Kuhusu kitisho kwenda ITV, kama una simu ya mtangazaji Sam Mahela aliyekuwa ITV kabla ya kuhamia TBC, kwani ndiye aliyerusha live covarage ya tukio lile, mpigie akuambie nini kilitokea. Mimi sina uwezo wowote kwa kupewa hiyo footage na ITV, kwani hata wao hawawezi kuthubutu kuitoa kama bado wanayo kwenye archive yao, maana hicho kituo kitakikuta kilicholikuta gazeti la Tanzania daima. Usitake kupotosha nilichosema, nimesema mabox ya kura yalitolewa vituoni mbele ya macho ya polisi, na msimamizi wa uchaguzi, na kurudishwa vituoni mbele ya macho ya polisi na msimamizi wa tume, na wala hawakuchukua hatua yoyote.
Daftari la kura halijawahi kuboreshwa toka mara ya mwisho 2015, hivyo kuna miaka mitano bila daftari kuboreshwa. Vijana ndio wengi, wangalau huko vituoni kusingepungua watu 4m+ wakijiandikisha na kuhuisha taarifa zao. Je umeona sign yoyote ya watu 4m+ wakiajiandikisha? Wakati wa kusajili line za simu kwa alama ya vidole tuliona misururu, mbona hatukuona misururu ya kujiandikisha wapiga kura?