Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Acha ujinga na kiingereza chako kibovubovu.When you discussed about politics I can see you as stupid just leave your life remember "POLITICS ITS A DIRTY GAME"
Taasisi kubwa kama CCM, CDM, ACT. Viongozi huwa hawachaguliwi ila wanaandaliwa, Nadhani Lisu amenusa harufu fulani kuwa yeye ahuyoko miongoni mwa Watu wanao andaliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama kwa hiyo anataka kutumia Force. Hii itamgharimu sana wala hiyo vita hataiweza. Pamoja na mapungufu yote aliyonayo Mbowe Lisu bado alipaswa amuheshimu Mbowe hata kwa unafiki, mbona amefanya hivyo kwa Mda mrefu, Lisu anajua madudu yote anayo yafanya Mbowe ndani ya Chama na yeye alikuwa anayamezea sasa iweje sasa akurupuke tu huko aliko toka na kuanza kumshutu mwenyekiti wake na viongozi wenzake hilo siyo sawa, kiongozi ni pamoja na kuwa na Roho ya uvumilivu na ustahimilivu bila kuchoka. Uwenyekiti wa taasisi kubwa hizo nilizozitaja, uongozi wake auji vup, vup tu unakuja kwa mipango ya mda mrefu. Tazama uongozi wa Magufuli, Haukuweza kudumu kwa mda Mrefu kwakuwa CCM walikuwa wamemuandaa Membe ndiye awe kiongozi lakini upepo ukabadilika katikati ya vikao ikabidi wamteue, Magufuli tazama jinsi alivyo tawala na kukanyaga kanyaga. Kwahiyo Lisu ajaribu kujituliza kwanza na wala asihame Chama kwasabu chama bado kinamuhitaji ila Mbowe tu na genge lake ndiyo hawamtaki kwa ajili ya mstakabali wa Maslahi yao, na kwakuwa hajajipanga na wenzake wameshajipanga yeye awe mpole tu.Uchaguzi wa viongozi wa vyama vya siasa na wale wa serikali una sheria, kanuni na taratibu zake ambazo zisipozingatiwa huweza kusababisha vurugu na kusambaratisha chama au nchi.
Kwa ujumla taratibu ziko hivi:
1. Siku na mwezi wa uchaguzi hujulikana mapema. Ni miaka mitano baada ya uchaguzi uliopita.
2. Siku au wiki chache kabla ya tarehe ya uchaguzi kwenye vyama vya siasa na serikali za mitaa fomu hutolewa kwa wale walio na nia ya kuwa wagombea. Watajaza fomu hizo na kuzirudisha kwenye mamlaka husika.
Mamlaka husika huzichakata fomu hizo na kwa wale watakaokubaliwa ndio watakaotangazwa na mamlaka kama "Watia nia" aka wangombea. Kwa uchaguzi mkuu wa serikali muda huu huwa mwezi mmoja au zaidi kidogo.
Huwezi tu mtu ukakurupuka kutoka huko ulikotokea, tena wakati wo wote na kujitangaza mwenyewe kuwa wewe ni mtia nia au mgombea wa kiti fulani kwenye chama chako.
Ingalikuwa hivyo basi tungalikuwa na maelfu ya watu wanaogombea kiti kimoja. Mtu yo yote anaruhusiwa na ni haki yake ya kutia nia, ie kujaza hiyo fomu ya kuomba kuwa mgombea kiti cho chote. cha kisiasa kwenye chama na serikali. Ni job application. Sasa ni kitu ambacho hakiwezekani (common sense) kwamba wapiga kura wakapelekewa maelfu ya majina kwa kila kiti wakayapigie kura. Lazima kuwe na mamlaka ya kuyapunguza (kuyakata) kubaki mawili hadi matano.
Kwani nani hapendi kuwa Raisi wa nchi au Mwenyekiti wa chama cha siasa?
