Hivi mtu anayetembea kifua wazi, mwanamke asiye hata na nguo za kuendea hospitali, sokoni akipewa kanga, fulana, kitambaa cha kichwani au kofia hivi vitu vinaashiria nini?
Nimewahi kuzunguka na kuwaangalia watu wakivitumia hivyo vitu katika siku za kawaida ambazo haziwatambulishi na ushabiki wa siasa bali kama vazi rasmi la kutokea. Kwa hiyo kwa mtu ambaye ni maskini kabisa kama ilivyo watanzania wengi wa vijijini ambako CCM hujitia inakubalika nguzo yake kubwa ni umaskini wa wa Watanzania na ugawaji wa vitu kama khanga, fulana, vitambaa vya kichwani na kofia ambazo hutolewa zawadi kwa wapiga kura na si kwa wanachama wake.
Tungependa waandishi wa habari wafanye uchunguzi kugundua hizi khanga na vitu vingine ambavyo hutolewa ikiwa ni pamoja na chakula vinaathiri kiasi gani mwenendo wa upigaji kura?
Bahati mbaya tuliyonayo ni kuwa PCCB na Tume ya Uchaguzi vyombo ambavyo vinawajibu wa kisheria kupiga vita rushwa katika uchaguzi ni kama idara maalum na zisizo halali za CCM