Uchaguzi Mkuu TFF - 27 Oktoba 2013: Jamal Malinzi Rais Mpya wa TFF!

Uchaguzi Mkuu TFF - 27 Oktoba 2013: Jamal Malinzi Rais Mpya wa TFF!

I wish ningekuwa nawajua vyema hawa candidates
Ila naomba tuu apatikane atayeipandisha soka na sio kulishusha
Ivi yupi ni yanga na yupi ni simba?
 
Wapinzani wa malinzi wanadai kama j malinzi akishinda, katibu mkuu anakuja kuwa m.wambura!
 
Mwanajf mwenzetu asishinde?!..haiwezekani. Mia

Mkuu kuna vituko halafu mimi nafuatiliwa mwenendo wangu tangu mwaka jana niwalipue na ile zkaunti yao wanayosaini wawili tenga na nyamlani,wameniwekea walinzi kila koma hata hiki kiganyio changu wananichunga sana,lakini sio mbaya sana tutaperekana hivyo hivyo hadi mwisho nikipata nafasi,wzmemaliza kujieleza wajumbe wa kamati ya utendaji wanataka kupiga kura kisha wanaingia makamu rais.
 
Hawa wanaweza kutuharibia au kulikomboa soka la tanzania tunawategemea sana wajumbe wetu.
Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu).

Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6- Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na Mbeya).

James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani).

Davis Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam). Mia
 
Mkuu kuna vituko halafu mimi nafuatiliwa mwenendo wangu tangu mwaka jana niwalipue na ile zkaunti yao wanayosaini wawili tenga na nyamlani,wameniwekea walinzi kila koma hata hiki kiganyio changu wananichunga sana,lakini sio mbaya sana tutaperekana hivyo hivyo hadi mwisho nikipata nafasi,wzmemaliza kujieleza wajumbe wa kamati ya utendaji wanataka kupiga kura kisha wanaingia makamu rais.

Mkuu wanapiga mande hiyo lD hapa jf?
 
Mkuu WABHEJASANA kunani tena mbona una hamaki kuna nini tena?
Btw, wewe ni mpiga kura katika mkutano wa leo ama ni mlinzi wa kura za Malinzi?

Mkuu samahani sana kwa kuvhelewa kukujibu,hawa wakuda wana mambo ya ajabu sana wameniwekea ulinzi wa kipumbavu sana mi ni mpiga kura lakini nimeshasumbuana nao sana tangu uchaguzi ulipoanza hawa,taki Malinzi kabisa wanaleta mambo ya ajabu sana,kwa mfano ilikuwa tuanze kupiga kura za rais kushuka chini kwa sababu hapo ndipo kuna kila kitu lakini ghafla wamebadilisha na kuanza na wajumbe wa kamati ya utendaji!!lakini ngoja kwa sbb naona wameganya makosa na kuruhusu watu kuingia na bastola humu mi sijui!!
 
Last edited by a moderator:
Sasa ni zamu ya Wagombea nafasi y urais!ameanza Nyamlani na anamalizia kujieleza!huyu kweli ni mburula akishinda zinapigwa humu ila kuna majumbe hapa n hasa ya Arusha sijui yalipewa nini!!
 
Mla rushwa hapewi ng'o

malinzi mwenyewe mroho wa madalaka yalimshnda ya yanga anataka tff kakamia sana.. kushnda
 
I wish ningekuwa nawajua vyema hawa candidates
Ila naomba tuu apatikane atayeipandisha soka na sio kulishusha
Ivi yupi ni yanga na yupi ni simba?

hatujui, ila tunajua kuwa nyamlani ni ccm
 
Wakuu bila shaka leo ndio siku iliyokua ikisubiliwa kwa hamu na wadau wa mpira wa miguu Tanzania.

Nini kinaendelea huko?

Maana nimepitia humu ndani sijaona post yoyote inayoelezea updates za uchaguzi Mkuu wa TFF,au siyo leo?

Tunaomba updates please.

UPDATES:

- Wallace Karia ameshajinadi...
- Makamu wa pili wa rais, Ramadhani Nassib anajinadi mbele ya wajumbe...
- Mwenyekiti wa uchaguzi anamwomba Nassib anadi sera zake na si kuwazungumzia wagombea wengine...
- Madega ametinga shati jeupe na tai nyeusi. Anasema yeye ni Seneta na kazi yake ya uanasheria inampa muda zaidi...
- Madega anasema pamoja na kuwahi kuiongoza Yanga anamtoa wasiwasi Aden Rage kuwa hatoipendelea Yanga..!
- Ajabu ya mkutano mkuu huu ni kuwa hata safari hii Yanga hawakuleta mjumbe mpiga kura. Yussuf Manji jina lake limeitwa lakini hakuonekana. Simba inawakilishwa na Aden Rage...
- Rage anamtania Madega kwa kutaka ufafanuzi wa Useneta wake; wa Marekani au wa Jangwani?
- Madega anasema aliwahi kujiuzuru Yanga kwa uzembe wa uongozi hivyo yeye akichemsha kazi suala la kujiuzulu si halina mjadala
- Wanafuatia Malinzi na Nyamlani: Kaanza Malinzi, anasema sisi wote ni familia ya mpira. Tuyasahau ya nyuma, anamshukuru Tenga. Anazungumzia ilani yake. Anasema iko kwenye Facebook, Twitter na kwengineko... Anaendelea kutoa historia yake

Ahsante sana Mendieta, ahsante kwa Updates! Please usiache hata kidogo. Endelea kutujuza na matukio madogo madogo pia usiache
 
Sasa ni zamu ya Wagombea nafasi y urais!ameanza Nyamlani na anamalizia kujieleza!huyu kweli ni mburula akishinda zinapigwa humu ila kuna majumbe hapa n hasa ya Arusha sijui yalipewa nini!!

Machalii wa Arusha wamelambishwa unga wa ndere, si tumeambiwa nyamlani iko gawa mpunga mwingi sana kwa wajumbe!
Hapo kwenye bastola hapo...!!! Tutalaumiana muda si mrefu...
 
Kama tunataka kuuwa soka Tanzania wampe Nyamlani namfahamu ni fisi mwenye tamaaa

Nyamlani mwizi sana...mla rushwa mkubwa pale kinondoni mahakamani...anachukua hela halafu anapiga watu mvua
 
Machalii wa Arusha wamelambishwa unga wa ndere, si tumeambiwa nyamlani iko gawa mpunga mwingi sana kwa wajumbe!
Hapo kwenye bastola hapo...!!! Tutalaumiana muda si mrefu...

Waruhusu watu waingie na mashoka kabisa
 
Leteni matokeo bana....au wanapika matokeo
 
Back
Top Bottom