation) ya vyama vyao.

Hivi nani anaweza kutuchambulia wagombea wote mmoja mmoja wanasimamia nini kwa wana Igunga na wao kama wagombea tarajio lao kwa Igunga ni lipi. Tofauti yao inajengwa na nini?

Tafakuri yangu:

Bado tuna safari ndefu sana kufikia lengo letu la kuibadili nchi yetu iwe imejaa viongozi ambao wanashabihiana na falsafa ya jamvi hili.

Sijaona chama cha kuvunja rekodi ya chadema, Leo Mkapa asubili aibu au wakodishe mabasi yasombe watu.

mie napita tu.. naangalia hoja.. Ukishamtambua mtu anaemwaga utumbo.. hata hupotezi kusoma thread zake, mfano mwita25, wala sitasoma chake chochote.. Mnisamehe ila lazima niwe muwazi jamani.. naskia uugwana kitendo.. Pia ni nimeandikiwa sms kwamba baadhi ya JF senior member wameshapewa karanga ili wajitose kujibu hoja... aibu jamani.. inasikitisha ingawa taarifa sijazithibitisha.. tuzichunguze..

Kiufupi CCM ndio imetufikisha hapa!! na tumeichoka, ngoja tuwang'oe kwanza halafu ndi tuijenge tanzania tunayoitaka. Hata hao wamarekani unaowasema uksefu wa ajira ndio umepamba moto huk na madeni ndo hayashikiki.

Toa CCM kwenye ubongo wako na tutafika tu.

hayawi hayawi sasa yamekuwa

Ccm leo siku ya tarehe 10/sep/2011 inategemea kuzinduwa kampani ya chama chao juu ya uchaguzi wa ubunge kwa kiti kilichoachwa na RA

Inasemekana Mzee Mkapa ndiye atakaye unguruma na kuamsha hisia za wana igunga

vipi kuhusu vyama vingine yaani CDM na CUF?

Mwananchi pia limepata mamilioni ili liusaliti umma?

uzuri tuna JF na yote haya yalishaandikwa hapa kuhusu mpango wa CCM kununua waandishi wa habari kwahiyo
hakuna jipya ila tusikilizie makamanda waliokuwa kwenye Ground hao ndio wa kuwasikiliza.

@Source ya habari hiyo ni Gazeti la Mwananchi la leo, bahati mbaya sana. Gazeti hilo liameandika kishabiki sana na kupotosha hata ukweli halisi, japokuwa lilitaka kubalance kwa kuweka matukio 2 tofauti kwenye habari moja. @Na hapa ni baadhi ya kasoro za upotoshaji wa habari hiyo: 1/Heading: "Makada wa CCM wasaka wapambe mitaani" (Mwandishi amesahau kuwa makada, wanachama & wapenzi wa CCM, wao ndio wapambe wa chama chao. Ni vipi tena waende mtaani kusaka wapambe? ) 2/Hakukuwa na maandamano bali kulikuwa na shamrashamra za muziki&burudani mitaani (Maandamano must address specific topic & walks toward specific point of gathering, unless yawe maandamano ya kushinikiza jambo). Akasahau kuwa siyo sera wala utamaduni wa CCM kufanya maandamano. Japokuwa CCM wanaweza kufanya maandamano kuiga wapinzani wao!! 3/Hakukuwa na taarifa yoyote (Ukiondoa gazeti la Uhuru) kuwa Mkapa alipokelewa na umati mkubwa wa watu alipofika Igunga, na hata pale aliposimama kusalimia wanaCCM palikuwa ni mahali maalum ambapo chama kulishafanya maandalizi kabla, kila mtu akijua kwamba Mkapa atafika hapo kuwasalimia. Na si kweli kwamba kulikuwa na umati wa watu pale, infact was not surprise to Mkapa &any one else there. 4/Mwandishi ameonyesha ushabiki wa wazi pale ulipokuwa akitaka kulinganisha shamrashamra hizo kuwa ni dalili ya kuja kufunika kampeni zilizoanza kufanywa na wapinzani. Nadhani hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo, ili kuepusha hisia za wasomaji juu ya upande unaoupigia debe.

Katika kile kinacho aminika kuwa Taasisi za dini ziajiingiza ktk siasa, Waisalamu huko Igunga wamewakatalia nyumba ya kupanga CDM kwa madai kuwa nyumba hiyo ilisha ombwa na CCM taarifa zinasema kuwa CDM walifika wakaomba nyumba hiyo inayo milikiwa na dini ya Kiislaamu wakakubaliwa na wakalipa kodi Tsh. 70000/= ya muda wote watakao ishi huko Baadaye Imamu akaja akaweka kufuli la SOLEX juu ya kufuli la CDM akisema nyumba hiyo iliombwa na CCM Habari zina pasha zaidi kuwa kila wanako omba nyumba za kupanga CDM wanaambiwa zilisha ombwa na CCM

source : Radio Ushindi

nawasilisha

KWANI UNAPATA NINI KUTOA TAARIFA ZA UONGO KAMA HIZII? shame on you

mwandosya jr. Na wewe unapata nini kusambaza upupu wa propaganda dhidi ya wapinzani ndani na nje ya chama katika sura ya uenezi?

