Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Hizi ama kweli ni siasa uchwara cha msingi ni hoja ya mtu sio udhaifu wa mwingine. Ndio maana siku zote nasema siasa ya bongo hazina mwelekeo wowote watu wanaacha kujadili shida za wananchi wa Igunga wanaanza kusema sijui yule ana nini na huyu yukoje.
 
Nakumbuka kuna kipindi aliulizwa kuhusu kashfa zake akasem akuwa ameshastaafu siasa naona sasa amerudi labda anafikiri tumeshasahau maovu na madhambi yake mabaya aliyoifanyia nchi hii. by the way naunga mkono kuwa CCM IMEISHIWA MPAKA KUMTUMIA STEVEN WASIRA NA MKAPA WATU WALIOCHOKA NA HAWANA MVUTO WOWOTE.
 
attachment.php

attachment.php


kweli inaungwa mkono kama vichochezi ndio hivi hatutafika
 
Jamani tunaomba mtuwekee magazeti angalau yanayojaribu kuwa fair angalau kidogo usitulete hapa gazeti liloandikwa na nape na mhariri akiwa kikwete mwenyewe.

Soma Tanzania Daima; Gazeti la Chadema
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"] [TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD] CHADEMA yatikisa Igunga
• Mkapa avuna aibu, apata watu ‘kiduchu’

na Salehe Mohamed na Mustafa Kapalata, Igunga



[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff, align: center"]
amka2.gif

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD] KATIKA siku ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga, jana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitikisa mitaa na vitongoji vyote, huku mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, akitangaza rasmi kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) ni janga la kitaifa.

Uzinduzi huo ulianza kwa maandamano yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi wa CHADEMA walioupamba kwa vifijo na nderemo, kuanzia saa 9.20 alasiri, wakiongozwa na magari, baiskeli na pikipiki zilizopambwa na rangi za bendera ya CHADEMA.
Viongozi wakuu wa chama hicho, akiwamo Mbowe, Dk. Willibrod Slaa, na wabunge wa CHADEMA walipokelewa na umati wa wana Igunga na kuongoza maandamano yaliyoanzia kijiji cha Hanihani hadi Uwanja wa Sokoine, ulikofanyikia mkutano mkubwa wa hadhara.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
kwani hujui kama wasukuma ukiwapa ubwabwa kama huo na maandazi umemaliza kula ni issue kanda ya ziwa, yaani wanapenda sana kula ndio shida yao kubwa na mlo ndio njia peekee ccm wanaisjua na wanaitumia hasa tabora uelewa wao bado ni mdogo sana.
siyo wasukuma wa siku hizi wewe...chadema kwa wasukuma ina wabunge zaidi ya watano bado UDP...wasukuma walisahaulika sana kielimu wakalia kuchunga ngombe ila kwa sasa wanaamka na siku wakiamka wote au wengi wao huu ujinga unaofanywa na CCM itakuwa mwisho...
 
kumbe kampeni zinaendana na chakula au ni sehemu ya shukran?/?
CCM wanarudisha pesa walizo waibia wanainchi wa Igunga...iko siku tutapiga mahesabu tujue imebaki kiasi gani kwao...
 
SIKU moja baada ya uzinduzi wa kampeni za CCM, juzi kutikisa mjini hapa, baadhi ya makada wa vyama vya upinzani wamekiri kwamba ni vigumu upinzani kushinda kiti hicho cha ubunge. Kampeni hizo zilizozinduliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi, zimeibua hisia za wananchi, kutokana na mambo mbalimbali yaliyowagusa. Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa makada wa CHADEMA alisema kuwa walidhani uzinduzi wa CCM ungedoda, lakini imekuwa kinyume cha matarajio yao. Alisema idadi ya watu waliohudhuria katika mkutano huo, uliwavunja nguvu za kuendelea kufanya kampeni, kwani imeonyesha dhahiri jimbo hilo bado ni mali ya CCM. "Sikufichi, pamoja na kwamba mimi naichukia CCM, lakini kwenye hili la uzinduzi halina ubishi, jamaa bado wanakubalika na kweli hapa upinzani tunasindikiza tu, kwani wale watu sio mchezo," alieleza.

