Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Status
Not open for further replies.
sheria inasemaje!
Hao sheria haiwaruhusu kupiga kura, wasubirie kushangilia. Wangekuwa na akili, wangelalamika mapema may be Nec wangelifanyia kazi.

Isije kuwa ni zile shahada zilizonunuliwa na magamba
 
Wameshindwa kupokea Elimu ya kuzikataa Tshirt, Kanga na Vilemba vya rangi ya njano na kijani magamba wanavyotumia kama chambo kuwanasa. Hatuna ujanja zaidi ya kutumia mbinu walizotuachia babu zetu, hadi pale TAKUKURU watakapoanza kuzuia rushwa ya manguo ya njano na buku buku za magamba. When one door is closed others are open
Ni kwel kabisa mkuu. Nakina mama wengi ni kama watu wa Tanga, wanapenda sana marangi rangi, hasa kijani na njano. Angalia hata mabasi yao, kama BEMBEA! Dawa ni kuwafichia kadi au kuwafungia ndani siku ya uchaguzi. Saa 12 jioni wapishane na kuku milangoni, kudadeki zao! Wanatumia demokrasia vizuri? Nchi ingefika hapa ilipofika? Tarime na Musoma Mjini mmetupa good lesson, ni sisi tu kufuata somo hilo. Lakini lgunga washachelewa!
 
Nimeambiwa na jamaa yangu aliye Igunga sasa hivi kwamba mamia ya vijana wameanza kujitokeza vituoni kupiga kura.Tuombe Mungu hali iwe hivihivi kila kona.

Nimeongea asubuhi hii na Mh. Lema akiwa Igunga kwa simu, kaniambia kuwa ana uhakika CHADEMA itashinda.
 
Wataruhusiwa kweli jamani?! Hii si watakua wamekosa haki yao ya msingi

Dena ukitafakari sana kuhusu democrasia ya nchi yetu unaweza kuugua wazimu hebu tungoje labda wataruhusiwa. Alafu kuna wengine no za id zimetofautiana na za kwenye daftari. Jamani lakini ni uzembe wa mwandishi kwanini wamnyime kupiga kura yani me nakasirika wanavyobaka democrasia.
 
gari ya ccm inapita mitaani kwenye kata ya nyandekwa ambayo ni ngome ya chadema ikitangaza kuwa mgombea wa chadema amejitoa,
diwani wa ccm kata ya nkinga alikuwa anatisha wapiga kura,lakini ameshughulikiwa na vijana wa chadema

Mkuu,
Lifanyieni shooting hata kwa simu tuje kuiweka hewani! P/se!
 
SIO siri, kwa mtu aliye mtaalamu wa kusoma hisia za watu kutokana na personality zao ikiwa ni pamoja na body expression na uongeaji, basi hana shaka pale atakapokuwa anawaelezea watu fulani fulani! Nafuatilia uchaguzi wa Igunga kupitia Chanel 10 ambao hivi sasa wanarusha LIVE! Mistari inaonekana ikiwa na watu walio na nyuso na ambao hata mavazi yao yanatosha kuwaelezea ni watu wa namna gani!! Vijana wapo, lakini wengi wao si wale ki-facebook au ki-hip hop ambao naamini ni mtaji tosha kwa CHADEMA!!! Wanaoonekana hapa ni wale walioundwa na nyuso za kiungwana zisizopenda shari!!! Sina shaka yoyote kwamba, hapa CDM hawana chao; si kutokana na kuibiwa kura bali kutokana na kushindwa kwa halali kabisa!!

Umemaliza?
 
Mwandishi wa ITV.

Kituo cha Upumbulya.

ID za baadhi ya vitambulisho ni tofauti na zile zilizo kwenye majina yaliyoko kwenye documents za NEC.

Sasa hapa wadau msnisaidie. kwani NEC wanatunza data za wapigakura kwa database au kwa Excel?

Mwanahabari anasema watu wanapiga kura na kuondoka kwa maana wengi wanaonekana wako na nidhamu na ni waoga.