Katika kile kinacho aminika kuwa Taasisi za dini ziajiingiza ktk siasa, Waisalamu huko Igunga wamewakatalia nyumba ya kupanga CDM kwa madai kuwa nyumba hiyo ilisha ombwa na CCM taarifa zinasema kuwa CDM walifika wakaomba nyumba hiyo inayo milikiwa na dini ya Kiislaamu wakakubaliwa na wakalipa kodi Tsh. 70000/= ya muda wote watakao ishi huko Baadaye Imamu akaja akaweka kufuli la SOLEX juu ya kufuli la CDM akisema nyumba hiyo iliombwa na CCM Habari zina pasha zaidi kuwa kila wanako omba nyumba za kupanga CDM wanaambiwa zilisha ombwa na CCM

source : Radio Ushindi

nawasilisha

Kwa hiyo hakuna hata mwana CDM aliyejitolea kupangisha nyumba yake kwa chama chake? na kama nyumba zote za Igunga ni za wana CCM basi ni halali yao kukataa, hapo kwa ufupi ni kwamba CDM haikubaliki Igunga.

KWANI UNAPATA NINI KUTOA TAARIFA ZA UONGO KAMA HIZII? shame on you

Kwani jamani, Nape Moses Nnauye, si ndiye yule aliyeibua sakata la mkataba feki wa UV-CCM akitetea haki ya Baraza Kuu la umoja huo kuona na kuridhia au kukataa mkataba alioita wa kinyonyaji. hali iliyoungwa mkono na Rais JK ambaye amemwagiza Katibu Mkuu Yusuph Makamba miaka hiyo ya 2008, kusimamia kupitiwa upya kwa mkataba huo kwa kuwa hauna maslahi kwa umoja huo. ambaye kwa hoja yake hiyo aliundiwa zengwe na KAMATI ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), na kumzawadia alama “E” inayoonyesha kuwa wamekataliwa kugombea uongozi kwa kuwa “ana dosari.” Ila kijana akakweakwea tukasikia akawa mkuu wa wilaya huko kusini, baadae tukaskia amekuwa Kaimu mwenezi wa CCM bara (sijui ni kweli manake wengine twaweza kosea kutamka vyeo vya watu),
Sasa watanzania mmemfanya nini kaka wa watu, mbona anatukana ovyo-ovyo jamani, inasikitisha sana kwa kiongozi kuropoka matusi. Ni kweli kwamba wanadamu wote tuna simile ya kukasirika ila tunajizuia kutukana, seuze kiongozi, mwenye stahiki aliyekasmiwa madaraka na Chama KIKUBWA kwetu kumwaga matusi hadharani, ni aibu sana.. kama kuna uwezekano namshauri aiondoe post yake haraka kabla wengi hawajaisoma.. unajua watu wakishaisoma, haiondoki vichwani mwao, watakudharau na kukuona holela. mie sijui amepatwa na nini Nape, Mbona hakuwa hivyo!! mie nimestuka sana, au ulevi wa madaraka, au fedha au nini tena kaka yetu ambaye wazazi wetu walikuwa sambamba kwa pamoja na Mwalimu.. Please back to square one, if not toka kwenye chama kinachokuharibu.. we still need you.. true..

Gazeti la mwananchi limeeleza kwa kirefu leo kuhusu maandalizi makubwa yaliyofanywa na ccm jana kuhusu kufanikisha uzinduzi wa mgombea wao leo.Waandishi wa gazeti hilo wameenda mbali zaidi na kutabiri mkutano wa ccm leo utavunja rekodi ya mikutano yote kuwahi kufanywa ktk uwanja wa sokoine.Kama vile haitoshi waandishi wa gazeti pendwa la mwananchi pia wamerudia taarifa ya mapokezi ya mkapa juzi ambapo wamesema alilakiwa na umati mkubwa wa watu kuwahi kushuhudiwa.Source habari kuu Mwananchi leo.
ni kweli gazeti hilo limeandika hivyo. sasa unatakaje??
kuandikwa hivyo na gazeti ndo faraja yenu ninyi ccm, wengine faraja yetu ni kuona tunaungwa mkono live live na watu maelf na sio kwa kupika propaganda.
kama ni hivi mbon hukuandika habari ya gazeti la mtanzania daima kua chadema imeiumbua ccm igunga??
ua just a walking dead body, you are waiting for your fall.
hiki kizazi hatuwataki na hamtaweza kutulazimisha tuwatake.

Ukiona hivyo ujue ushindi upo karibu maana yake haiwezekani unyimwe wakati sio hatari. Ila ninasikitika kuona dini zinatumika kisiasa hii inabidi wabadilike

Kwani nani kasema ni lazma waishi kwenye nyumba? waende na hema wafanye camping kama yule mfadhili wa zamani wa Iddi Amini kutoka Tripoli.

Aluta continua!😛eace:

udini huu...ngoja tuone utatufikisha wapi, kama vp waombe nyumba za wakristo, kwani wakristo hawana nyumba huko igunga??

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom