Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Endeleeni kuhesabu sahani tu, Oktoba wenzenu watahesabu kura halafu nyie mtaanza ooh tumechakachuliwa.
Siasa si kama mahusiano mkuu, usiamini kuwa hao kwenye picha 'wanaichuna' tu Ccm halafu watalala kwenu. Ohoo..

Ukweli ni kama Jua lichomozalo,popote ulipo litachomozea Mashariki!!

• ADAI INAIANDAMA CHADEMA KUIBEBA CCM

na Mwandishi wetu
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema Chama cha Wananchi (CUF), kinaelekea kujimaliza kisiasa na kimepoteza mwelekeo kwani badala ya kuhubiri sera zake kimekuwa bingwa wa kuishambulia CHADEMA, kwenye majukwaa ya siasa kila kinapomnadi mgombea wake katika jimbo la Igunga.

Katibu huyo aliitoa kauli hiyo juzi jioni wakati alipowahutubia wananchi wa kijiji cha Simbo akisema CUF imepoteza dira na imekuwa ikiwaambia wafuasi wake washiriki kwenye siasa chafu za kubandua picha za mgombea wa CHADEMA, Joseph Kashindye.

Alisema kuwa CUF imewadhihirishia Watanzania kuwa si wapinzani kwani wapinzani wa ukweli kamwe hawezi kuwa viongozi wa kuwasema wenzao wanaopambana na chama tawala ambacho kimeshindwa kuwaletea maendeleo wananchi.

“CUF imepoteza dira, tulitegemea wao wangekuwa mstari wa mbele kuungana nasi katika mapambano ya kuiondoa CCM madarakani lakini wao wamekuwa sehemu ya kuisaidia CCM ishinde, sisi hatutawahofia; tutaendelea kupambana nao kama tunavyofanya kwa CCM,” alisema Dk. Slaa.

Alibainisha kuwa kamwe CHADEMA haitawaachia CUF waendeleze harakati zao za kuwabeba ndugu zao wa CCM ambao wamekuwa wakihaha huku na huko kuhakikisha wanalibakisha mikononi mwao jimbo hilo lililoachwa wazi na kada wao Rostam Aziz, aliyechoshwa na siasa za maji taka.

Alisema wananchi wanahitaji vyama vya kutetea maslahi yao na rasilimali za taifa ambazo hivi sasa zinatumiwa na watu wa CCM kwa maslahi ya kikundi cha watu wachache.

Dk. Slaa, aliongeza kuwa CUF imekuwa bingwa wa kutumia propaganda ambazo zinaonekana wazi kuisadia CCM ishinde uchaguzi wa Igunga ambao unaonekana kuwaponyoka na kuangukia CHADEMA.

Alisema CHADEMA ni chama chenye kupenda mabadiliko kwani kilikuwa kikishirikiana na wapinzani katika maeneo mbalimbali kwenye chaguzi zilizopita lakini hivi sasa kimebaini kuwa si kila mpinzani ni mpinzani.

Alibainisha kuwa CHADEMA waliiachia CUF ipambane na CCM katika mikoa ya Lindi na Mtwara lakini haikuweza kufanya vizuri kama walivyotarajia.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka jana jimboni Igunga, CUF ilisema mgombea wao wa ubunge, Leopard Mahona, alipata kura 11,000 ambazo hivi sasa ndizo wanazozitambia wakati wanasahau kuwa CHADEMA haikusimamisha mgombea wa ubunge, ndiyo maana CUF walipata kura hizo.

“Mimi nawaambia Mahona hana ubavu wa kupambana na Kashindye, tumeamua kusimama Igunga kuwaonyesha CUF nini maana ya upinzani; wao waendelee na kampeni zao za kuwasaidia CCM lakini wajue wananchi watawahukumu,” alisema.

Aliongeza kuwa ili kuthibitisha kuwa CUF haina nguvu mkoani Tabora, mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, aliyewania urais mwaka jana, aliambulia kura 3,000 wakati yeye (Slaa) alipata kura 8,000.

Naye mgombea ubunge wa CHADEMA, Kashindye, aliwaomba wananchi wa vijiji vya Simbo na Igoweko kumchagua ili awasaidie kutanzua matatizo yanayowakabili.

“Nimekuwa mwalimu wa shule ya msingi muda mrefu katika jimbo hili, natambua matatizo yenu ya maji, zahanati na barabara, kama mkinichagua kwenda bungeni nitahakikishia haya yote nayafanyia kazi,” alisema Kashindye.

Onyo kwa CCM
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa siku tatu kuanzia jana kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba, kuomba radhi au kutoa ushahidi kuthibitisha kuwa CHADEMA iliandika barua serikalini kutaka bei ya pamba nchini ishushwe.

Dk. Slaa alisema kama Nchemba alitoa kauli hiyo alipokuwa kwenye uzinduzi wa chama hicho juzi kuwa CHADEMA hawawezi kuwasaidia wakulima kwa kuwa waliandika barua ya kuzuia bei ya pamba kuongezwa atoe vielelezo kuthibitisha kauli yake.

