Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
changamoto je, mtaweza kuwashawishi mambumbumbu kukichagua chama chenu?!
Get smart daugg...

inahotaji kukaza moyo na kujikita katika kuwaelimisha na kuwafanya wawe consciouse. Lakini ccm wana mbinu nyingi mno na chafu kuhakikisha suala hili halifanikiwi. Mfano ni matajiri kutishiwa maisha yao au biashara zao iwapo hawataisaidia ccm.

Mwanza tajiri mmoja aitwaye gachuma mmuliki wa hisa karibu 70 za serengeti na hisa karibu 25 za cocacola amefuatwa na rostam, naye yuko igunga kusaidia kampeni za ccm.

kila unapotokea uchaguzi mdogo najikuta namkumbuka Halima Mdee

yeye peke yake alizungumza kitu cha maana kuhusu hizi chaguzi ndogo...

alisema chaguzi ndogo zinapoteza muda na pesa nyingi

ni bora ukawekwa utaratibu wa chama kinachoshikilia jimbo hilo
kuchagua ni nani arithi jimbo......

hakuna anaesikiliza haya,but huu ndo ukweli mtupu....

hizi chaguzi ndogo its a waste of time and money.....

zipigwe marufuku......

A political or economic analysis?

hii ya watu kurudisha kadi za vyama vya upinzani tulishaizoea. Inabidi watafute propaganda nyingine. This is a very old trick.

kweli kabisa bubona, wanakununulia kadi, wanakupa, wanakulipa pesa ufanye usanii, kwao haya mambo ni ya kawaida.

igunga chadema iko juu kwa mtaji huu,ccm wanajisiriba kinyesi chao wamepanga watu wamsifu mtu waliyemtuhumu kwa miezi nane wakimuita gamba
4.jpg

aliyetoa tofasiri ya siasa ni mchezo mchafu, tufikirie kumpa credit.

Haingii akilini mtu ambaye ametuhumiwa kuwa chanzo cha ccm kufanya vibaya uchaguzi 2010, akatakiwa ajiuzulu nyazifa zake zote, akijiuzulu kwa masikitiko makubwa tena kwa kutoa kashifa nzito za .'.....kuchoshwa na siasa' uchwara......leo hii anashiriki siasa zilizo mnyanganya donge lake, inatisha.

Lazima kuna 7bu za kiuchumi anazozilinda.

"we are ruled, governed, controlled and our actions being decided by what we call social facts, which are external to indivudual but coercive to him/her".

We also call it the system

kila unapotokea uchaguzi mdogo najikuta namkumbuka Halima Mdee

yeye peke yake alizungumza kitu cha maana kuhusu hizi chaguzi ndogo...

alisema chaguzi ndogo zinapoteza muda na pesa nyingi

ni bora ukawekwa utaratibu wa chama kinachoshikilia jimbo hilo

kuchagua ni nani arithi jimbo......

hakuna anaesikiliza haya,but huu ndo ukweli mtupu....

hizi chaguzi ndogo its a waste of time and money.....

zipigwe marufuku......

kama wananchi wa jimbo la uchaguzi wanapewa fursa ya kuchagua mbunge wao mwingine inapotokea mbunge wao wa sasa amejiuzulu , ikiaminika kwamba huenda wameshabadili msimamo wao kuelekea chama kilicho kuwa kinashikilia jimbo, je tume ya uchaguzi haioni haja ya kuwapa wananchi kumpima na kumtathmini mbunge wao kila miaka miwili kama anafaa kuendelea ama la.! Kama hawaridhishwi naye wachague mwingine, maana baada ya uchaguzi tu wabunge huwa wanajisahau kupindukia.!

Andiko zuri, lakini metaphor ya Hitler sio sahihi.
Nilitaka kuonyesha kwamba hata Hittler kama si kutumika kwa nguvu za ziada hata yeye kuna watu ambao mpaka dakika hii wanaamini kwamba alikuwa yuko sahihi kwa aliyoyafanya. Hata CCM inatakiwa tushikane mikono ili nguvu yake ya ushawishi iishe kabisa!

Mkuu,

Tunaposema haingwi mkono wewe pia usikosee kutuelewa, nani kakwambia bondia aingiapo ulingoni kupambana husema atapingwa japo ngumi moja, au unadhani hajui kuwa mpinzani wake atarusha makonde. Hivyo basi unaposikia 'ccm haiungwi mkono' wewe malizia na neno hili 'na watanzania wengi' kuliko kuanza kuwatishia watu yakwamba ..........watakuwa wajinga kumbe wewe ndiyo umefikiri ndani ya box. Soma picha kwenye post #6, utatafuta mpaka kwa tochi hukuti cdm inawarubuni watu kwa peremende ili wakawasikilize.