3. Baada ya mamlaka husika kuchagua wagombea wa hivyo viti ndipo wagombea hao hupewa kipindi fulani cha kujitangaza, kufanya kampeni kwa wapiga kura. Kwa vyama vya siasa na s/mitaa kipindi hiki huwa ni kifupi tu cha siku au wiki chache tu kabla ya kupigiwa kura za uchaguzi.
Sasa hiki alichofanya Tundu Lissu ni sahihi kweli? Yeye ghafla kaitisha mkutano wa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama chake, kwenye ukumbi wa gharama kubwa wa Mlimani City na kujitangaza kwamba yeye ndiye mgombea wa kiti cha Mwenyekiti. Kafanya kampeni yake kwa wajumbe hao wa mkutano mkuu wa uchaguzi uliotangazwa na vyombo mbali mbali vya habari alivyo kuwa amevialika. Gharama zote: za usafiri, accommodation, perdiem, ukumbi etc kazilipa yeye kwa fedha alizochangiwa na akina Robert Amsterdam!
Mbaya zaidi katika kampeni yake hiyo kakivua nguo chama chake na Mwenyekiti wake wa sasa. Yaani kakitukana, kakifedhehesha mbele ya umma hadi umma hauna hamu nacho tena.
Kakisambaratisha vibaya, Kakitwanga na kukiacha mahututi. Yaani kumbe Mbowe alikuwa akikiendesha chama hicho kidikiteta? Maamuzi ya vikao mbali mbali ya chama tuliyokuwa tunaambiwa kumbe yalikuwa ni ya Mbowe pekee? Tundu Lissu kakichafua sana chama chake.
Sasa mtu unabaki unajiuliza: Itakuwaje kama mamlaka husika ya chama ikikata jina lake kuwa mgombea wa kiti hicho? Itakuwaje hata kama mamlaka ikapitisha jina lake kuwa mgombea lakini kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama akishindwa na Mbowe? Ataweza kubaki kwenye chama hicho kweli? Ndiyo maana kanuni na taratibu za kampeni za uchaguzi zinakataza kuchfuana. Sasa huyu anachafua hadi chama chake.
Mamlaka za chama zikiamua kumfukuza kwenye chama ataenda wapi? CCM au ACT kwani kuanzisha chama chake Jaji Mtungi hatakubali kwani anamfahamu busara zake.
Kwa nini hakufuata busara za Msigwa? Alitakiwa kuondoka kwanza kwenye chama hicho ndipo ayaseme hayo aliyoyasema kwenye huo mkutano. Au angalifuata busara za Lowasa za kusubiri kuenguliwa na kufanya alichofanya.
Ngoja tusubiri. Ngoma inaweza kuwa tamu kuliko ile ya Lyatonga Mrema enzi zile alipokuwa NCCR - Mageuzi.
Mm#nina,kingereza cha kisukuma hiki😅🤣When you discussed about politics I can see you as stupid just leave your life remember "POLITICS ITS A DIRTY GAME"
Kajikakamua hadi mwisho tena kwa kufoka.Lugha ni kipaji.Mm#nina,kingereza cha kisukuma hiki😅🤣
Rudi ukajifunze upya maana sahihi.Haahaa juzi anasema Nyerere alikuwa eti ni mtumishi wa umma ndo maana alngatuka, nilishangaa Sana, kwani kiongozi wa chama sio wa umma?
Naona Sasa mmeamua ila upepo unawakataaUchaguzi wa viongozi wa vyama vya siasa na wale wa serikali una sheria, kanuni na taratibu zake ambazo zisipozingatiwa huweza kusababisha vurugu na kusambaratisha chama au nchi.
Kwa ujumla taratibu ziko hivi:
1. Siku na mwezi wa uchaguzi hujulikana mapema. Ni miaka mitano baada ya uchaguzi uliopita.
2. Siku au wiki chache kabla ya tarehe ya uchaguzi kwenye vyama vya siasa na serikali za mitaa fomu hutolewa kwa wale walio na nia ya kuwa wagombea. Watajaza fomu hizo na kuzirudisha kwenye mamlaka husika.
