Hii siyo mifano bali umetaja tu kesi zilizokua mahakamani. Onyesha ni wapi ambapo mahakama haikutoa haki wakati sheria ipo wazi halafu ikapindishwa? Tatizo lenu kila Kesi inayomhusu mpinzani ili mahakama ionekane ipo huru basi lazima huyo mpinzani ashinde kinyume na hapo hiyo mahakama haipo huru inashinikizwa. Sasa sheria hazipo hivyo na wala haziangalii watu usoni.
Nikitolea tu mfano mzuri wa kesi ya Lissu na Spika. Mawakili wenu walifanya kosa la kiufundi badala ya kwenda mahakamani kupinga uchaguzi usifanyike ili kesi msingi isikilizwe kwanza, wao wakasubiri mpaka uchaguzi umefanyika halafu ndo wakaenda mahakamani kupinga mbunge mpya asiapishwe ili kesi ya lissu kuvuliwa ubunge isikilizwe. Sasa kisheria unapopinga mbunge asiapishwe maana yake unapinga utaratibu wa kuchaguliwa kwake. Mahakama ilipowauliza Kuna sheria au Kanuni gani zimekiukwa kwenye uchaguzi ili wazuie asiapishwe, jibu lao eti Lissu alivuliwa ubunge isivyo halali. Mahakama ikauliza tena kwann hakumzuia uchaguzi usifanyike kwanza? Hawakua na majibu. Kuvuliwa ubunge kwa Lissu na kuchaguliwa kwa mbunge mpya kuna mahusiano gani? Wakakosa majibu. Mahakama ilipotoa rulling mbunge aapishwe, kosa Lipo wapi?