Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
mkuu sijazungumzia kabisa kuhusu uchumi wa Marekani kama sehemu ya mada yangu. ukichunguza nilichokizungumzia ni tofauti ya misingi ya mijadala kati yetu na Marekani. wao wanazungumzia masuala muhimu ya jamii yao na sisi kazi yetu ni kuonyesha chama kipi ni kizuri au kibaya kuliko kingine kama vile chama kinaweza kuwa na watu wazuri tu au watu wabaya tu.Mtu unalinganisha apple na chungwa? Sasa masuala ya uchaguzi Igunga na uchumi wa Marekani yanahusiana nini? Hueleweki kabisa mkuu.
Sarah pallin na wenzake hawasemi Democtras wooote ni wabaya bali wanasema Obama kashindwa kuitoa Marekani kwenye anguko la uchumi kwa sera zake za kishoshalist. Nilitarajia kuona kampeni zilizojaa uchambuzi yakinifu badala yake kila chama kinajitahidi kupuliza "vuvuzela" lake la propaganda kama vile Igunga imezaliwa jana.
CCM imekuwa ikitawala Igunga kwa miaka yote tangu 1992, Imefanya kitu gani wanachojivunia ili wapewe tena ubunge wa jimbo la Igunga baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kutoka chama hicho hicho kujiuzulu. Hizi gharama tunazoingia watanzania kwa kufanya chaguzi mbili chini ya mwaka mmoja hazijasababishwa na CCM?
CDM,CUF na vyama vingine vimewekeza kiasi gani kwenye jimbo la Igunga hadi tuamini navyo pia havina tofauti na CCM? Wakati wote msimamo wangu ni kwamba siasa za kishabiki haziwezi kutufikisha popote. Take my word, leo hii Lowassa au Mwakyembe wakiamua kujiunga na CDM amini usiamini wtapokelewa kama mashujaa walioachana na Mafisadi. Kwani ilikuwaje kwa Mpendazoe na Shibuda?