Mamlaka husika huzichakata fomu hizo na kwa wale watakaokubaliwa ndio watakaotangazwa na mamlaka kama "Watia nia" aka wangombea. Kwa uchaguzi mkuu wa serikali muda huu huwa mwezi mmoja au zaidi kidogo.
Huwezi tu mtu ukakurupuka kutoka huko ulikotokea, tena wakati wo wote na kujitangaza mwenyewe kuwa wewe ni mtia nia au mgombea wa kiti fulani kwenye chama chako.
Ingalikuwa hivyo basi tungalikuwa na maelfu ya watu wanaogombea kiti kimoja. Mtu yo yote anaruhusiwa na ni haki yake ya kutia nia, ie kujaza hiyo fomu ya kuomba kuwa mgombea kiti cho chote. cha kisiasa kwenye chama na serikali. Ni job application. Sasa ni kitu ambacho hakiwezekani (common sense) kwamba wapiga kura wakapelekewa maelfu ya majina kwa kila kiti wakayapigie kura. Lazima kuwe na mamlaka ya kuyapunguza (kuyakata) kubaki mawili hadi matano.
Kwani nani hapendi kuwa Raisi wa nchi au Mwenyekiti wa chama cha siasa?
3. Baada ya mamlaka husika kuchagua wagombea wa hivyo viti ndipo wagombea hao hupewa kipindi fulani cha kujitangaza, kufanya kampeni kwa wapiga kura. Kwa vyama vya siasa na s/mitaa kipindi hiki huwa ni kifupi tu cha siku au wiki chache tu kabla ya kupigiwa kura za uchaguzi.
Sasa hiki alichofanya Tundu Lissu ni sahihi kweli? Yeye ghafla kaitisha mkutano wa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama chake, kwenye ukumbi wa gharama kubwa wa Mlimani City na kujitangaza kwamba yeye ndiye mgombea wa kiti cha Mwenyekiti. Kafanya kampeni yake kwa wajumbe hao wa mkutano mkuu wa uchaguzi uliotangazwa na vyombo mbali mbali vya habari alivyo kuwa amevialika. Gharama zote: za usafiri, accommodation, perdiem, ukumbi etc kazilipa yeye kwa fedha alizochangiwa na akina Robert Amsterdam!
Mbaya zaidi katika kampeni yake hiyo kakivua nguo chama chake na Mwenyekiti wake wa sasa. Yaani kakitukana, kakifedhehesha mbele ya umma hadi umma hauna hamu nacho tena.
Kakisambaratisha vibaya, Kakitwanga na kukiacha mahututi. Yaani kumbe Mbowe alikuwa akikiendesha chama hicho kidikiteta? Maamuzi ya vikao mbali mbali ya chama tuliyokuwa tunaambiwa kumbe yalikuwa ni ya Mbowe pekee? Tundu Lissu kakichafua sana chama chake.
Sasa mtu unabaki unajiuliza: Itakuwaje kama mamlaka husika ya chama ikikata jina lake kuwa mgombea wa kiti hicho? Itakuwaje hata kama mamlaka ikapitisha jina lake kuwa mgombea lakini kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama akishindwa na Mbowe? Ataweza kubaki kwenye chama hicho kweli? Ndiyo maana kanuni na taratibu za kampeni za uchaguzi zinakataza kuchfuana. Sasa huyu anachafua hadi chama chake.
Mamlaka za chama zikiamua kumfukuza kwenye chama ataenda wapi? CCM au ACT kwani kuanzisha chama chake Jaji Mtungi hatakubali kwani anamfahamu busara zake.
Kwa nini hakufuata busara za Msigwa? Alitakiwa kuondoka kwanza kwenye chama hicho ndipo ayaseme hayo aliyoyasema kwenye huo mkutano. Au angalifuata busara za Lowasa za kusubiri kuenguliwa na kufanya alichofanya.
Ngoja tusubiri. Ngoma inaweza kuwa tamu kuliko ile ya Lyatonga Mrema enzi zile alipokuwa NCCR - Mageuzi.
