Uchaguzi Rais 2015: Utabiri Wa Mshindi Baina ya CCM na CHADEMA

Uchaguzi Rais 2015: Utabiri Wa Mshindi Baina ya CCM na CHADEMA

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Lifuatalo ni zoezi la utabiri juu ya mshindi Urais uchaguzi Mkuu 2015 baina ya CCM na Chadema; Lakini kabla hatujaenda kwenye hatua nyingine yoyote, ningependa kuwasilisha takwimu za idadi ya wapiga kura kwa kila mkoa Tanzania kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi (NEC); Ni dhahiri takwimu hizi zitaendelea kubadilika jinsi tunavyo karibia mwaka 2015, lakini halitakuwa tatizo kwani tutaendelea kufanya marekebisho accordingly;

[TABLE="width: 469, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]MKOA[/TD]
[TD]IDADI YA WAPIGA KURA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1[/TD]
[TD]ARUSHA[/TD]
[TD]723,874[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2[/TD]
[TD]DAR ES SALAAM
[/TD]
[TD]1,912,662[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3[/TD]
[TD]DODOMA
[/TD]
[TD]849,561[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4[/TD]
[TD]IRINGA
[/TD]
[TD]758,262[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5[/TD]
[TD]KAGERA
[/TD]
[TD]1,048,294[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6[/TD]
[TD]KIGOMA
[/TD]
[TD]666,114[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7
[/TD]
[TD]KILIMANJARO[/TD]
[TD]739,529[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]8
[/TD]
[TD]LINDI
[/TD]
[TD]450,620[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]9[/TD]
[TD]MANYARA
[/TD]
[TD]533,894[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]10[/TD]
[TD]MARA
[/TD]
[TD]752,906[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]11[/TD]
[TD]MBEYA
[/TD]
[TD]1,056,126[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]12
[/TD]
[TD]MOROGORO
[/TD]
[TD]988,113[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]13
[/TD]
[TD]MTWARA
[/TD]
[TD]658,220[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]14[/TD]
[TD]MWANZA
[/TD]
[TD]1,586,919[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]15[/TD]
[TD]PWANI
[/TD]
[TD]518,841[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]16[/TD]
[TD]RUKWA
[/TD]
[TD]489,289[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]17[/TD]
[TD]RUVUMA
[/TD]
[TD]607,920[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]18[/TD]
[TD]SHINYANGA
[/TD]
[TD]1,380,953[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]19
[/TD]
[TD]SINGIDA
[/TD]
[TD]545,074[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]20[/TD]
[TD]TABORA
[/TD]
[TD]840,014[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]21[/TD]
[TD]TANGA
[/TD]
[TD]891,942[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]22[/TD]
[TD]* ZANZIBAR
[/TD]
[TD]15,540[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD] JUMLA[/TD]
[TD]18,014,667[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

  • BLUE maana yake ni Ngome za uhakika za Chadema;
  • KIJANI maana yake Ngome za uhakika za CCM;
  • NYEKUNDU maana yake ni Mikoa ambayo hivi sasa ni 'Toss Up' au Sadakalawe;

Kabla ya kusonga mbele kwenda kwenye hatua nyingine za zoezi hili, ningependa kufahamu:

  • Je, wengi wetu mnashauri au mna mtazamo tofauti na picha niliyowalilisha hapo juu kuhusu mikoa gani ni ngome ya nani na mikoa gani ni sandakalawe? Kumbukeni, hili ni zoezi la utabiri tu; Lengo langu katika hatua hii ya awali ni kujaribu tukifikie muafaka juu wapi ni BLUE, GREEN na RED, (KWA HOJA), halafu tutaingia kwenye hatua zinazofuata; Ni imani yangu kwamba mjadala huu utatusaidia kuwa na mjadala ambao utakuwa more organized, interesting, and consistent, kuelekea 2015; Natumaini hoja kwamba hiki au kile ni siri ya ndani ya chama na kwahiyo haziwezi jadiliwa hadharani, hazitakuwa na nafasi katika mjadala huu;

Tukishirikiana, hakika tutajifunza mengi;
 
Mkuu Mchambuzi,kwanza nadhani thread hii itatumika na vyama vyote kuwasaidia waelewe ni wapi panahitajika kupafanyia kazi kuelekea uchaguzi mkuu 2015.

However nilikuwa na ombi moja;je kuna uwezekano wa kutuwekea rekodi za kura zilizopatikana kwa kila chama kwenye hiyo mikoa ambayo inaelekea kuwa ni ngome zao?

