Sio kwamba nimekuambia hilo kwamba halina ushahidi, na kwa taarifa yako hata serikali haitaki liongelewe, kutokana na ukakasi wake. Huo uhayawani ndio ulipelekea kusitisha matangazo yote live ya uchaguzi, kwani wanajua nini kilikuwa kinafanyika kwenye vituo vya kura. Mahakama kwa sasa chini ya awamu ya tano, ni sehemu ya hizi hujuma. Ni hakimu gani asiyejua kundi la watu wasiojulikana?
Huyo DJ Hana ulazima wowote wa kususia uchaguzi, lakini ni wapi atapata wapiga kura? Wapiga kura wa ccm hawana cha kuogopa, maana wao ni wanufaika kwa hizi chaguzi za kishenzi. Je wapinzani watapata nini? Sisi wapiga kura wengi wa upinzani tunaojitambua, hatuko tayari kupiga kura chini ya tume hii isiyo huru ya uchaguzi. Na tunaendelea kushawishi watu wengi kutokupiga kura chini ya tume hii, na hilo tunafanikiwa sana. Kama ni maandamano ya amani kwa ajili ya kudai tume huru ya uchaguzi tutashiriki, na sio zaidi ya hapo. Tumechoka kupata viongozi wasio na ridhaa yetu.