Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo
Status
Not open for further replies.
Mkuu Mzee wa Rula asante sana kwa picha lakini naomba sana uongezee na hii
Huu msosi mpaka baada ya miaka mingine mitano. wasidhani wanakula bure, ccm wajanja sana lazima wananchi watalipa hii chakula, na itawagharimu kwa muda wa miaka mitano. chadema hatuna pilau, the comedy, wala hata maji ya kunywa lakini watu wanajaa uwanjani.
Kimsingi hapa mtoa thread kamwaga upupu.Nashindwa kuelewa uwezo wake wa kupambania pumba na mchele.Ukiona mtu anakumwagia pumba we fungasha virago vyako uishie
Mi kuna thread moja nimesoma jana usiku km saa sita hiv inasema mwita 25 kapigwa ban na moods, ss inakuaje tena?
kila unapotokea uchaguzi mdogo najikuta namkumbuka Halima Mdee
yeye peke yake alizungumza kitu cha maana kuhusu hizi chaguzi ndogo...
alisema chaguzi ndogo zinapoteza muda na pesa nyingi
ni bora ukawekwa utaratibu wa chama kinachoshikilia jimbo hilo
kuchagua ni nani arithi jimbo......
hakuna anaesikiliza haya,but huu ndo ukweli mtupu....
hizi chaguzi ndogo its a waste of time and money.....
zipigwe marufuku......
cho
Mimi ndiyo kinachonishangaza, yaani siasa ya bongo kuna kipindi ni kama hadithi za mahoka, yaani ni ngumu kuelewa anachukia kwa kumananisha!
Jamani RA hakuacha Ubunge kwa kuchukia gutter politics ila walimtega Lowasa na Chenge ili wapate pa kupumulia lakini wakakuta ma mvi an ngozi ngumu kuliko gamba anapasua tu na wao wakawa wamesha mtoa kafara RA. JK na CCM kwa pamoja mkakati wao umeshindwa kabla hawaajaanza .Ndiyo maana unamuona Rostam yuko hapa anakula matapishi yake this is typical CCM maana huwezi kuwa mmember wao wa juu hata wa chini kabla hujawa kichaa.
Nimeipenda ile picha yenye bango linalowataka CDM wapeleke fujo zao Arusha na Kilimanjaro. Wakamalizia...KURA HATUWAPI!
Saafi sana.
Aisee hii ni hatari kumbe licha ya kutoa tshirt na kofia huwa wanatoa na mpunga..kweli ccm ni ya kuogopa kama ukoma. Kwa jinsi hao watoto wanavyoonekana wanyonge mbele ya hizo sahani za ubwabwa itatuchukua muda sana kuikomboa hii nchi.
Rostam nakupongeza kwa moyo wa kuthubutu kuwepo tena kwenye medani za siasa, kama sikosei kilichokuondoa ccm NI SIASA uchwara. Vipi leo uwe msatari wa mbele kumpigia kampeni mtu aingine kwenye shimo la siafu wa siasa uchwara? au ndiyo changa la macho? au ndiyo kusema akili kichwani?
Duh!hii noma sasa.
Sidhani kama kuna wataalamu, kuna waganga njaa walioamua kuganga njaa kwa kukaa darasani mda mrefu, mwisho wanakuja kufanya yale yale ambayo hata ambaye hakumaliza std VII anafanya na 'yes sir' nyiingi.
Ongeza na hizi picha:
View attachment 36990
Hii chupa ya Mwenyekiti Mbowe imejazwa nini? inafanana na wiski.
Nashawishika kusema kuwa chupa ya maji imetumika kuficha kilevi!
Hwa nao vipi? Wanamuiga mwenyekiti wao?
Hivi CDM hawawezi kufanya kampeni bila ulevi wa kupindukia? Matokeo yake ni kumwagia tindikali watu wasio na hatia.
WAKATI UMEFIKA KUKOMESHA HUU UHUNI NA KUWAADHIBU KWA KUWANYIMA KURA.
Reactions: Omr
Kama CCM itashinda igunga, mimi nitaomba mwongozo kwa madocta wa milembe waje wawapime hawa watu.
Mkuu mbona hawa si wanyamwezi?
Mkuu hao ni wanyamwezi original bila chenga. CCM wanaendeleza utamaduni wao wa kuwadanganya watanzania kwa vitu vidogo.
Lazima tutambue kwamba ni kweli wananchi wana njaa, na wanahitaji chakula, lakini ni jinsi gani utawawezesha ili wakaondokana na matatizo ya njaa kama hawatawezeshwa?
Mfano hapo watakula, wakishiba wataondoka na baadaye watasikia njaa tena.
Namkumbuka mwalimu Nyerere aliwahi kwenda Marekani kumwona Rais Jimmy Carter akamwomba Carter amsaidie chakula kwa kuwa watu wake wana njaa, Carter akamsaidia. Lakini mwaka uliofuata Nyerere kafanya hivyo hivyo, hapo Carter kamwuliza mbona Tanzania ina rutuba nzuri kwanini kila mwaka njaa? Carter akamwambia Nyerere "Nikikusaidia leo na kesho utarudi tena"
Akamsaidia wataalamu wa kilimo kutoka canada na nyerere hakurudi tena kwa Carter kuomba mahindi.
t-shirt, kofia, kanga na chakula ya siku moja na mateso, manyanyaso, dhiki na njaa ya miaka mitano. Jamani hii ni dhambi na laana mbaya kuliko..
Inasikitisha, hapo ccm wanatumia njaa ya baadhi ya wanaIgunga kuhitaji kura kwa nguvu. Lakini wakumbuke kuwa kesho wakishindwa kuwapa hicho chakula itajakuwa ni zahma, walitakiwa wawape pembejeo za kilimo na wataam ili kuwaletea maendeleo. TANZANIA VITA NI LAZIMA, na hayo ndo maandalizi yake. THINK.
Yap, yamewakuta. Wengi wa wananchi waliokwenda kwenye mkutano wa ufunguzi Chicm Igungwa walikusanywa. Vijana walikusanywa kutoka vijiji mbalimbali wakapewa uniform labda na posho. Ndo waliojaza mkutano.
Mbaya zaidi, wananchi wakaanza kuondoka. Sababu za kuondoka ni kuwa ccm haina jipya, Hao wananchi waliohojiwa na gazeti la mwananchi walisema ndio serikali inakusanya hela, mbona hakuna maendeleo??
Source: Mwananchi Paper, page 4.
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…