Alieleza kwamba pamoja na kwamba uzinduzi uliofanywa na CHADEMA Septemba 8, ulikuwa na watu, lakini ule wa CCM ulifunika mara tatu zaidi, jambo linaloonekana dhahiri kwamba upinzani una kazi ngumu. "Tutajitahidi kuendelea kufanya kampeni, lakini mpaka sasa kama hatutumii hisia za uchama, lazima ukiri kwamba jimbo hili ni la CCM, na ni ndoto kwenda upinzani," alisisitiza. Akijibu swali juu ya kwa nini, hawakuiunga mkono CUF kutokana na mgombea wake kuwa na mtaji mkubwa kisiasa, alisema hakuna msimamo wa pamoja juu ya vyama vya upinzani, ndiyo maana kila chama kimeamua kusimamisha mgombea wake. "Kweli mgombea wa CUF ana mtaji mkubwa kuliko wa kwetu (CHADEMA), na kama tungeungana ni wazi tungewaangusha CCM, lakini bado vyama vya upinzani hatujawa na sauti moja," alikiri.

Source: Gazeti la Uhuru, Jumatatu, Septemba 12, 2011

Katika hali ambayo inadhihirisha kukata tamaa kwa upinzani, juzi akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, alikiri kwamba sio rahisi kuiondoa CCM madarakani, kupitia siasa za mapambio zinazofanywa na baadhi ya vyama vya upinzani.

Mtatiro alikiri kwamba CCM bado ni chama imara, kina nguvu na miundombinu mingi ya ushindi, hivyo bila kutafuta mwafaka wa pamoja wa upinzani haitakuwa na maana.

"Wenzetu CHADEMA mwaka jana hawakusimamisha mgombea na sisi mgombea wetu alipata kura 11,000 tulidhani wangetuunga mkono, badala yake wamekuja kugawa kura Igunga,
"
alieleza.

Baadhi ya wananchi walisema kwamba uzinduzi uliofanywa na CCM na kueleza sera zake, kumewafanya wananchi kuendelea kuwa na matumaini na chama hicho.

"Unajua wapinzani ni watu wa ajabu sana, kila kitu kwao tatizo, hawajui hata historia ya jimbo hili, lilikuwa mwisho kwa maendeleo mkoani Tabora, lakini leo ni wa kwanza, lakini wanasema hakuna kitu kilichofanyika," alieleza Juma Herman.

Herman alisema kwamba wananchi wamekuwa wakitaka kusikia sera za vyama, lakini wanachukizwa na sera za kutukana viongozi wa kitaifa na kupakana tope, kitu ambacho hakiwasaidii wananchi.

"Hivi mtu akisema huyu mbaya, mwananchi anajua ubaya wake nini... ni bora wakaeleza sera na namna ya kuwasaidia wananchi, lakini wao matusi na maandamano, ambayo hayana faida kwetu," alieleza.

Alisema CCM itaendelea kuongoza jimbo hilo na kushika dola kutokana na mikakati yake imara ya kuwaondolea wananchi umasikini na kuwahimiza katika kufanya kazi kuliko kuandamana.

Katika uzinduzi wa kampeni hizo, Mkapa aliwataka wananchi kuwapuuza CHADEMA kutokana na kukosa sera nzuri za kuendeleza nchi zaidi ya kuandamana bila kutoa sera mbadala.

Katika hatua nyingine, baadhi ya vijana wamelaani kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CHADEMA cha kummwagia tindikali kijana mwenzao.

Jacob Maduhu (25) alisema kwamba kitendo hicho kimewasikitisha vijana na imekuwa matusi kwao kutokana na chama hicho kujitangaza kwamba ni mkombozi wa vijana.

"Hivi mkombozi wa vijana anaweza kuwaua vijana, hapana hiki ni chama cha mauaji, huwezi kumuharibia maisha kijana unayetaka kumkomboa kwa kumwagia tindikali," alisema Mahudu.

