Unajisikia vibaya! I know. Lakini mkuu do again your calculations, the opposite might be true. Kwamba Ccm haters wanaweza kuwa converted na kuwa Ccm lovers just to have something in common with their favourite commedians. Love that huh...
Hakika unachokisema ndio sahihi kuwa CCM kwa sasa ndio wako kazini kuakikisha wale wote wnaoichukia CCM wageuke kuwa waumini wazuri wa CCM.Na hilo limekuwa hivyo ukizingatia hata humu ndani ya JF watu wamekuwa na chuki ya dhahili juu ya CCM el maalufu humu jamvini kama wanamagamba..
Sipendezwi na siasa za kuona kuwa hakuna watu wazuri ndani ya CCM,na kuwa ni lazima kila jambo sasa liwe ni upinzani tuu,no hiyo siyo sahihi,ili Nchi iende kwenye mstari tunawaitaji wote chama tawala na vyama upinzani,leo hii CCM wakiwa upinzani chadema wakawa chama madaraka CCM wataonekana wa maana kwa mujibu wa mapungufu ambayo CDM watayaonyesha na uhitaji wa matakwa ya umma.
Lakini kinachoendelea sasa haters wamekuwa mbele hata kwa mambo ambayo ni kwa faida ya Taifa na sio ya Chama.Ndio CCM wanamadudu yao lakini sio kuwa sasa kila jambo watu watengeneze chuki isiyo na msingi.Tutashindwa kutofautisha tofauti hiko wapi,itafikia hatua wananchi wataamua ni heri ya zimwi likujualo alikuli likakwisha.
Yani ili kwa lugha nyepesi ni afadhari ya kubaki na CCM hii ya sasa kuliko kuchagua chama ambacho ujui kesho itakuwaje.Na hili swala itabidi wana JF ambao baadhi yao wana mapenzi na chama cha CDM, watumie uchaguzi mdogo wa Igunga kubadilika na kuwa na mikakati [strategies] humu ndani za kisayansi na sio kuwa na ushabiki wa kupinga na kumwaga matusi kwa kila kitu,vinginevyo tunakokwenda uenda wakatengeneza aina ya usindikizaji wa kudumu na kuanza kupoteza credit kwa kada ya waelewa kusupport movement yao.
Ebu tuwe wazi humu ndani wapenzi wa JF ni wangapi wanachama au wapenzi wa CCM uwa wanalusha madongo ya kuwakejeri wanaCDM humu ndani ukiachia FF ambae anajulikana kwa misimamo yake ambayo imeegemea kuchallange zaidi na kujenga mjadala uweze kuleta tofauti ya mawazo lakini hayuko kukejeri kiivyo.
Binafsi nimeshaweka msimamo wangu wazi Tanzania Mbele, kwangu Nchi kwanza vyama baadae,hivyo ni ukiwa mwana CDM kwangu poa,ukiwa CCM mwake,ukiwa CUF kama kawaida,hivyo kila mmoja atizame kuwa kwa zama hizi tuanze kujenga uungwana wa vitendo na maneno kwa kuwa fito wanazopigania CDM,CCM au CUF ni kwa ajili ya ujenzi wa Nchi inayoitwa Tanzania.
Vyama hivi vishindane kwa
HOJA kumjenga MPIGA KURA NA KUKUSANYA WAPENZI NA WANACHAMA WA KUWAUNGA MKONO.Ni vyema pia CDM waanze kutoa elimu ya kwa wapenzi na wanachama wao jinsi ya kuwa na muonekano
[behave] ambao unabeba sura ya kichama kwa kila mmoja ambao kwa jumuiko lao ndio tunapata taswira ya kundi ambalo ndio chama kwa ujumla wake.
Tukiendelea kuona matusi ya kuwakebehi wana magamba kuliko mikakati ya kuibua mapungufu na changamoto za kuwafungua masikio yao Wananchi kuwa UPINZANI una sababu zote za kuaminika hakika itakuwa ni hadithi na malalamiko yasiyoisha wanaiba kura na maneno kadha wa kadha yasiyo na tija na ufanisi.
Ukiwaangalia CCM uwa wanabolonga kwelikweli,lakini ninachowakubali wakigundua kosa lao hakika CCM uwa ni wepesi sana kujirekebisha kimya kimya tena chini kwa chini ikibidi hata kwa kukopi mbinu ya adui wao lakini wao cha msingi wa win mapenzi yao kwa wananchi wao.Kwa sasa wameeanza kuwa na ustaarabu wa kauri hata kwa viongozi wao,ambao walio wengi walikuwa na busara.CDM viongozi wana ustaarabu wa matumizi ya maneno lakini wapenzi wake na wanachama wamekuwa na lugha za matusi na kejeri kwa wingi sana na kwa mfano mkubwa ni ndani ya JF.
Please tunawategemea CDM,kuleta changamoto kwa CCM na CUF ambao ni vyama tawala,kwa mambo haya tufika kweli mpaka CDM kuwa chama tawala uko tunakokwenda.Kwenye Red ni hakika hesabu mpya zinatakiwa