Alilishambuliaje chama?Wengi sisi ni wapenzi na washabiki wa Lissu, lakini kitendo chake cha kukisema chama hadharani si afya, kitendo cha kumshambuklia kiongozi wa taasisi hadharani si afya.
Lissu kashakosa maadili na nafikiri kaamua bila kufuata kanuni kwamba liwalo na liwe - kaamua kuisambaratisha CDM na msije mkashamgaa akasaidiwa na Msajili kumwomdoa Mbowe kama walivyofanya kwa NSSR Mageuzi. Mbatia aliondolewa kihuni kwa usaidizi wa Msajili.
CDM inatakiwa kiwa makini sana kwenye jambo hili vinginevyo tayari CCM itapenda kuweka mkono wake kumalizia kazi aliyoianzisha Lissu.
SI dhambi kutangaza nia lakini fuata taratibu basi na si kutangaza vita.
Katiba yao haina time limit wala mambo ya kung'atuka. Take from me atakayeng'atushwa ni Tundu Lissu mwanaharakati na kibaraka wa mabeberu
Hahaha Lisu huyu hawezi kuivusha CHADEMA, analia lia sana.
Alipewa TLS ikamshinda, hakufanya chochote, leo anaitaka CHADEMA bila Mbowe mtaja kusema humu humu kwamba anahujumiwa na Mbowe, lakini ukweli ni kwamba CHADEMA Lisu anaweza kelele tu lakini hawezi na hana uwezo kuendesha chadema.
CHADEMA siyo shule kwamba yeyote anaweza kuwa mwalimu mkuu, CHADEMA ni Tanzania, huwezo huo LISU hana jamani.
When you discussed about politics I can see you as stupid just leave your life remember "POLITICS ITS A DIRTY GAME"
Amepiga kimwanjoka cha mwaka.Huyo hata kiswahili lazima kinamsumbua.Elimu ya Tanzania ipo ICU, ndio kiengerza gani hiki?
Alitawala miaka 24, lakini baba yako akifanya makosa na kujifunza kwamba alifanya vibaya unatakiwa ujifunze kwake usirudie makosa. Usitumie makosa yake kutaka kurudia makisa na wewe.Kwani Mwl alitawala miaka mingapi ?.
Mbowe anavyozidi kuongea ndiyo anavyozidi kudhihirisha kuwa ana elimu ndogo.Haahaa juzi anasema Nyerere alikuwa eti ni mtumishi wa umma ndo maana alngatuka, nilishangaa Sana, kwani kiongozi wa chama sio wa umma?
Hivi elimu ndogo ni hadi kiwango gani?Mbowe anavyozidi kuongea ndiyo anavyozidi kudhihirisha kuwa ana elimu ndogo.
Ule.msemo wa "Kaa kimya ili watu wasijue ujinga wako" unamhusu sana Mbowe.
Hili jambo la ujinga wa Mbowe lilikuwa linafichika kirahisi wakati anaisema serikali na CCM, kwani hapo huhitaji elimu kubwa kuisema CCM. Huhitaji mambo mengi ya nuance. Hata mjinga anaweza kusema tu "Katiba mpyaa, tume huruu, peopleees, power" akaonekana ana akili.
Lakini, ukija kwenye issue kama kutetea kukaa kwenye uenyekiti muda mrefu kwenye nchi ambayo Nyerere kashaweka somo na standard, mpaka tumejifunza neno "kung'atuka", Mbowe ameshindwa kujenga hoja za kimantiki kwa nini yeye abaki. Kasema, kawafokea watu, halafu baada ya kusema kwa mihemuko kaja Lissu kapanga maneno vizuri, kwa hoja, kabla.Lissu hajatangaza kugombea uenyekiti mimi nikasema hapa mbona Mbowe kaongea pumba halafu Lissu ndiye kaongea vizuri?
Kumchoka kunaoneshwa kwenye sanduku la kura. Ukikionesha kwa mtindo aliofanya Lissu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kwa chama na mwenyekiti wake. It is insubordination to Mr Freeman Mbowe. Hili halikubaliki, hatua kali za kinidhamu zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Tundu Lissu.Ni kweli walikuwa wanamuunga mkono, sasa wameshamchoka.
