Uchaguzi 2020 Uchaguzi: Ikiwa Tundu Lissu atagombea Urais 2020, Majimbo haya Singida yajiandea kuwa CHADEMA

Uchaguzi 2020 Uchaguzi: Ikiwa Tundu Lissu atagombea Urais 2020, Majimbo haya Singida yajiandea kuwa CHADEMA

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Asalaam wajumbe wa jukwaa hili!

Nataka niwape taarifa kwa wanaccm wote ambao ni wagumu kuelewa, hili nalisema kabisa kutokana na hali ilivyo ambayo inaambatana na matukio ya kura za maoni CCM ambayo kwa kiasi kikubwa yalitawaliwa na rushwa. 99% ya majimbo ambayo yalifanya uchaguzi kura za mjini Singida kuna minong'ono mikubwa yalitawaliwa na rushwa.

1.SINGIDA MASHARIKI
Hili jimbo lilikua chini ya mh Tundu Lissu toka 2010 mpaka 2017 aliposhambuliwa na risasi mkoani Dodoma na watu akijulikana, baada ya tukio hilo alipelekwa hospitalini na baadaye jimbo likatangazwa na Spika Ndungai kua liko wazi na tume ya taifa ya uchaguzi kulitangaza kua wazi, alipewa ndugu Miraji Mtaturu ambaye inasemekana kua hana ushawishi wa kisiasa kabisa kumfananisha na Mh Lissu.

Huyu Mtaturu pia anasemwa kutokana na elimu yake kua ya msingi pia uelewa wake umekua mdogo sana kwenye mambo ya kisiasa. Ikumbukwe kua katika jimbo hilo pamoja na madiwani wote kua CHADEMA lakini alishindwa kupata diwani hata mmoja aliyeweza kuunga mkono juhudi mpaka uchaguzi mkuu mwaka huu.

Inasemekana kutokana na umoja walionao watu wa kabila la Wanyaturu ikiwa Lissu atagombea Urais na ikizingatiwa wana uchungu na masahibu yaliyomkuta na wabunge wa CCM kugoma kwenda Nairobi kumujulia hali mbunge mwenzao,Wanasema tukiwa Lissu atagombea Urais watamuunga mkono kuanzia nafasi za udiwani hadi ubunge.Kwa maana hiyo Chadema wakisimamisha mgombea yeyote hata kama ni jiwe watalipigia kura.
#Haya siyo yangu ni ya wananchi Singida Mashariki#

2. SINGIDA MAGHARIBI

Hili jimbo shida kubwa ni CCM kumrudisha mgombea ambaye kuna malalamiko makubwa alishinda kura za maoni kwa kugawa rushwa nyingi za pesa kwa kuwasafirisha wajumbe kwenda ukumbi wa kupigia kura, huyu huyu mgombea kuna tuhuma na inasemeka kua alikwapua pesa za Mfuko wa jimbo Million 76 ambazo zilitakiwa kujenga madarasa shule ya sekondari Puma amezitumia kuhonga wajumbe.

Kwahiyo hapa kwa upinzani na kwa kuongezea nguvu ya Lissu kama atagombea Urais, wananchi wameapa kua wapo tayari kwa gharama zozote kuwapa CHADEMA jimbo hilo kuliko kurudi kwa mdau ambaye ana tuhuma nyingi za rushwa.
#Haya ni maoni ya wananchi siyo yangu#

3.SINGIDA MJINI

Hili jimbo inasemekana limewekwa kimkakati na viongozi wa CHADEMA kanda ya kati ambapo kama Lissu atasimamishwa kugombea Urais, basi Lazaro Nyalandu ana ushawishi mkubwa katika mji huo anaweza kugombea na kuunganisha nguvu na Lissu.

Sababu nyingine ya jimbo hili kwenda Upinzani ukiachilia nguvu ya Lissu na Nyalandu ni mchanganyiko wa jamii za makabila mbali mbali ndani ya mji huo ya Wanyaturu,Wachaga,Wanyiramba na Warangi ukitoa maeneo ya pembezoni mwa mji.Hawa ya makabila hayana mtu maalumu zaidi yataangalia umaarufu wa mtu tofauti na majimbo mengine ya mkoa huo ambao hutazama zaidi uzawa.
#Haya siyo yangu ni ya wananchi wenyewe#

4.SINGIDA KASKAZINI

Hili zimbo lilikua chini ya Ndugu Lazaro Nyalandu ambaye alijiuzulu na kuhamia CHADEMA mwaka 2017, inasemekana bado nguvu yake ni kubwa sana kwa wanachama wa CCM hivi sasa. Kwahiyo anatarajiwa kuongeza nguvu kwa mgombea yeyote atakayewekwa na CHADEMA ambaye inasemekana kua ni aliyekua mgombea wa mwaka 2015 kupitia chama hicho ndugu DAVID JUMBE.

Sababu nyingine ya jimbo hili kwenda Upinzani ni CCM kuruhusu uchaguzi kura za maoni kutawaliwa na vitendo vya rushwa ambapo washindi namba 1 hadi 3 wanatuhumiwa kugawa rushwa sana na walizidiana viwango tu.
Kwahiyo wananchi wameapa akirudi mmojawapo ni bora wapate mwakilishi kupitia upinzani.
#Siyo yangu haya ni ya maadhi ya wananchi"

5.MKALAMA

Sababu kuu ya jimbo hili kwenda Upinzani zile zile hasira za wananchi juu ya michakato ya CCM kutawaliwa na rushwa ambapo mshindi wa 1 hadi wa 5 wanatuhumiwa kwa kugawa sana rushwa ispokua wamezidiana pia.Wananchi wana hasira kubwa pia wameapa kutopigia kura yeyote atakerudishwa kati ya hayo majina 5. Kuna taarifa kua CHADEMA wanajipanga kuweka mgombea mwenye ushawishi na nguvu ili aweze kuungana na upepo wa Mhe Tundu Lissu kulitwaa jimbo hilo.

#Ni maeno ya wananchi wanasikika eneo husika siyo yangu#
 
Naona yale matumaini ya kuupaka upepo rangi walikuwa nayo wana ccm yanaanza kuyeyuka
 
Watakuwa wamelaaniwa kama watashindwa kumuunga mkono ndugu yao aliyepigwa risasi mchana kweupe kusudio likiwa kumuua. Kwanza kwa kitendo hicho ningetegemea mkoa mzima kuikataa ccm. Nyalandu alionyesha moyo mwema baada ya kujua kuwa ndugu yake kapigwa risasi akaamua kuhama chama cha mauwaji.

Nitawashangaa sana. Yaani huko inatakiwa iwe kitovu cha ukombozi.
 
Ukweli gani hapo zaidi ya kujikalia kwenye keyboard nakujiandikia upupu mtupu?
Kwani CHADOMO ipi Singida?
Kama manguruwe ya Lumumba yanavyojidanganya kukubalika kumbe zerooo na mwaka huu tunayanyoosha.
 
Back
Top Bottom