Alisema kuwa kama mbunge huyo hataomba radhi, CHADEMA watamwita mwongo kila wanapokwenda ikiwemo kupiga kambi katika jimbo lake la Iramba, kueleza uongo wake kwa wananchi wa Igunga.

Alisema CHADEMA haiwezi kuandika barua hiyo, kwa sababu sera ya chama hicho ni kulinda wakulima na mazao yao ikiwemo kuweka mfuko maalum wa kulinda bei ya zao hilo.

“Mwigulu ni muongo, hakuna barua tuliyoandika CHADEMA, atuombe radhi la sivyo tutamwita mwongo kila aendako na nitapiga kambi katika jimbo lake na kutangaza mambo yake,” alisema.

Dk. Slaa pia alimpiga kijembe Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akisema juzi hakujibu hoja zilizotolewa na wapinzani na badala yake alijikita kudai kuwa vyama hivyo vinatoa shutuma zisizo na mashiko.

Alisema Mkapa alipaswa kueleza alivyoshiriki kwenye utafunaji wa rasilimali za nchi wakati akiwa Ikulu.

Alibainisha kuwa CHADEMA hakijaingia madarakani; lakini kinaona nchi inavyokwenda halijojo kwa sababu ya utawala mbovu wa CCM ambayo iko madarakani kwa zaidi ya miaka 30.

CCM yasitisha kampeni

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeahirisha shughuli za kampeni wilayani Igunga kwa siku moja kuomboleza msiba wa kitaifa wa watu zaidi ya 190 waliofariki kwa ajali ya kuzama na meli baharini huko visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Tanzania Daima, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye, alisema CCM inawapa pole wafiwa na kuwaombea wapone haraka majeruhi wa ajali hiyo.

Kwa mujibu wa Nape, chama hicho hakikufanya kampeni zozote jana na kuahidi kuendelea na shughuli hizo bila shamrashamra kwa siku mbili.

“Tumeahirisha kampeni zetu kwa siku moja lakini kuanzia leo kwa kipindi chote ambacho taifa litapeperusha bendera nusu mlingoti hatutakua na shamrashamra kwenye kampeni

“…Huu ni msiba wa taifa, kama chama tunawapa pole Wazanzibari na Watanzania wote; tunaziombea roho za marehemu zipumzike kwa amani na majeruhi wapate nafuu ya haraka,” alisisitiza Nape.

Wakati CCM ikiomboleza kwa namna hiyo, Chama cha Wananchi (CUF), kimesisitiza kuendelea na ratiba ya kampeni zake kama kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, alisema msiba huo hautavuruga ratiba ya kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga.

Mtatiro alibainisha kwamba uzinduzi rasmi wa kampeni hizo utafanyika kesho ambapo mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, atawahutubia wananchi wa Igunga na kumwombea kura mgombea wake, Leopold Mahono. Uzinduzi wa kampeni utakwenda sambamba na maandamano.

Alisema CUF inatoa salamu za pole kwa wote walioathirika kwenye ajali hiyo na kuishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kuweka wazi idadi ya walionusurika na waliokufa huku akiitupia lawama za uzembe serikali hiyo na kutaka waliohusika wawajibishwe.

chama cha wanainchi CUF kitazindua kampeni zake kesho katika viwanja vya sokoine kuanzia saa 8 mchana kabla ya hapo kutatanguliwa na maandamano ya mapokezi akiongea leo katika kikao cha waandishi wa habari mratibu wa kampeni wa cuf igunga kasim khamisi chogamawano amesema maandalizi yote yamekamilika na wanachama na wapenzi wa cuf wameanza kuwasili kutoka vijiji mbalimbali vya Igunga kwa ajili ya mapokezi ya aina yake ambayo yatavuta umati mkubwa wa watu kwa ajili ya kumpokea mwenyekiti wa cuf Taifa Prof I. H. Lipumba.

Huu mchezo wanaoucheza CCM ni mchezo wa kipumbavu sana. Wanatumia ujinga wetu wetu kutufanya Majuha/mazezeta/mazuzu.... Wameanza na vikombe. Wakatuzuga sote na leo walipoona Mkapa (mtuhumiwa mkuu wa mikataba feki na mwanzilishi wa Ufisadi) anaenda Igunga wakaibuka na Single mpya ya MSEMAKWELI kuhusu KAGODA ili mkapa apate kuongea!!!!

Hilo liliposhindwa sasa wamemlipua kijana ili wasingizie CDM.Huu ni upuuzi. Lakini Mungu yupo. Ipo siku tutawakamua kwa vyote walivyonyonya na wao wasukume mikoteni na watoto wao wawe wa mitaani, wajifungue njiani, walalenjaa, wafanyiwe operationi bila ganzi nk.

