Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, kimesema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, na mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wassira ameitwa kwenda Igunga ili kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo.

Hayo yalielezwa jana wilayani Bunda na Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka wilayani hapa katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda.

Alisema Wassira atakwenda Igunga kuongeza nguvu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, utakaofanyika hivi karibuni.

Chama hicho tawala katika uchaguzi huo kimemsimamisha Dk Dalaly Kafumu, ambaye atapambana na wagombea wa vyama vya upinzani.

"Wassira atakwenda Igunga na tutahakikisha jimbo hilo linarejea CCM, kwani tayari chama chetu kimejipanga vizuri na ni chama chenye sera zinazotekelezeka," alisema.

Aidha, mwenyekiti huyo wa CCM mkoani Mara, alisema kuwa chama hicho mkoani hapa, kimejipanga vizuri ili kuhakikisha katika uchaguzi mdogo utakaofanyika katika kata tatu za Jimbo la Rorya, ambazo madiwani wake walijiuzulu na kata moja ya wilayani Serengeti na moja ya wilayani Tarime kinapata ushindi wa kishindo.

Aliongeza kuwa hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Jimbo la Musoma mjini ambalo liko Chadema litarudi CCM.

Akichangia katika kikao hicho mjumbe mmoja Athumani Mambo, alisema kuwa CCM kumchagua Wassira kuwa mmoja wa wapiga kampeni katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, ni jambo la msingi sana kwani Wassira anao uwezo mkubwa wa kushawishi wananchi.

Aliongeza kuwa katika uchaguzi mkuu uliopita, Wassira alisababisha majimbo mengi ya mkoani Mara, kuchukuliwa na chama hicho, ikiwa ni pamoja na Jimbo la Tarime ambalo lilikuwa chini ya Chadema.

Kwa upande wake Wassira ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, alisema kuwa Jimbo la Igunga litakuwa la CCM, kwa sababu wamejipanga vizuri na kuweka mikakati madhubuti, kuhakikisha ushindi unapatikana.

swali langu je, kweli ccm wamekosekana watu wakuokoa jimbo la Igunga au maji yamezidi unga?

mwacheni akapige zake usingizi. na itakuwa kila akisimamishwa ili kuongea na wananchi, watu wa igunga watakimbia mbio kali kwa kuogopa SURA YAKE INAYOFANANA NA FARU wa porini
 
kwani igunga kuna bahari? hilo jahazi linasafirishwa kuelekea dar na gari gani? si wapeleke polisi tu na bunduki..... teh teh
 
Nimeangalia kura za maoni kwa jimbo la Igunga kwenye site ya mwanahalisi, ingawa kura hizi hupiwa na Watanzania wote lakini pia inawapa taswira hawa wanaojiita wamiliki wa nchi (CCM) jinsi waTZ walivyochoshwa na Uzemba na udhalimu wao.


Kwa leo: 09/09/2011

Leopold Mahona (CUF) 4%


Joseph Kashindye (CHADEMA) 89%



Peter Kafumu (CCM) 6%



Said Makeni (DP) 1%



Lazaro Ndageya (UMD) 0%



John Maguma (SAU) 1%



Total votes: 305



Kwa matokeo zaidi bofya hapa: Gazeti la MwanaHalisi


Labda mimi sijui hesabu kwa kuwa nilifeli,lakini hebu jaribu kujumlisha hizo asilimia jumla zinakuwa ngapi?
 
Umetumia jina zuri sana TINGATINGA Mkapa sasa linataka kusafisha KOKOTO za Magwanda.
 
ha ha ha ha kazi kweli kweli, CCM hawato tuachia nchi yetu salama bila kuwanyanganya kwa nguvu ya umma, kila la heri kwa wana upinzani woote
 
Labda mimi sijui hesabu kwa kuwa nilifeli,lakini hebu jaribu kujumlisha hizo asilimia jumla zinakuwa ngapi?

Kwa wale wanaofahamu hesabu kidogo, ni kwamba:

John Maguma (SAU) 0.78% approx. 1%

Said Makeni (DP) 0.8% approx. 1%
 
@Malecela ameshindwa kwenda Igunga kwa sababu za kiafya na umri umeanza kumtupa mkono, lakini nasikia pia hataki kutumiwa tena kama "Tingatinga" kwani alifanya hivyo zamani lakini viongozi wenzie hawakuona thamani ya mchango wake kwenye chama (Hasa baada ya kumwekea zengwe mara 2 kwenye hatua za awali za kinyang'anyiro za urais 1995 & 2005) @Inatia huruma&kusikitisha sana kuona CCM kinafanya maamuzi yaliyokosa busara tena bila kufanya utafiti wa kutosha kuhusu Mkapa kuwa mpiga debe wa CCM Igunga. Kwa kifupi Uwepo wa Mkapa huko Igunga hautaongeza chochote kwa CCM, Zaidi unawapa nafasi wapinzani wake kupata la kuongea & kujiongezea umaarufu kutokana na kashfa kubwa zakutisha zinazomkabili Mkapa. Hivyo basi CCM wajiandae vyakutosha kumsafisha pia wakati na baada ya kampeni kwisha. Bahati mbaya gharama ya kumsafisha ni kubwa sana & sidhani kama inawezekana. Lets wait&watch the cinema...
 
Siku zote namfahamu Mwita wa Ukweli ambaye ni Mwita Maranya. Hiyu Mwita25 ambaye anaye shangazi yate Mbeya si Mwita kimeo kweli ilichakachuliwa????

Umetumia jina zuri sana TINGATINGA Mkapa sasa linataka kusafisha KOKOTO za Magwanda.
 
Huku hali si nzuri, CDM inaona aibu kuwajuza mlio mbali nje ya Igunga. Walifikiri mteremko, mpambano hapa ni CCM na CUF vyama vingine vimekuja kushiriki na si KUSHINDANA.

Acha uongo wewe una magambo usoni ndio maana huoni!!!
TBC1 jana walionyesha mafuriko ya wana-CDM pamoja na kufichaficha lakini bado ulionekana!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa kusoma tu hii thread nahisi kusinzia, ngoja nisepe zangu tusije ambukizana bure am not belong to magambaz




A friend of my enemy is my enemy too
 
yeye pekee ndie wameona at least bado ana mvuto ndani ya chama.
 
Mkuu, umeona mbali sana.
You deserve to be who you are.
Mkapa anaenda kupambana na zitto, mr. Two na mnyika. Hiyo ni akili au matope?
Anaenda kusema ccm imejenga lami dar to mwanza....my bad.
Wakulima wa pamba, karanga na warina asali wao wamefanyiwa nini?
 
Siku zote namfahamu Mwita wa Ukweli ambaye ni Mwita Maranya. Hiyu Mwita25 ambaye anaye shangazi yate Mbeya si Mwita kimeo kweli ilichakachuliwa????
<br />
<br />
Kwa ujinga wako unafikiri wakurya hawaruhusiwi kuishi Mbeya?
 
Kila mtu aombe mungu wake hiyo laana ipishe mbali tuchague CDM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom