Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
1962 mondlane aliasisi chama Kikongwe kwa ajili ya kuikomboa msumbiji kutoka kwenye makucha ya wareno !kutoka na Hali ya msumbiji nyakati hizo iliwalazimu frelimo kuweka makao yake makuu jijini dar es salaam! Mapambano makali wakisaidiwa na serikali ya Tanzania chini ya jemedari hayati mwalimu Nyerere ! 1975 frelimo ilifanikiwa kuingia madarakani rasmi na ofisi zikahamishiwa mjini maputo ! Frelimo ilijulikana kama chama Cha ukombozi na raia wengi walikufa ili kuipigania frelimo ,Kuna watu wapo kaburini mpaka Leo walikufa kabla hata frelimo haijakalia mamlaka ! Huko walikolala hawajui kama frelimo ya Leo ipo kwenye kikaango Cha kuondolewa madarakani kwa nguvu na raia walio choka kabisa na wanatamani kuiona msumbiji ikiwa chini ya chama kingine ! Frelimo iliongozwa na samora machel ,kisha joachimu chisamo ,akafuata Philip nyusi na sasa guebuza ! Tujifunze jambo hapa wananchi hawatawaliwi Bali wanaongozwa ! Tukiendelea kuamini kwamba wananchi wanatawaliwa kwa mitutu ya bunduki zama hizo zimebadilika! Ione msumbiji Leo tangia uchaguzi ufanyike mpaka Leo maputo haikaliki Tena ! Kila kitu kimeharibiwa na vijana hawamtaki utani wanasonga huku mamia ya vijana wakiwa tayari wameuwawa ! Vijana wameacha kabisa uoga ! Tunapoelekea uchaguzi mkuu tujifunze jambo kutoka kwa majirani zetu ! Tushinde kwa haki chaguzi zetu ,tufanye mambo kwa weledi bila tamaa ,aliyeshinda atangazwe kwa uwazi na uhalisia ,kinyume chake ipo siku wananchi wataifuta haki yao kwa njia isiyo nzuri kabisa mungu ibariki Tanzania