matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Kinachofanya uonekane unakashikashi ni mitandao tu ya kijamii.
Ila huko kwenye uhalisia utadhani hatuko kwenye Uchaguzi.
Napita mitaani hakuna anayezungumzia. Ukiacha mabango ya CCM ambayo yametapakaa jiji zima LA DSM, yaani hata Bango la diwani ni kali kuliko la mgombea Rais yoyote wa upinzani hapo NATO hayaonekani, pamepoa mno.
Nilisafiri Mwanza DSM nikawa naangalia harakati za kisiasa mabarabarani sioni chochote.
Chakushangaza hata watu Wawili walipojaribu kujadili, Dereva aliongea kwa kipaza sauti kwa ukali na hofu Kubwa kukataza mjadala huo. Ila nakumbuka 2005 ndani ya treni Mwanza DSM behewa zima tulijadili hadi tukasinzia.
Cha ajabu leo kwenye daladala tulikuwa tunajadili kana kwamba huo Uchaguzi hautuhusu ni wa watu flani au nchi nyingine. Mfumo huo wa kujadili ulinishangaza hata mimi nilijishangaa. Kwanza sina hamu kabisa hata kusikia Lissu au Magufuli wanasema nini.
Najiuliza tatizo ni nini?
Je, ni uwekezaji mdogo wa rasilimalifedha?
Je, watu tumechoka siasa?
Je, siasa zimehamia online?
Je, maisha magumu hivyo kila mmoja anapambana na hali yake?
Mini maoni yako kama angalau na wewe umeona hii tofauti.