ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,938
- 6,942
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, kimesema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, na mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wassira ameitwa kwenda Igunga ili kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo.
Hayo yalielezwa jana wilayani Bunda na Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka wilayani hapa katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda.
Alisema Wassira atakwenda Igunga kuongeza nguvu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, utakaofanyika hivi karibuni.
Chama hicho tawala katika uchaguzi huo kimemsimamisha Dk Dalaly Kafumu, ambaye atapambana na wagombea wa vyama vya upinzani.
"Wassira atakwenda Igunga na tutahakikisha jimbo hilo linarejea CCM, kwani tayari chama chetu kimejipanga vizuri na ni chama chenye sera zinazotekelezeka," alisema.
Aidha, mwenyekiti huyo wa CCM mkoani Mara, alisema kuwa chama hicho mkoani hapa, kimejipanga vizuri ili kuhakikisha katika uchaguzi mdogo utakaofanyika katika kata tatu za Jimbo la Rorya, ambazo madiwani wake walijiuzulu na kata moja ya wilayani Serengeti na moja ya wilayani Tarime kinapata ushindi wa kishindo.
Aliongeza kuwa hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Jimbo la Musoma mjini ambalo liko Chadema litarudi CCM.
Akichangia katika kikao hicho mjumbe mmoja Athumani Mambo, alisema kuwa CCM kumchagua Wassira kuwa mmoja wa wapiga kampeni katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, ni jambo la msingi sana kwani Wassira anao uwezo mkubwa wa kushawishi wananchi.
Aliongeza kuwa katika uchaguzi mkuu uliopita, Wassira alisababisha majimbo mengi ya mkoani Mara, kuchukuliwa na chama hicho, ikiwa ni pamoja na Jimbo la Tarime ambalo lilikuwa chini ya Chadema.
Kwa upande wake Wassira ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, alisema kuwa Jimbo la Igunga litakuwa la CCM, kwa sababu wamejipanga vizuri na kuweka mikakati madhubuti, kuhakikisha ushindi unapatikana.
swali langu je, kweli ccm wamekosekana watu wakuokoa jimbo la Igunga au maji yamezidi unga?
mwacheni akapige zake usingizi. na itakuwa kila akisimamishwa ili kuongea na wananchi, watu wa igunga watakimbia mbio kali kwa kuogopa SURA YAKE INAYOFANANA NA FARU wa porini