Tatizo la Wasimamizi wa Uchaguzi kubadilisha ID za wapiga kura limekuwa ni kero sasa. Mimi mwaka 2010 sikupga kura kwa sababu hiyo. Nilikuta ID yangu ni tofauti na iliyo kwenye Daftari la kupigia kura. Ni njama mbaya na dhalimu za CCM.
 
Kashindye (ambaye ni mgombea wa CHADEMA) kahojiwa sasa hivi ITV baada ya yeye kupiga kura na kusema kwa hapo alipo hali ni shwari ila atapata uhakika zaidi ya mwenendo wa uchaguzi baada ya kutembelea vituo zaidi ya kumi.

Amesema yupo postive na matokeo yoyote yatakayotoka lakini ana uhakika wa yeye kufanya vizuri na kuibuka kidedea.
 
SIO siri, kwa mtu aliye mtaalamu wa kusoma hisia za watu kutokana na personality zao ikiwa ni pamoja na body expression na uongeaji, basi hana shaka pale atakapokuwa anawaelezea watu fulani fulani! Nafuatilia uchaguzi wa Igunga kupitia Chanel 10 ambao hivi sasa wanarusha LIVE! Mistari inaonekana ikiwa na watu walio na nyuso na ambao hata mavazi yao yanatosha kuwaelezea ni watu wa namna gani!! Vijana wapo, lakini wengi wao si wale ki-facebook au ki-hip hop ambao naamini ni mtaji tosha kwa CHADEMA!!! Wanaoonekana hapa ni wale walioundwa na nyuso za kiungwana zisizopenda shari!!! Sina shaka yoyote kwamba, hapa CDM hawana chao; si kutokana na kuibiwa kura bali kutokana na kushindwa kwa halali kabisa!!

Unafikiri hadi kufikia 2015 bado wenye sura zilizochoka ndio watakuwa majority? kama wenye sura za kisharobaro walikuwa 600,000 mwaka 2005, wakaongezeka na kufika 2,000,000 mwaka 2010, unafikiri mwaka 2015 watakuwa wangapi? Kama waliokuwa na sura zilizochoka mwaka 2005 walikuwa 9,000,000 wakapungua hadi 4,000,000 kwaka 2010, unadhani hadi 2015 watakuwa wamebaki wangapi?

Najua hesabu ni tatizo shuleni, so hii assignment huiwezi
 
huyu dada yetu fatuma wangempa kiti na yeye akae kidogo.mwenzake masako kakaa.wangemletea kiti kirefu kama cha bar.wenzao cnn wanasimama wanaletewa kiti maji juice na mandazi.mia

na "long" aliovaa inaharibu baraka zote za jpili
 
SIO siri, kwa mtu aliye mtaalamu wa kusoma hisia za watu kutokana na personality zao ikiwa ni pamoja na body expression na uongeaji, basi hana shaka pale atakapokuwa anawaelezea watu fulani fulani! Nafuatilia uchaguzi wa Igunga kupitia Chanel 10 ambao hivi sasa wanarusha LIVE! Mistari inaonekana ikiwa na watu walio na nyuso na ambao hata mavazi yao yanatosha kuwaelezea ni watu wa namna gani!! Vijana wapo, lakini wengi wao si wale ki-facebook au ki-hip hop ambao naamini ni mtaji tosha kwa CHADEMA!!! Wanaoonekana hapa ni wale walioundwa na nyuso za kiungwana zisizopenda shari!!! Sina shaka yoyote kwamba, hapa CDM hawana chao; si kutokana na kuibiwa kura bali kutokana na kushindwa kwa halali kabisa!!

hao hawana elimu hawajui haki yao ..mtawanyonya sana ila mwisho utafika tu kwani tanzania yote haina vijana kama hao mbumbumbu ambao ni mtaji wenu ccm....na kama unaidharau facebook nenda kamuulize mubarak
 
Upigaji kura umeanza rasmi saa ngapi hali ikoje, kila kituo kimeanza kazi? Nifahamisheni tafadhali wadau....
 
Halahala yasije yakatokea ya kule songea Nchimbi kukimbia na masanduku ya kura! magamba ktk hili wamefuzu kinomaaaaaaaaaaa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom