Wakuu,

Wengi tumeshangaa Rais mtaafu kupanda tena jukwaani, kwa kawaida tulikuwa tumezoea kuliona Tingatinga la CCM (Samweli Malecela) kuwa front na kukata kata magogo, mizizi, miamba na miti ili kuchonga barabara.

Cha ajabu namwona Mkapa naye anapiga front Igunga, ndiyo najiuliza VIPI HILI NDIYO TINGATINGA JIPYA LA CCM ? kama kweli hili limetengenezwa toka China, Japan au Ujerumani? Je litahimili misukosuko ya miamba ardhini na kusonga mbele?

Binafsi watu tunamuheshimu sana huyu Rais wetu katufanyia mengi sasa kupanda jukwaani ni ishara kuwa sasa anataka mashambulizi yote ya kiasiasa yaanze kuelekezwa kwake? Je bado anaweza purukushani za kisiasa za majukwaani? Je atavumilia makombora toka kwa vijana wa CHADEMA? hatakasirika?

Tunamkaribisha sana igunga ila asije akatuambia sisi vijana tunamkosea adabu maana kaingia mwenyewe ulingoni kwa mara nyingine tena.

MY TAKE: CCM acheni wazee wapumike, kulikuwa hakuna haja yoyote ya kumsumbua mzee wa watu, kashawatumikia wananchi miaka 10 akiwa rais na mingine mingi tu. Huu ni muda wake wa kupumzika. Kama Mmewakosea wananchi na mna uhakika hawatawapeni kura angalieni mlipojikwaa lakini si kuwasumbua wazee wetu. Mtamponza mzee wa watu.