Kwa mfano kwenye mkoa wa Arusha ambao ni ngome ya chadema,waliojiandikisha ni 723,874,je kati ya hao ni wangapi waliipigia kura chadema?Nadhani ukiongeza na information ya kuhusu idadi za waliopiga kura kwenye mikoa hiyo,itasaidia kuupanua zaidi mjadala huu na kuweka mwangaza zaidi.

Kwa mfano,jumla ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye mikoa ambayo ni ngome ya ccm,ni 6,973,509,wakati jumla ya kwenye mikoa ambayo ni ngome ya chadema ni 5,724,347.Ikiwa na maana kwamba ngome ya ccm imeizidi ngome ya chadema kwa kuwa na wapiga kura wengi waliojiandikisha(6,973,509-5,724,347=1,249,162).Kwahiyo tukipata pia idadi ya waliopiga kura kwa ccm na chadema kwenye hiyo mikoa ambayo ni sadakalawe,basi tutaweza kuona wapi kila chama kili zembea ama ni wapi kitahitajika kuwekeza nguvu na ni nguvu za aina gani.Maana nilishangazwa kusikia jinsi ambavyo wananchi wengi walijiandikisha kupiga kura kwenye mkoa wa Arusha kata ya daraja mbili,na hawakupiga kura,mkoa ambao ni ngome ya chadema.

Kama kuna uwezekano wa kupata idadi ya waliopiga kura(kwa chama),kwenye mikoa yote hiyo hapo juu,itatusadia pia kujuwa ni mikoa gani kati ya hiyo ya sadakalawe ambayo inahitaji attention zaidi.Je kuna uwezekano wa kupatikana kwa hizo takwimu za waliopiga kura na vyama walivyovipigia kura?

Pia inaonekana kamavile chadema ni maarufu zaidi kwenye mikoa michache ambayo hata hivyo ina wapiga kura wengi waliojiandikisha tofauti na ccm ambayo ni maarufu zaidi kwenye mikoa ambayo ina wananchi wachache waliojiandikisha kupiga kura.Pia nadhani mikoa hiyo iko nyuma kimaendeleo(except for Mwanza), kuliko mikoa mingine ambayo ni ngome ya chadema.Hilo linaonyesha kuwa nguvu ya ccm ni ujinga wa wananchi.

Mwisho,nadhani hapo kwenye "toss up",ni "sadakalawe" na si "sandakalawe"
 
Mkuu Mchambuzi, nionavyo mimi kwa upande wa idadi ya wapiga kura uko sahihi+or -20%, ila;
Kuelekea 2015 ngome zote zitakuwa zimevunjwa, itategemea M4C itaendeleaje, itategemea kama CCM itajivua gamba na kuachana na rushwa na kama referee atakuwa huru na pia itategemea stability ya viongozi wakuu wa vyama hasa CCM na CHADEMA kubaki kwenye vyama vyao au kuvihama.

Udini wa CCM utaiathiri kidogo CHADEMA, lakini utaiathiri zaidi CCM yenyewe na utaifaidisha zaidi CUF.

CUF itaongeza wabunge bara lakini bado itaachwa mbali na CHADEMA na CCM. Vyama vya CUF na CCM vitakuwa pamoja vikishindana na CHADEMA kwa upande mwingine.

Kama afya zao zitakuwa njema( tunategemea zitakuwa njema) Wagombea wa urais wa vyama hivi watakuwa Mh. Prof. Lipumba-CUF, Mh. Lowasa-CCM na Dr. Slaa-CHADEMA.

Kuna uwezekano baadhi ya viongozi wa CCM zaidi ya 12 kuhamia chama kingine hasa kuvua gamba na kuvaa gwanda na kuimega CCM, na vile vile kuna uwezekano wa baadhi ya viongozi wawili au zaidi kidogo wa CHADEMA kuondoka CHADEMA kwa kushawishiwa na nguvu ya pesa au tu usaliti na hii itafanyika dakika za mwisho kuelekea uchaguzi.
Matukio haya yanaweza kubadili kabisa mwelekeo wa siasa za Tanzania.

Polisi watakuwa na upande lakini watakosa nguvu kwa sababu kubwa tatu; kwanza wengi wa polisi wa ngazi ya kati na wa chini watataka mabadiliko, pili usalama wa taifa watagawanyika na tatu Askari jeshi hawatakuwa na upande wowote
 
Mwanza, Shinyanga na Kigoma ni blue hiyo mikoa CCM haina nafasi usiweke sandakarawe kuiplease CCM nikiwa kama mwenyeji wa hiyo mikoa hiyo Mwanza na Shinyanga CCM hawatakiwi bali wanasurvive kwa kutumia mabavu na Kigoma watavote CHADEMA kama si NCCR-Mageuzi
 
Mkuu Mchambuzi,kwanza nadhani thread hii itatumika na vyama vyote kuwasaidia waelewe ni wapi panahitajika kupafanyia kazi kuelekea uchaguzi mkuu 2015.

However nilikuwa na ombi moja;je kuna uwezekano wa kutuwekea rekodi za kura zilizopatikana kwa kila chama kwenye hiyo mikoa ambayo inaelekea kuwa ni ngome zao?

Kwa mfano kwenye mkoa wa Arusha ambao ni ngome ya chadema,waliojiandikisha ni 723,874,je kati ya hao ni wangapi waliipigia kura chadema?Nadhani ukiongeza na information ya kuhusu idadi za waliopiga kura kwenye mikoa hiyo,itasaidia kuupanua zaidi mjadala huu na kuweka mwangaza zaidi.

Kwa mfano,jumla ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye mikoa ambayo ni ngome ya ccm,ni 6,973,509,wakati jumla ya kwenye mikoa ambayo ni ngome ya chadema ni 5,724,347.Ikiwa na maana kwamba ngome ya ccm imeizidi ngome ya chadema kwa kuwa na wapiga kura wengi waliojiandikisha(6,973,509-5,724,347=1,249,162).Kwahiyo tukipata pia idadi ya waliopiga kura kwa ccm na chadema kwenye hiyo mikoa ambayo ni sadakalawe,basi tutaweza kuona wapi kila chama kili zembea ama ni wapi kitahitajika kuwekeza nguvu na ni nguvu za aina gani.Maana nilishangazwa kusikia jinsi ambavyo wananchi wengi walijiandikisha kupiga kura kwenye mkoa wa Arusha kata ya daraja mbili,na hawakupiga kura,mkoa ambao ni ngome ya chadema.

Kama kuna uwezekano wa kupata idadi ya waliopiga kura(kwa chama),kwenye mikoa yote hiyo hapo juu,itatusadia pia kujuwa ni mikoa gani kati ya hiyo ya sadakalawe ambayo inahitaji attention zaidi.Je kuna uwezekano wa kupatikana kwa hizo takwimu za waliopiga kura na vyama walivyovipigia kura?

Pia inaonekana kamavile chadema ni maarufu zaidi kwenye mikoa michache ambayo hata hivyo ina wapiga kura wengi waliojiandikisha tofauti na ccm ambayo ni maarufu zaidi kwenye mikoa ambayo ina wananchi wachache waliojiandikisha kupiga kura.Pia nadhani mikoa hiyo iko nyuma kimaendeleo(except for Mwanza), kuliko mikoa mingine ambayo ni ngome ya chadema.Hilo linaonyesha kuwa nguvu ya ccm ni ujinga wa wananchi.

Mwisho,nadhani hapo kwenye "toss up",ni "sadakalawe" na si "sandakalawe"

jmushi1,

Nashukuru kwa kuona umuhimu wa zoezi hili; Takwimu za kila mkoa zipo lakini wachangiaji wengi wamekuwa wananajenga hoja kwamba takwimu za mwaka 2010 zilichakachuliwa kwahiyo hazifai kutumiwa kwa uchambuzi wowote wa kina; wewe una mtazamo gani juu ya hili? vinginevyo itarahisisha sana zoezi letu hili;

Nashukuru kuhusu corrections za sadakalawe, maisha yangu yote nimekuwa najua ni sandakalawe;
 
mkuuu mchambuzi mwanza umemaanisha mwanza jiji ama mkoa? maaana mwanza imetengwa tayari watu wa ccm hawapo jijini tena...so mwanza ni ngome ya chadema,
 
Mwanza ni bluu aisee - na Kigoma ni nyekundu (kama sio bluu ya NCCR)

Nilidhania Mwanza Blue ila sikuwa na uhakika sana niiweke wapi; Lakini nadhani upo sahihi; ngoja tuone wadau wengine wanasemaje, ila ningependa ufafanue kidogo kwanini unadhani mwanza ni blue, nafanya hivyo ili kuepuka wajinga wa CCM wakija humu waanze kutaja tu fulani kijani kwa hoja za ovyo; Kuhusu Kigoma, pia nakubaliana na wewe, lakini kati ya nyekundu na blue for NCCR, imelalia zaidi wapi kwa mtazamo wako?
 
mchambuzi umekosea mwanza.... mwanza ni blue kabisa... ni kati ya ngome kubwa ya chadema na kura nyingi zilitoka mwanza za chadema.. hapo panahitajika kurekebishwa..
 
jmushi1,

Nashukuru kwa kuona umuhimu wa zoezi hili; Takwimu za kila mkoa zipo lakini wachangiaji wengi wamekuwa wananajenga hoja kwamba takwimu za mwaka 2010 zilichakachuliwa kwahiyo hazifai kutumiwa kwa uchambuzi wowote wa kina; wewe una mtazamo gani juu ya hili? vinginevyo itarahisisha sana zoezi letu hili;

Nashukuru kuhusu corrections za sadakalawe, maisha yangu yote nimekuwa najua ni sandakalawe;
You're welcome mkuu.

Kuhusu takwimu ambazo wanachadema wanazikataa,je ni zile zenye kuonyesha idadi ya waliovipigia kura vyama?Kama zilichakachuliwa,je kuna ambazo huwa wanazitumia?

Mkuu nadhani unaweza tu kuziweka hapa halafu kama kuna watakaoweza kuongezea kutokana na wanavyoona,ama kama wanazo takwimu za tofauti basi wataziweka.Cha muhimu ni kuona ni wananchi kiasi gani waliowapigia kura chama flani kwenye hizo ngome zao.Hata kama zimechakachuliwa,bado tutakuwa na uwezo wa kuona ni wananchi wangapi kati ya waliojiandikisha kupiga kura na wakafanya hivyo wakati wa uchaguzi.
 
mkuu mi naomba unionjeshe kidogo data je unatumia vigezo vipi ktk mikoa ili kuipa ngome fulani ?

Nimeweka rangi hizo kwa hisia zangu tu hasa kwa kusoma mwenendo wa kisiasa lakini mgawanyiko huo sio rasmi, naomba mawazo yenu yenye nguzu za hoja tujue nani tumuweke wapi kisha kusonga mbele na mjadala;
 
Jambo la kwanza ungeomba wamiliki na wasafishaji wa JF kuweka site ya kura ambayo inaweza kupigwa kwa kila mwenye account JF once bila kurudia rudia, kwa mtindo huu wa sasa ni kupotea kura ambayo haina uhakika.
 
Nadhani ungeweka idadi ya waliopiga kura kwa kila chama kwenye hiyo mikoa,halafu maybe tuangalie na idadi ya wabunge na madiwani,then tunaweza kusema ipi ni ngome ya chama kipi.Hilo litasadia badala ya kukisia tu.Especially kama lengo ni kutabiri ushindi wa uchaguzi wa rais 2015 baina ya chadema na ccm.
 
Kuna saa naona kama vichwa venu haviko sawa.Hivi kweli Chadema mnawaza Kushika nchi hii.Hizo ni ndoto za alinacha
 
Kuna saa naona kama vichwa venu haviko sawa.Hivi kweli Chadema mnawaza Kushika nchi hii.Hizo ni ndoto za alinacha

ndio nyinyi niliokuwa nawazungumzia; cha ajabu Chadema kushika nchi ni kipi kama CCM wamechoka kuhudumia wananchi na badala yake wanahudumiana wenyewe? wananchi watawaondoa tu, siku hiyo inakuja;
 
Kuna saa naona kama vichwa venu haviko sawa.Hivi kweli Chadema mnawaza Kushika nchi hii.Hizo ni ndoto za alinacha
acha mipasho ya taarabu tunajaribu kufanya tafakari makini... nani kakuambia chadema hawawezi chukua nchi? kadri siku zinavyokwenda wajinga tz wanapungua... hivyo chadema kinapata wanachama wengi...therefore chadema have got the capability to win the 2015 elections man....
 
Jambo la kwanza ungeomba wamiliki na wasafishaji wa JF kuweka site ya kura ambayo inaweza kupigwa kwa kila mwenye account JF once bila kurudia rudia, kwa mtindo huu wa sasa ni kupotea kura ambayo haina uhakika.

wazo zuri; sasa tunafanyeje, nianzishe mjadala mpya as a poll?
 
Mwanangu Mchambuzi nakupongeza kwa kukuna kichwa na kuja na kitu cha kufundisha na kufikirisha. Utabiri au uchambuzi wako na utafiti vingekuwa na maana kama Bongo chini ya Chama Cha Machakachuaji kusingekuwa na sayansi ya uchakachuaji. Mimi natabiri kuwa mshindi wa uchaguzi katika uchaguzi ujao ataamriwa kwa ithibati ya watanzania. Kama wataibiwa na kukubali basi hakuna maana ya utabiri. Kama watasimama kidete, naamini kabisa wataamua nani mshindi kutokana na ukweli kuwa CCM walishasema hawako tayari kuachia ushindi kupitia sanduku la kura uwanyang'anye dola. These beasts are hellbent to see to it that they even burn the country. Theirs has always been to rig and manipulate. It is upon our beloved people to wake up and reclaim their lost fief so to speak. May God bless Tanzania. May God curse and destroy CCM.
 
Back
Top Bottom