Dada ahasante kwa habari hizi. Nimesikitika kuona Nchembe anavyoongea kinafiki, nimetamani Mungu ashushe jiwe limbondembode pale jukwaani. Huu ni ufisadi wa maisha ya watu, uzandiki wa ccm, mauaji ya kinyama na ushenzi uliopitiliza. Nawalaani timu yote ya kampeni ya ccm igunga akiwemo fisadi tembo NKAPA kwa kuwafanyia vijana masikini huo uharamia.
Mungu ibariki Tanzania

Last edited by a moderator:
Watu huwa wanamlaumu sana Kiranga akikwambia ukweli Regia lakini nimegundua kuwa Kiranga yuko Sahihi. Yaani wewe Regia umeridhika kuwa huu ni ushahidi tosha wa kujua nani amefanya tenda la kinyama la kummwagia mtu tindikali?

Hufai kuwa kiongozi wa jamii iliyoamua kuendelea.

Kiongozi anayejali maslahi ya watu anapaswa kutaka uchunguzi huru ufanyike ili yeyote aliyehusika achukuliwe hatua.
Narudia tena, kwa kitendo chako hiki cha kufanyia masihala swala la mtu kumwagiwa tindikali, Regia, hufai kuwa kiongozi wa Tanzania bora.
You are just politics as usual.

Kwamtazamo wangu mimi, taarifa hii ya Regia ipo balance na yamuhimu sana katika kupata ukweli wa jambo hili. Ametoa maelezo ya Mh.Mwigulu pamoja na ya huyu kijana wa CCM. Hakuongeza neno lake lolote wala kutoa hukumu/hitimisho. Kama jambo hili litachunguzwa na litahukumiwa kwa haki, litatufumbua macho na tutaweza kukemea/kuwaadhibu wahusika kwa kura zetu ama vinginevyo. Mungu Ibariki Tanzani

achen unafik watakamatwa tu mlio watuma na huyo mwanaccm mliemrubun awasemee itakula kwake wauwaji nyie
Punguza mapovu mtego mtege wenyewe kuingia muingie wenyewe halafu msingizie wengine na bado watakapotajwa waliotoa pesa ndipo mtakapoijua gogogo kwa kijapani inaitwaje.

Mnatapa tapa kutengeneza video nyie Chadema kaeni macho mda wote CCM wanaandaa kujibu mapigo! Mnaleta siasa za kitoto yani mnamumwagia mtu tindikali halafu mnamtafuta mtu ajifanye ni CCM ampinge Mwigulu! Kaeni mkao wa kupokea tukio Igunga! "To every action there is equal and opposite reaction"
Tunasubiri hilo tukio ujinga wenu ndio unawaponza kwa vile huwa mnatuarifu in advance lakini usisahau kama ulivyoandika "To every action there is equal and opposite reaction".

Mimi tangu nipo mtoto nimekua nawaamini sana walemavu ni watu waaminifu sana lakini dada yangu Regia kama umejiingiza kwenye propaganda hizi za Chadema unaondoa hata uaminifu tulio nao kwa walemavu!

Last edited by a moderator:

Mimi tangu nipo mtoto nimekua nawaamini sana walemavu ni watu waaminifu sana lakini dada yangu Regia kama umejiingiza kwenye propaganda hizi za Chadema unaondoa hata uaminifu tulio nao kwa walemavu!
Imewatachi eh.......niliwaambia manati huwa haipigwi hivo ikiwa imegeuzwa.

Mimi tangu nipo mtoto nimekua nawaamini sana walemavu ni watu waaminifu sana lakini dada yangu Regia kama umejiingiza kwenye propaganda hizi za Chadema unaondoa hata uaminifu tulio nao kwa walemavu!
Nani atakuwa na imani nawewe ambaye umelemaa akili?hovyoooo

Mtatiro zuia hiyo zahama kwa chama chako; ipisheni kwanza maombolezo ya msiba - ni busara tu.

Hao wanalipwa pesa nyingi yaani mavazi, chakula, posho za kukenyua wakati wa mikutano ya kampeni za magamba,
ina ukwel kwamba hat magamba hawawezi kuchukiwa na watu wote ila, hao wasiwatishe kwanza ni mamluki

Ukiona dalili hizo, jua CCM ina pumulia mashine! Muda si mrefu itabaki kwenye kumbukumbu ya vitabu vya historia!

Mimi tangu nipo mtoto nimekua nawaamini sana walemavu ni watu waaminifu sana lakini dada yangu Regia kama umejiingiza kwenye propaganda hizi za Chadema unaondoa hata uaminifu tulio nao kwa walemavu!

Mkuu naomba unikosoe kwa hoja lakini usiuhusishe ulemavu wangu..Jenga hoja lakini si vema kushambulia mumble ya watu,hakuna mtu aliyemuomba MUNGU kuwa jinsi alivyo,awe mbaya,mzuri,mwenye ulemavu au kutokuwa na ulemavu..

Hakuna uhusiano wa ulemavu na kuwa muaminifu au kutokuwa mwaminifu...Haya mengine ni tabia na ulemavu ni hali.

Usicheze na MUNGU,Mshukuru MUNGU kama huna ulemavu wa aina yeyote ile.

MUNGU akubariki sana na nakuombea MUNGU asikupe ulemavu ama wewe au yeyote yule katika familia yako..

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom