Mda mfupi uliopita nilikuwa natizama TBC wakimuhoji mama mmoja aliye jitambulisha kwa jina la Mwajuma Shabani, amedai kuwa walilazimishwa na balozi wa nyumba kumi ambaye alikuwa anaorodhesha majina na namba za vitambulisho vyao kukipigia kura chama flani ambacho hakikitaja jina, Mwisho kamalizia kwa kusema kuwa amekipigia chama anachokipenda na siyo kile alichokuwa akilazimishwa kukipigia kura..
Inapendeza sana kuona hakina mama nao hawako nyuma wanasimama kutetea kile wanacho amini ni sahihi kwa licha ya vitisho vyote hivyo walivyopewa, Hakika elimu ya Makamanda wetu imewaingia vizuri ndugu zetu wa Igunga..
Nampongeza huyu mama kwa kuwa jasiri, wanaohusika natumaini wamemsikia huyu mama sasa niwakati wakumchukulia hatua huyo balozi na aeleze hizo namba za shahada alikuwa anazichukua za nini?na kwa nini awatishe watu.