CCM haina ubavu wa kuitisha mkutano igunga au sehemu yoyote isijifiche nyuma ya ze comedi, tot, usafiri na ubwabwa wa kumwaga, usijaribu kujenga hofu kwa wapiganaji wako, wajasiri wataku fire friendly, ndugu jamaa na marafiki wakaishia kukuombea u-rip.
Hata mimi najua ni wengi hawaiungi mkono CCM, lakini uhalali wa CDM unatakiwa uwe wa kimantiki na wala si wa kimazingira. Ukiwa na watu wawili wabaya watu watamchagua aliye nafuu zaidi kwa mwenzie, CDM kwa sasa inakubaliwa kwa sababu ya Mning'ino (hang over) ya CCM kutawala kama chama dola kwa muda mrefu.

Ninachotaka ni CDM kujijenga kwa falsafa yake na si kwa kutegemea udhaifu wa CCM. Leo CCM wakiwashitaki wale mafisadi na kubadili mifumo yake ya undeshaji mambo 'COme 2015" kazi itakuwa kubwa kwelikweli kwa CDM. Soma bandiko la mwanakijiji "CHADEMA 2010" utaelewa nini ninamaanisha. Vitani si mitulinga pekee inayotawala bali inahitajika mikakati (Strategies) iliyoegemea kwenye uhalisia na Lojistiki za kiukweli.

Huyu Mkapa apuuzwe tu kwanza yeye siyo Mtanzania, yeye ni raia wa msumbiji na kabila yake ni m'meto.

Akili matope hizo! Kwani CDM na CUF hawajagawa Tshirts huku Igunga! Acha hoja za kijinga jana CUF walikuwa wanagawa TSshirt na kofia kwa vijana the same CDM walifanya majuzi so tuite nini kwa hawa wengine? Mnachekesha sana watu wazima mnafikiri kwa kutumia masaburi.....

Kumbe huyu Kafumu ni MUKAKA, loo wana Igunga mumekwisha kama mna bisha mchagueni muone, ameshajifunza tabia mbaya za kimombasa huyo mwogopeni.

Akili matope hizo! Kwani CDM na CUF hawajagawa Tshirts huku Igunga! Acha hoja za kijinga jana CUF walikuwa wanagawa TSshirt na kofia kwa vijana the same CDM walifanya majuzi so tuite nini kwa hawa wengine? Mnachekesha sana watu wazima mnafikiri kwa kutumia masaburi.....

Nape ndugu, watu wanaomboleza we unatoa mitusi.

Hii ni madhara ya ccm kuwaingiza watu wasio wanasiasa kama wafanyabiashara, professionals mbali mbali nk kwa kigezo cha pochi zao ktk siasa. Unategemea nini?

Ulichokizungumza ni kweli kabisa wana cdm tusijibweteke maana kuna watu wapo vijijini huwezi kuwaambia kitu kuhusu ccm, inatakiwa wana cdm tusilale na kujisahau elimu kwa wanajami inatakiwa ili wajuei nini maana ya ukombozi wa kweli.

Unajua kwa wale tumekulia vijijini tunajua kwamba Tshirt, Khanga na Kofia ni kitu adimu mno, kwa hiyo mtaji mkubwa wa CCM ni ufukara wa watu.

Kule vijijini Pilau / Ngoma ni dili kubwa sana, pia chama kinachokwenda na magari mengi ya kifahari ni mtaji mkubwa maana wananchi wanapenda kuangalia chama kipi kina manjonjo na si Sera, CCM pia wanatumia mbinu ya kupeleka wasanii ili kuvuta watu kwenye mikutano yao, kutumia vijana wa bodaboda kuhamashisha vijana wenzao huku wakipata buku kumi na mafuta full tanki bure.

Haya yote ndugu zangu huwa yana mwisho wake ingawa yanachukua muda sana - ila kwa sasa yanawasaidia na yameshawasaidia sana CCM kushinda katika chaguzi mbali mbali na siwezi kushangaa nikisikia Igunga pamoja na hayo yote yaliyotokea ya ujivuaji magamba wao wakashinda tena.

Taratibuu elimu ya uraia inaanza kuwaingia na baadhi wameanza kuelewa haki zao za msingi.

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom