Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Masikini nape jali ubinadamu kwanza kuliko madaraka kama kweli ulihusika kutoa pesa 150,000/= kwa unyama huu utalipwa hapahapa...............

321642_265761296778624_100000342668655_939079_1865404671_n.jpg

Hii ni laana kwa mungu muumba. Nilisema hapa hii ni shughuli ya ccm katika fani yao ya kutengenezea watu makesi. Hawana ubinadamu kabisa chama chao kimefanana na sura zao, wauwaji wakubwa.

Ninadhani mpaka sasa huko Igunga wanajibu sahihi ni nani kafanya hii kazi ya kumwaribia huyu kijana maisha yake. Hapa watanzania tuelimishane kuachana na mambo ya kinafiki tuwe wakweli. Mimi ninashangaa anzia juzi walitangaza kuwa kuna mmoja alikamatwa lakini mpaka leo hawajataja ni nani. Na angekuwa ni wa chadema ungekuta mabango yamesha andikwa kila kona.

Wanasema ukiwa na mawazo ya kuuwa na kila kitu utakachokifanya kitakuwa cha mauaji tu. Tukianzia na uchukuaji fomu mtoto wa watu kapoteza maisha, kufungua kampeni wenyewe kwa wenyewe wanamwagiana Tindikali, siku hiyo hiyo taifa kupata msiba duh........!. CCM ni mkosi kwa watanzania na ndio maana watanzania hawatakaa wajue kwa nini ni masikini.
 
Tulisha sema watakao mwaga damu za watanzania ni CCM wenyewe si vyama vya upinzani, sasa mnaona wameshaanza ili wachaguliwe
 
Mjadala alioibua Boss hapa ni idea nzuri kufikiria siku zijazo tunapofanya mabadiliko kwenye Katiba ya nchi. Sikubaliani na kwamba aliyeshika nafasi ya pili ndiye achukue kiti kwa sababu inaweza hatarisha usalama wa wabunge wengi.

Maoni yangu ingefaa kama ifuatavyo:
  • Utaratibu wa baadhi ya wabunge kuteuliwa na chombo cha juu kama rais ungeweza chukua nafasi.
  • Ratiba ya vyama vya siasa kupeana nafasi ya uteuzi huo kwa kadiri ya sheria zitakazowekwa.
  • Tume ya uchaguzi kushauriana na wanasheria, Msajili wa vyama vya siasa na wanasiasa ili kujaza nafasi hiyo.
Nchini Marekani inaelekea walishayapata matatizo hayo ndio maana wakaweka sheria ya Gavana wa State kufanya uteuzi baada ya kushauriana na vyombo kadhaa vya kisheria na kisha uteuzi huo hupitiwa na wahusika ili kuthibitishwa, na asipokuwa na kiwango kinachotakiwa anakataliwa.

Tukumbuke kuwa kwa sasa hivi uchaguzi unaofanyika huko Igunga ni nje ya bajeti ya serikali na vyama vya siasa, kwa maana hiyo pesa hizo zimechukuliwa kutoka kitengo cha maendeleo au huduma nyingine za jamii na kupelewa kwenye uchaguzi. Kesho tutailalamikia serikali kwa nini haijajenga barabara, haijaajiri walimu nk kumbe pesa zilizokusudiwa zimepelekwa kwenye chaguzi ndogo ambazo hazikuwa na budget.
 
THE BOSS na quote ya Mh H. Mdee, mada ya chaguzi ndogo na changamoto za kupoteza muda na gharama zake linajadilika....,
nakupongeza kwa kulizungumzia hilo jamvini...,

ni muhimu kwa Taifa kulitafutia ufumbuzi.
ni kwel Demokrasia inahitajika but huwa inakwenda na gharama zake, je chini ya JK, Govt inaweza kukuza uchumi wenye kuweza kukabiliana na hizo gharama..?
mjadala wetu utafute njia sahihi na iliyo bora (kwa gharama na muda) ktk kukabiliana na hizo chaguzi ndogo ndogo kwa nchi yetu Tanzania.....!

Tukiamua tutaweza ni jambo ambalo haliwezi kutushinda....!
 
Wana Jamvi.

Nimepata ushahidi wa maelezo kutoka kwa watu tofauti wa igunga juu ya tindikali igunga, kifupi ni kwamba aliye mwagiwa tindikali alipewa shilingi 1.5 million na Nape pamoja na kabineti yake ili akabandue mabango na picha za mgombea wa chadema yeye na wenzake watatu ambao walikataa kushiriki hujuma hizo na kuamua kuingia kichwa kichwa yeye mwenyewe, wakati akiwa kwenye mchakato huo ndipo alipokutana na mazila yote ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana kama ni wa cdm au ccm walioamua kumtoa kafara.

Source na kumjua shahidi wa habari hii ambaye pia ni kada wa ccm gonga hapa


MwanaCCM amkosoa Mwigulu kuihusisha CHADEMA na tindikali - YouTube

Nawakilisha
 
Hivi huyo Regia Mtema ndio mahakama na hiyo Youtube video? ya kutengeneza? CDM bana hakuna kitu hapo mtaangaika bure vijana waliokamatwa na polisi na vijana wa CDM nyie endeleeni kujifariji na kulidhishana, wewe unategemea nini kesi ya mbuzi umpe chui hukumu itakuaje?
 
Wana JF, nitatoa mawazo yangu kulingana na hali halisi inavyoongelewa na vyombo vya habari na uzoefu wangu na siasa za Tanzania.

Hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kwamba chama fulani kimeiteka, kimeishika, ama kitashinda uchaguzi Igunga na ndio maana wote sasa hawalali ni kampeni hadi kieleweke. Kama kipo kile ambacho kina uhakika kitashinda basi hakuna haja ya kuendelea kuhangaika hovyo majukwaani kukenua meno bila sababu, ilhali ushindi upo basi ni muda muafaka wa kutafuta suti, viatu safi, na kuandaa sherehe baada ya kuapa.

Hali Igunga ni tete mno na wananchi wote huko wanatafakari na sio rahisi kutoa msimamo wa matokeo kwa kuwa wao ndio wapiga kura. Narudia tena, kujaza watu ama kutoa wali haku garantii ushindi, inatakiwa kampeni tu na kuachana na propaganda za kipuuzi.

Sasa Nisimange Kidogo ndugu zangu mtaniwia radhi: Hivi hawa CCM nani huwa anaongea hata kwa mvuto kwa wananchi, mbona Mkapa zero, mwigulu lugha tabu jazba juu - hivi huyu alipataje kura kule jimboni kwake? Mukama zero, yaani sijui huwa wanajipanga ama ni kukurupuka tu! Kama siasa ndio hivi walah bora ya yule gamba RA aliyeamua kwa hali ya kukata tamaa kabisa kuishia kusema mimi wajameni ni mwanaigunga na mwanachama wa ccm huku moyoni akilia na nadhani ataona furaha kama ccm ikiangukia pua Igunga.

Wana JF, natoa mawazo tata.
 
Sikubalian na híi hoja kwan kuna sababu za tofauti tofauti..zinazosababisha kufanyika uchaguz mdogo.unategemea sababu kama hii ya ufisad wa ccm tuwaachie jimbo kienyeji?

Mkuu naam umenena jambo jema, tukumbuke hizi chaguzi zina gharama na muda kupotea...., hapa ndipo hawa jamaa Mafisad wanapo take advantage...,
tutafute njia sahihi ambayo hao mafisad hawataweza kupora Ushindi halali toka kwa wananchi husika.....!
 
kuna siku nilijisemea moyoni "hizi kambeni kuna watu watakufa" sasa tayari mtoto alikufa,sasa huyu kijana nae hoi kwa tindikali! minaomba uchunguzi ufanyike ili tujue wahusika siyi kushabikia tu kwamba chadema wamehusika! pia vijana wenzangu kwanini unakubali kutumiwa kwapesa kidogo jamani? dah nimehuzunika sana! sasa huyu kijana sindokesha kuwa kilema jamani kisa kutumiwa na wanasiasa!
 
Meneja kampeni anasema mgombea wa CDM anafanya kazi katika serikali ya kifisadi,hivi CUF huko ZnZ wako katika serikali na chama kipi? hata hivyo Cuf ni kwanini wanaona adui yao mkubwa ni CDM kuliko CCM.? Kuna kitu cha kujifunza hapa..
 
Watu bana, mnatokwa mapoooooovu!! Tusubiri uhalisia, matokeo ya kwenye mi-blogu haiwakilishi nzega!!!

Ninachoamini lazima mpambano utakuwa mkali sana!!!

kumbe hata jimbo lenyewe hujui, Nyinyi ndio mnaofikiri waTZ bado wamelala.
 
ni vigumu kuamini, leo nilikuwa igunga ki ukweli watu wanakiri wazi kuwa ccm kushinda labda kwa mbinu chafu tu ila wamebanwa haswa, wanatumia mbinu nyingi sana chafu kuichafua chadema lakini hawawezi.

Mtu mmoja akaniambia walikuwa wamepanga kuchoma moto jengo lao wenyewe la ccm ili wauaminishe uma kuwa ni mahasim wao , ila naona chadema wana intelenjesia kali wakabaini huo mchezo mapema kabla haujatekelezwa. hayo siyo maneno yangu ni yajamaa tena walikuwa wananizibia pancha gari. Ni mengi mno wameniambia ukiachia shoo ya bure waliyopelekewa ya akina joti walipomaliza tu watu wakaondoka zao, mkapa hakuamini.

ukitaka kujua uhalisia wa mambo Igunga pata info ambazo hazijachakachuliwa kutoka hukohuko or kwa watu ambao sio biased. Yaani Magamba are capable of anything niko so worried wajameni.
 
Hivi huyo Regia Mtema ndio mahakama na hiyo Youtube video? ya kutengeneza? CDM bana hakuna kitu hapo mtaangaika bure vijana waliokamatwa na polisi na vijana wa CDM nyie endeleeni kujifariji na kulidhishana, wewe unategemea nini kesi ya mbuzi umpe chui hukumu itakuaje?


There is my big worry.

Hapa CCM watacheza sana, watu wanaweza pewa hela watoe ushahidi wa Uongo Dhidi ya CDM
 
East africa kuna msiba hawa wanaendeleza siasa uchwara...tz bana
 
wakuu kwa hali ya mgonjwa ilivyo sina la kusema ila hukumu atatoa Mungu pekee,hata kama hukumwaga tindikali lakini umehusika kwa namna yeyote.Roho itendayo haya kwa makusudi imlilie Mungu sasa kwa dhambi hii!
 
Wana Igunga walikwenda ktk tamasha la sanaaa..... haikuwa Campaign ya Siasa.
so hakuna haja ya kuwa na hofu...,
wanaigunga wanajua nini cha kufanya cku ikifika!
 
welevu wanakuchora tu, uku mimi nabaki nacheka tu!...........
Teh teh teh! Ant Matola, bana ujui nini hapo bana nilijua lazima utabold, maana ya hiyo ni Ingia halafu hiyo ingine Masaburi mpaka watu wote wajue? Umenipata sasa
 
Nimeangalia kura za maoni kwa jimbo la Igunga kwenye site ya mwanahalisi, ingawa kura hizi hupiwa na Watanzania wote lakini pia inawapa taswira hawa wanaojiita wamiliki wa nchi (CCM) jinsi waTZ walivyochoshwa na Uzemba na udhalimu wao.


Kwa leo: 12/09/2011

Maggid Mjengwa Blog

Joseph Kashindye (Chadema)) 270 (73%)
Leopard Mahona (CUF) 26 (7%)
Dr Peter Kafumu (CCM) 72 (19%)

Votes so far: 368


Mwanahalisi

Leopold Mahona (CUF) 4%
Joseph Kashindye (CHADEMA) 89%
Peter Kafumu (CCM) 5%
Said Makeni (DP) 1%
Lazaro Ndageya (UMD) 0%
John Maguma (SAU) 1%


Total votes: 305

Kwa matokeo zaidi bofya hapa: Gazeti la MwanaHalisi

RAI

CCM (40%, 297Votes)
Chadema (40%, 297 Votes)
CUF (18%, 131 Votes)
UDP (1%, 11 Votes)
SAU (1%, 4 Votes)

Total Voters: 740



Wangeruhusu tuu wakazi wa Igunga wapige kura; hata hivyo hizi haziwakilishi mawazo ya Wanaigunga kwani wenye access na computer ni watu tofauti kabisa na maskini wa kule Igunga
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom