SaintErick
Member
- Aug 7, 2013
- 90
- 53
Mchakato wa uchaguzi wa viongozi hua ni mgumu na mrefu na hivyo huruhusu makosa ya kibinadamu na kimfumo na kiteknolojia kutokea katika mchakato huo. Tatizo kubwa Afrika ni Kutokukubali matokeo ya mwisho kwa washiriki wa uchaguzi na katika nchi nyingi kushindwa kupinga matokeo mahakamani kwani sheria nyingi ni za kikoloni.
Hili sio suluhisho pekee linalohitajika bali ni moja kati ya yale ambayo yanaweza kuongeza imani na kuondoa marumbano. Nchini Marekani serikali za majimbo zina kanuni ambazo huruhusu kuhesabiwa upya kwa kura ikiwa Wagombea wawili wamekaribiana sana hasa ikiwa tofauti ya kura ni chini ya 0.5% lakini baadhi ya majimbo ikiwa chini ya 1%.
Na katika historia ya Marekani ni imefanyika mara 27 pekee na mara 3 wagombea ambao hawakushinda waliweza kushinda katika marudio ya uhesabuji kura.
Hata hivyo, kwetu tunaweza kuongeza kanuni ili kuendana na mazingira yetu. Mtu akitaka kuhakiki kwamba ameshindwa kihalali basi kufanyike Recount. Nchini Marekani wagombea walioshinda huwaunga mkono ambao wameshindwa na wanatafuta Recount ili kuhakikisha hawakushinda kwa upendeleo.
Ikiwa uchaguzi wetu tunaweza kujivunia kwamba ni wa huru na haki basi turuhusu kurusmdiwa kuhesabu kura kwa njia yoyote iwe ya kibinadam au kiteknolojia.
Gharama za zoezi ziwe katika mafungu kuazia tume ya Uchaguzi, Vyama vya kisiasa na Wagombea binafsi. Pale haja inapotokea sheria ziwe wazi kuruhusu tukio hili.