Angalieni kauli za Chenkapa akimsifia matonya kwa safari zake za kuombaomba (ikiwepo kuomba suti)
MWENYEKITI mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa amezindua kampeni za chama hicho jana katika uchaguzi mdogo wa Igunga na kuwataka wananchi kumchagua mgombea wa chama hicho na kuwakanyagakanyaga wapinzani.
Akizungumza huku akijibu vijembe vya wapinzani hasa Chadema kwa kuainisha maendeleo yaliyofanyika Igunga na Tanzania kwa ujumla, Mkapa alisema kauli za wapinzani kuwa tangu Uhuru hakujafanyika kitu ni kufuru na hawawatendei haki waasisi wa Taifa.
Alifafanua kuwa asingesemea suala la vyama hivyo kukebehi maendeleo yaliyofikiwa kwakuwa wanajidhalilisha wenyewe, lakini amelazimika kulizungumzia kwa kuwa wanadhalilisha nchi.
Kabla ya kumtambulisha mgombea wa CCM katika uchaguzi huo, Dk. Peter Kafumu kuhutubia wananchi hao, Mkapa alianza kujibu hoja zinazoelekezwa kwake na kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu safari za nje, sera ya ubinafsishaji, elimu, afya na maji.
*Safari za nje za Rais Kikwete
Mkapa alisema Rais Kikwete anakwenda nje kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania na kutafuta mitaji, ujuzi na utaalamu ili nchi ibadili rasilimali zake kuwa utajiri wa wananchi wake wakati vyama vya upinzani na vyenyewe vikienda nje ya nchi, lakini kutafuta ruzuku za vyama kwa ajili ya maandamano.
"Ukimpata atakayekuja na mtaji, utaalamu wapate stahili zao na sisi wenye rasilimali zetu tupate stahili yetu," alisema.
*Sera ya ubinafsishaji
Mkapa alisema Serikali ilikuwa na uchumi wa Dola ambao karibu kila kitu mpaka bucha vilikuwa vikimilikiwa na Serikali lakini wananchi walikuwa wamefungwa mikono.
"Tukasema hapana, tufungue mikono wananchi wajiletee maendeleo," alisema Mkapa na kuongeza kuwa katika sera ya ubinafsishaji, kati ya mashirika karibu 300 yaliyobinafsishwa, sera hiyo inaweza kulaaniwa kwa kushindwa kwa mashirika mawili tu; Shirika la Reli (TRC) na Shirika la Ndege (ATC).
*Elimu, afya na maji
Mkapa alisema yeye alipokuwa akienda shule, alikwenda akiwa peku na alilazimika kulala njiani tofauti na sasa ambako shule ziko nyingi na wanafunzi si tu, hawaendi shule peku, bali wanakwenda na baiskeli.
*Rostam amuombea kura Dk.Kafumu
Naye Rostam alipopewa nafasi ya kuwasalimu wananchi hao, alisema amekwenda katika kampeni hizo kwa shughuli moja ya kumuombea kura Dk. Kafumu.
Source: Habari Leo aka Udaku