Inawekana ikawa vigumu kuamini, lakini ni kweli imetokea kwenye mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za CCM jana jioni, ilipofika zamu ya mgombea ubunge wa CCM kujieleza na kuomba ridhaa ya wananchi, alimpandisha Mke wake jukwaani na kusema "MNAMUONA HUYU? HUYU NDIE MKE WANGU, MAMA KAFUMU, ALINICHAGUA MIMI NIWE MUME WAKE, KWA HIYO NA NYINYI NYOOTE FANYENI HIVYOHIVYO!" Nadhani kwa kila aliehudhuria hawezi kubisha, sasa wengi wetu tusio na ushabiki wa kupitukia tulipigwa na butwaa, yaani sijui alikuwa anataka kutufanya nini sijui, maana kama ni hao wake zetu na dada zetu wamtake yeye Kama alivyotakwa na mkewe, yenyewe ni balaa tosha, lakini sisi wanaume wenzake, marijali tuliokamilika sijui ametuweka kwenye fungu gani? Namuomba Dr Kafumu afanye uungwana kidogo atuombe radhi kwa kejeli hiyo, kwani na sisi pia tuna wake zetu waliotuona tunafaa wakatuchagua.