Bw. Kiranga, jaribu kutofautisha Nyerere wa kabla ya uhuru na yule Nyerere wa baada ya uhuru.Kufanya kitu sahihi si lazima ulazimishwe na katiba.
Hata Nyerere alivyong'atuka urais, hakulazimika kung'atuka kwa sababu ya katiba. Katiba ilikuwa inamruhusu aendelee urais.
Si hivyo tu, wananchi wengi walikuwa bado wanamtaka Nyerere awe rais. Lakini akakataa kuendelea, akang'atuka. Hakuendelea urais kwa kusema katiba inamruhusu.
Kwa nini?
Alifanya vile kwa busara zake tu. Aliona kawa rais muda mrefu zaidi si vizuri, aliona awaachie wengine waendeleze kazi.
Kwa hiyo hoja ya "katiba yao haina kung'atuka" ni hoja mufilisi.
Ama kukaa madarakani mtu mmoja muda mrefu ni kitu kibaya, ama kukaa madarakani mtu mmoja muda nrefu si kitu kibaya. Regardless ya katiba inasema nini.
Mimi mpaka sasa nipo kwa Mbowe aliyekaa kwenye uenyekiti muda mrefu bila ya kuwa na chochote cha maana cha kuonesha. Kwa Lissu sijafika kwa sababu sina nia ya kufanya hiki suala kiwe la ligi ya Mbowe na Lissu. Inawezekana kabisa Mbowe akatolewa na mtu mwingine kabisa ambaye hata si Lissu akaongoza chama. Kuna watu tofauti na Mbowe na Lissu watagombea uenyekiti, so in principle, this is not a strictly Mbowe vs. Lissu race.
Mbowe natakiwa ajiondoe mwenyewe wakati bado anaheshimiwa kabla hajaondolewa kama Nicolae Ceausescu kwa kuvunjiwa heshima zote.
Kipindi cha kampeni ni kipindi hatari sana. Ni kipindi cha kubomoana. Busara na taratibu zinawatakq wagombea wabomoane kwa staha. Ndiyo maana kwa kuzingatia athari zake, kipindi hicho hupangiwa siku au wiki chache tu kabla ya uchaguzi wenyewe. Ratiba lazima izingatiwe. Huwezi ukaanza kufanya kampeni kabla ya filimbi ya kuanza kampeni aka kubomoana haijapulizwa. Tundu Lissu kaanza kabla ya filimbi haijapulizwa. Tarehe ya uchaguzi wala bado haijapangwa. Inawezekana ikawa hata mwezi wa nne mwakani. Sasa ataendelea kubomoa kwa miezi yote hiyo kabla ya uchaguzi? Hadi siku ya uchaguzi si atakuwa amebomoa kila kitu?Kuna uwezekano Mbowe mwenyewe amempa baraka Lissu ya kutangaza nia.
Hilo la Lissu kuonekana kama anakosoa chama na uongozi wa sasa ni muhimu sana. Hata JPM na CCM kwa ujumla walifanya hivyo 2015.
Hapa majuzi tu Kamala Haris alifanya kosa kama hilo la kuogopa kumkosoa bosi wake kwenye uchaguzi wa Marekani, aliulizwa ni kitu gani atafanya cha tofauti na Joe Biden, akasema hakuna atakachofanya cha tofauti. Alisema hivyo kwa kutotaka kumkosoa bosi wake. Kosa kubwa.
Lazima uoneshe tofauti yako na waliopo sasa ili kuwapa sababu watu ya kukuchagua. Kama hauna cha tofauti utakachokifanya kwanini watu wakupigie kura? Si afadhali waendelee na huyohuyo aliyepo?
NEC hupokea majina kutoka kwa vyama vya siasa, jina moja kwa kila chama kilicho na usajili kamili. Tundu Lissu hakupeleka jina lake mwenyewe huko NEC. Angalifanya hivyo halingalipokelewa. NEC haina ya kukata majina yaliyowakilishwa na vyama hali vya siasa.Mwaka 2020 NEC TANZANIA yenyewe haikukata jina la Lissu kugombea urais sembuse hao viongozi wa CHADEMA ambao ni vibaraka wa CCM! Unaota ndoto mbaya sana, Amka!