Naye Salma Hamisi alisema kwamba amekuwa haelewi maana ya nguvu ya umma inayohubiriwa na chama hicho, kumbe maana yake ni kuangamiza umma kwa tindikali.

"Kila siku utasikia nguvu ya umma, hawaelezi sera zao, wao ni fujo na maandamano na kuwapiga wanaopingana nao, hizi ni siasa za wapi, maana waasisi wa taifa walitujengea siasa nzuri, sasa hizi za kumwagiana tindikali si zitatumaliza?" aliuliza.

bila shaka umetumwa wewe. unatumia gazeti la uhuru kuthibitisha uyasemayo?

to me uhuru ni irrelevant source to use, tafuta magezeti ya kizalendo
 
Vichochezi ni vingi sana,wapo pia orijino comedy kuwavutia watu waje ktk ufunguzi wa kampeni za chama cha mapinduzi a.k.a magamba.Binafsi nnakubali hakuna binaadamu anaechukiwa na watu wote,lkn je wanaoipenda ccm na kuiunga mkono ni asilimia ngapi ya watanzania masikini?????
 
Hatushangai taarifa hii kwani ilitegemewa. Kama ilivyoripotiwa awali watu na vikundi mbalimbali yakiwemo magazeti wamemegewa mpango ili ku-cover CCM katika uchaguzi huu mdogo. Umati wa watu walioonekana pale wengi wameletwa na mafuso kutoka sehemu mbalimbali za mkoa na mikoa jirani. Tulimsikia Rais mstaafu akiwanaga wapinzani (hapa ieleweke ni Chadema kwani vyama vingine vyote viko na chama tawala. Rais mstaafu ama anafanya kusudi au alikuwa anajibu mapigo bila utaratibu. Kwamba havina asera mbadala inashangaza kwani uchaguzi wa mwaka jana kama hakuushuhudia alielezwa. Asaidiwe anakala ya ILANI YA CHADEMA apate majibu mahsusiu. anasema vinatoa matusi, kama kuwaambia mafisadi warudishe trasliumali za umma walizopora ni matusi basi hayo ni matusi mazuri yanayosaidia umma wa watanzania ili waondokane na kero mbali mbali zinazowakabili kwa nusu karne sasa. Tupime tunayoambiwa kama yana mashiko au la.
 
mafililiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....i naona uko kazini kama kawa.
cccm ni nouma,misosi,fuso,tindikali,kofia,kanga,tishet,buku tano,fiesta duh!
ile ccm ya nyerere ingekuwepo sijui hii cccm ya ****** ingehamia nchi gani?
mkumbuke na ilani yenu waislamu tunasubiri mahakama ya kadhi kabla hatujapiga TAQBIRRRRRRRRRRRRRRRRRR
 
mimi nimeipenda hiyo picha ya sahani za ubwabwa, maana tumezoea kuhongwa ubwabwa kna baadaye majuto na vilio
 
Kwa siasa za Tanzania hiyo ni kawaida kabisa, mie nafikiri kutopata nafasi hapo pia inasaidia kwa usalama wao mana wana CCM hawaaminiki hata kidogo!
 
hata huko marekani hawarudii rudii chaguzi kwa staili yetu....
mbona kila kitu marekani? huwa sielewi, kuwa wao wako perfect sana au? fanyeni mambo yenu acheni kujilinganisha na watu ambao hamfanini na wala hamuelekeani nao
 
Wewe uko kwenye payroll ya Nepi nini unaona watu wanagawiwa wali na kusombwa na magari unasema inavutia, ukweli kuna vichocheo tu vinavyowavutia watz, ikiwemo Ze Komedi, Wali, buku 2, na usafiri to and from
 
Nilisema jana CDM hawana biashara kama hiyo ni ya CCM muda ukifika watasemana wenyewe kwa wenyewe, tunamtaka na aliyetoa hizo hela awekwe hadharani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom