Picha za Uzinduzi wa kampeni jimboni Igunga[/h]
Hizo ni baadhi ya picha ambazo zimepatikana leo katika uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM jimboni Igunga.
Rais Mstaafu Ndg Benjamini Mkapa akimnadi mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM Ndg Dr. Kafum.
Sehemu ya umati uliohudhuria mkutano huo.
Kama kawaida wasanii wa Original Komedi walikuwepo kusherekesha uinduzi huo.
Baadhi ya vijana wakirudisha kadi za CDM baada ya Mkapa kumwaga sumu.
Katibu mkuu Ndg Willson Mkama anaonekana akisisitza jambo katika uzinduzi huo. Awali ilidhaniwa asingehudhuria.
Hapo awali ilidhaniwa Rostam asingehudhuria uzinduzi wa kampeni za kumtafuta mrithi wake, swali sijui siasa uchwara zilizomuondoa amezisamehe.
Rostam na Mkama wakionekana wakifuatilia kwa umakini uzinduzi huo, siasa kazi kweli kweli.
Bango hili mmmm utalisemea mwenyewe.
hapo wengi wanaonekana walikuja kuwaangalia the orijino komedi. Hao vijana wanaorudisha kadi ni wanaccm walioandaliwa na magamba kana kwamba ni vijana wa chadema wanajiunga ccm, ili kutaka kuwapumbaza wana mageuzi.