Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Uchaguzi wa viongozi wa vyama vya siasa na wale wa serikali una sheria, kanuni na taratibu zake ambazo zisipozingatiwa huweza kusababisha vurugu na kusambaratisha chama au nchi.
Kwa ujumla taratibu ziko hivi:
1. Siku na mwezi wa uchaguzi hujulikana mapema. Ni miaka mitano baada ya uchaguzi uliopita.
2. Siku au wiki chache kabla ya tarehe ya uchaguzi kwenye vyama vya siasa na serikali za mitaa fomu hutolewa kwa wale walio na nia ya kuwa wagombea. Watajaza fomu hizo na kuzirudisha kwenye mamlaka husika.
Mamlaka husika huzichakata fomu hizo na kwa wale watakaokubaliwa ndio watakaotangazwa na mamlaka kama "Watia nia" aka wangombea. Kwa uchaguzi mkuu wa serikali muda huu huwa mwezi mmoja au zaidi kidogo.
Huwezi tu mtu ukakurupuka kutoka huko ulikotokea, tena wakati wo wote na kujitangaza mwenyewe kuwa wewe ni mtia nia au mgombea wa kiti fulani kwenye chama chako.
Ingalikuwa hivyo basi tungalikuwa na maelfu ya watu wanaogombea kiti kimoja. Mtu yo yote anaruhusiwa na ni haki yake ya kutia nia, ie kujaza hiyo fomu ya kuomba kuwa mgombea kiti cho chote. cha kisiasa kwenye chama na serikali. Ni job application. Sasa ni kitu ambacho hakiwezekani (common sense) kwamba wapiga kura wakapelekewa maelfu ya majina kwa kila kiti wakayapigie kura. Lazima kuwe na mamlaka ya kuyapunguza (kuyakata) kubaki mawili hadi matano.
Kwani nani hapendi kuwa Raisi wa nchi au Mwenyekiti wa chama cha siasa?
3. Baada ya mamlaka husika kuchagua wagombea wa hivyo viti ndipo wagombea hao hupewa kipindi fulani cha kujitangaza, kufanya kampeni kwa wapiga kura. Kwa vyama vya siasa na s/mitaa kipindi hiki huwa ni kifupi tu cha siku au wiki chache tu kabla ya kupigiwa kura za uchaguzi.
Sasa hiki alichofanya Tundu Lissu ni sahihi kweli? Yeye ghafla kaitisha mkutano wa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama chake, kwenye ukumbi wa gharama kubwa wa Mlimani City na kujitangaza kwamba yeye ndiye mgombea wa kiti cha Mwenyekiti. Kafanya kampeni yake kwa wajumbe hao wa mkutano mkuu wa uchaguzi uliotangazwa na vyombo mbali mbali vya habari alivyo kuwa amevialika. Gharama zote: za usafiri, accommodation, perdiem, ukumbi etc kazilipa yeye kwa fedha alizochangiwa na akina Robert Amsterdam!
Mbaya zaidi katika kampeni yake hiyo kakivua nguo chama chake na Mwenyekiti wake wa sasa. Yaani kakitukana, kakifedhehesha mbele ya umma hadi umma hauna hamu nacho tena.
Kakisambaratisha vibaya, Kakitwanga na kukiacha mahututi. Yaani kumbe Mbowe alikuwa akikiendesha chama hicho kidikiteta? Maamuzi ya vikao mbali mbali ya chama tuliyokuwa tunaambiwa kumbe yalikuwa ni ya Mbowe pekee? Tundu Lissu kakichafua sana chama chake.
Sasa mtu unabaki unajiuliza: Itakuwaje kama mamlaka husika ya chama ikikata jina lake kuwa mgombea wa kiti hicho? Itakuwaje hata kama mamlaka ikapitisha jina lake kuwa mgombea lakini kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama akishindwa na Mbowe? Ataweza kubaki kwenye chama hicho kweli? Ndiyo maana kanuni na taratibu za kampeni za uchaguzi zinakataza kuchfuana. Sasa huyu anachafua hadi chama chake.
Mamlaka za chama zikiamua kumfukuza kwenye chama ataenda wapi? CCM au ACT kwani kuanzisha chama chake Jaji Mtungi hatakubali kwani anamfahamu busara zake.
Kwa nini hakufuata busara za Msigwa? Alitakiwa kuondoka kwanza kwenye chama hicho ndipo ayaseme hayo aliyoyasema kwenye huo mkutano. Au angalifuata busara za Lowasa za kusubiri kuenguliwa na kufanya alichofanya.
Ngoja tusubiri. Ngoma inaweza kuwa tamu kuliko ile ya Lyatonga Mrema enzi zile alipokuwa NCCR - Mageuzi.