Kwa upande wa vyama vya siasa kasome katiba, kanuni na taratibu za kila chama ambazo huwa zimepitiwa na kukubaliwa na msajili wa vyama vya siasa kwa niaba ya serikali. Hizi zisipofuatwa msajili ana mamlaka ya kuwaadhibu wahusika.Tunaomba utusaidie huo utaratibu ulioanisha upo kwenye Katiba au Sheria ipi ili tupate rejea
Sasa kwani kuna mtanzania ambaye halijui hilo? Chadema kwa upande wa Tanzania bara kwa sasa ndiyo chama cha upinzani chenye wanachama na washabiki wengi na kimeenea kote. Na aliyewezesha hili kutokea ni Freeman Mbowe kwa kuwapokea Edward Lowasa na Sumaye kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.Kweli CHADEMA ni chama kikubwa,imara na chenye nguvu na mshikamano mkubwa sana Tanganyika.. Yaani mpaka leo bado mijadala zinaendelea baada tu ya TAL kutangaza nia ya kugombea uenyekiti siku tatu zilizopita
Viva CHADEMA! Viva forever📌🤣💪🏿❤❤❤
Kumchoka kunaoneshwa kwenye sanduku la kura. Ukikionesha kwa mtindo aliofanya Lissu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kwa chama na mwenyekiti wake. It is insubordination to Mr Freeman Mbowe. Hili halikubaliki, hatua kali za kinidhamu zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Tundu Lissu.Ni kweli walikuwa wanamuunga mkono, sasa wameshamchoka.
Kama lengo kuu la chama cha siasa cha upinzani ni kuung'oa utawala madarakani kama unavyosema, Mbowe anatakiwa kujiuzulu uenyekiti kwa sababu ameshindwa kutimiza lengo hilo over and over again.Kumchoka kunaoneshwa kwenye sanduku la kura. Ukikionesha kwa mtindo aliofanya Lissu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kwa chama na mwenyekiti wake. It is insubordination to Mr Freeman Mbowe. Hili halikubaliki, hatua kali za kinidhamu zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Tundu Lissu.
Bw. Kiranga, jaribu kutofautisha Nyerere wa kabla ya uhuru na yule Nyerere wa baada ya uhuru.
Nyerere wa kabla ya uhuru aliacha kazi yake ya umma kama mwalimu wa sekondari huko Pugu, na kwenda kujiunga na chama cha siasa cha TAA ambacho baadaye kiliitwa TANU na yeye akawa mwenyekiti wake. Lengo la TANU lilikuwa ni kuung'oa utawala wa Muingereza ili Tanganyika ipate uhuru. Aliacha mshahara wake mzuri wa ualimu. Kazi ya uenyekiti wa TANU haukuwa na mshahara wo wote. Ilikuwa ni kazi ya kujitolea. Kazi hiyo ilitegemea michango ya matajiri wa wakati huo hususani akina Sykes na baba yake na Freeman Aikel Mbowe ambao walikuwa wanaharakati wa mbio hizo za kuleta uhuru. Hivyo katika mbio hizo huwezi ukaweka muda wa ukomo wa uongozi wala mambo ya kung'atuka.
Nyerere wa baada ya uhuru alichaguliwa kwenye utumishi wa umma kwenye ngazi ya uraisi wa nchi na amiri jeshi mkuu. Pia aliendelea kuchaguliwa na chama chake cha TANU kilichoitwa baadaye CCM kama mwenyekiti wake. Katiba na sheria za nchi na zile za TANU hazikuwa na kipengele cha ukomo wa kugombea nafasi hizo. Baada ya kushika nafasi hizo kwa miaka takribani 25 mfululizo, busara yake ikamuongoza kung'atuka na kuweka utaratibu wa kikatiba wa ukomo wa miaka 10 kwenye vyeo hivyo serikalini na kwenye chama chake cha CCM.
Lengo kuu la vyama vya siasa vya upinzani kama CHADEMA ni kuung'oa madarakari utawala wa CCM, kama ilivyokuwa lengo kuu la TANU kabla ya uhuru ie kuung'oa utawala wa Muingereza. Mbio au harakati zote za vyama vya upinzani ni hilo. Uongozi wake ni wa kujitolea. Uendeshaji wake unategemea michango ya wanachama wake. Utumishi wao hauna mishahara, tofauti na wengi wanavyofikiria. Inashangaza hadi watu wanararuana na wakati mwingine kuuana kugombea vyeo kwenye vyama hivyo? Jee sababu ni kwenda kudokoa au kuiba hiyo michango ya wanachama ya kuendeshea chama chao? Freeman Aikel Mbowe alizaliwa siku ya uhuru wa Tanganyika. Baba yake alikuwa kati ya wanaharakati waliochangia kwa hali na mali kumng'oa Muingereza. Hivyo uanaharakati huo wa Mbowe ni wa kuzaliwa na kulelewa nao.
Kipindi cha kampeni ni kipindi hatari sana. Ni kipindi cha kubomoana. Busara na taratibu zinawatakq wagombea wabomoane kwa staha. Ndiyo maana kwa kuzingatia athari zake, kipindi hicho hupangiwa siku au wiki chache tu kabla ya uchaguzi wenyewe. Ratiba lazima izingatiwe. Huwezi ukaanza kufanya kampeni kabla ya filimbi ya kuanza kampeni aka kubomoana haijapulizwa. Tundu Lissu kaanza kabla ya filimbi haijapulizwa. Tarehe ya uchaguzi wala bado haijapangwa. Inawezekana ikawa hata mwezi wa nne mwakani. Sasa ataendelea kubomoa kwa miezi yote hiyo kabla ya uchaguzi? Hadi siku ya uchaguzi si atakuwa amebomoa kila kitu?
NEC hupokea majina kutoka kwa vyama vya siasa, jina moja kwa kila chama kilicho na usajili kamili. Tundu Lissu hakupeleka jina lake mwenyewe huko NEC. Angalifanya hivyo halingalipokelewa. NEC haina ya kukata majina yaliyowakilishwa na vyama hali vya siasa.
Kwa upande wa vyama vya siasa kasome katiba, kanuni na taratibu za kila chama ambazo huwa zimepitiwa na kukubaliwa na msajili wa vyama vya siasa kwa niaba ya serikali. Hizi zisipofuatwa msajili ana mamlaka ya kuwaadhibu wahusika.
Kwa upande wa uchanguzi wa serikali kasome katiba ya nchi, sheria na kanuni za uchaguzi
Sasa kwani kuna mtanzania ambaye halijui hilo? Chadema kwa upande wa Tanzania bara kwa sasa ndiyo chama cha upinzani chenye wanachama na washabiki wengi na kimeenea kote. Na aliyewezesha hili kutokea ni Freeman Mbowe kwa kuwapokea Edward Lowasa na Sumaye kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.
Hivyo mitifuano ye yote kwenye vyama hivi viwili (CCM na CHADEMA) vinaweza kuleta athari kwa mtanzania yeyote, mwanachama na asiye mwanachama hususani kutekana na kuuana kwa sababu za kisiasa. Na kwa kiasi kikubwa vyama hivi vinaendeshwakwa pesa ya kodi zetu kupitia ruzuku ya serikali.
Huko tunakoelekea Tundu Lissu anaweza kuiua CHADEMA na kuiacha Tanzania bara kuelea kwenye utawala wa chama kimoja, kitu ambacho hakipendezi.
Ukipewa wewe unaweza kutekeleza,ulichoandika hapa?Kama lengo kuu la chama cha siasa cha upinzani ni kuung'oa utawala madarakani kama unavyosema, Mbowe anatakiwa kujiuzulu uenyekiti kwa sababu ameshindwa kutimiza lengo hilo over and over again.