Uchaguzi Rais 2015: Utabiri Wa Mshindi Baina ya CCM na CHADEMA

Uchaguzi Rais 2015: Utabiri Wa Mshindi Baina ya CCM na CHADEMA

mchambuzi umekosea mwanza.... mwanza ni blue kabisa... ni kati ya ngome kubwa ya chadema na kura nyingi zilitoka mwanza za chadema.. hapo panahitajika kurekebishwa..

sawa sawa, nilikuwa sina uhakika sana; vinginevyo kama nilivyomueleza jmushi1 na companero, wengi humu hawapendi sana mijadala na uchambuzi unaotumia takwimu za matokeo ya uchaguzi 2010 kwa madai kwamba takwimu zile sio sahihi kwani zilichakachuliwa; ndio maana nikaonelea tujikite tu zaidi kwenye database ya wapiga kura halafu kwa pamoja tukubaliane kwa hoja wapi ni blue, wapi kijani, wapi nyekundu, ili hoja ya uchakachuaji ififie kimashiko;
 
You're welcome mkuu.

Kuhusu takwimu ambazo wanachadema wanazikataa,je ni zile zenye kuonyesha idadi ya waliovipigia kura vyama?Kama zilichakachuliwa,je kuna ambazo huwa wanazitumia?

Mkuu nadhani unaweza tu kuziweka hapa halafu kama kuna watakaoweza kuongezea kutokana na wanavyoona,ama kama wanazo takwimu za tofauti basi wataziweka.Cha muhimu ni kuona ni wananchi kiasi gani waliowapigia kura chama flani kwenye hizo ngome zao.Hata kama zimechakachuliwa,bado tutakuwa na uwezo wa kuona ni wananchi wangapi kati ya waliojiandikisha kupiga kura na wakafanya hivyo wakati wa uchaguzi.
Sawa sawa, ngoja niziweke sawa then nitazipandisha;
 
Mkoa wa Geita hupo wapi?

Tunafanyeje hapo mkuu, maana kuna Mkoa wa Katavi na pia wa njombe; lakini kwa takwimu za sasa, geita ipo kwenye takwimu za Mwanza, kama ilivyokuwa katavi rukwa na njombe iringa;
 
kwa sasa mikoa mingine imeanzishwa mipya. hukuijumuisha. hata hivyo na hiyo kama dsm kusema ni ngomehakika ya CDM, kwa takwimu za mwaka gani? ukiangalia kati ya chadema ina jimbo la kawe & ubungo (2) . CCM inamajimbo (6) ya kinondoni, ilala,ukonga,segerea,kigamboni,temeke nk. hivyo kusema dsm ni ngome ya uhakika Chadema, kwa kutumia tafiti zipi ?
the same to maeneo mengine ya mikoa mingine. uchambuzi huu hauko realistic.
 
Tunafanyeje hapo mkuu, maana kuna Mkoa wa Katavi na pia wa njombe; lakini kwa takwimu za sasa, geita ipo kwenye takwimu za Mwanza, kama ilivyokuwa katavi rukwa na njombe iringa;

I thought the national website should have the data.
 
Mkuu Mchambuzi, asante sana kutufikirisha. Hizo data ulizotoa ni ithibitisho wa hoja yangu niliwahi kuitoa mara baada ya kuhudhuria uchaguzi mdogo Busanda na Biharamulo, nilisema CCM imekuwa ikishinda kwenye baadhi ya maeneo kutokana na povety level ya hali ya juu inayo pelekea watu hao kuwa ignorants hivyo kwao kuuza kura kwa T-shirt, kofia na shibe ya siku moja, its a big deal!.

Hivyo nikasema CCM ina capitalize on ignorance ya Watanzania kuendelea kuwaswaga masikini wale wa kututupwa kutokana na kutopea kwenye umasikini!.

Ukiangalia mikoa ambayo ni strong hold ya CCM, ni ile mikoa yenye dhiki na umasikini uliotopea na katika mikoa hivyo ignorance level iko juu with the exception of Bukoba!, huko nako kiukweli CCM haipendwi ki vile, ila "nshomile hawa" kuliko ku team up na kina "mangi", wameona bora wa opt kubaki na CCM!.

Kwa vile mtaji mkubwa wa ushindi wa CCM ni umasikini uliotopea na ignorance ya Watanzania, CCM itaendelea kushinda kwa sababu japo Chadema kupitia M4C "is doing the right thing" kwa kuwaamsha walio lala, but "it got to do things right" kwenye ku deal na object poverty!.

CCM imetishika sana kwa M4C kuwa sasa Chadema watawatibulia ule mtaji wao wa kutegemea ignorance kwani kufikia 2015 wale ma ignorants wengi wanaoipigia kura CCM kwa ignorance ya mazoea wengi watakuwa ni wamepungua na wachache watakao bakia watakuwa ni "spent force" tuu!.

Kwa kulitambua hilo, CCM imekuja na kitu inaitwa "safety net" ambapo serikali imetenga Sh. Bilioni 400 kuzigawa kama ruzuku kwa familia masikini!. Hivyo 2015 CCM sasa itashinda tena this time sio kwa kura za ignorance!, bali kwa kura za "appreciation" kama shukrani kwao kwa kugaiwa pesa hard cash for doing nothing!.

Hivyo 2015 mshindi ni CCM tena!. Be it ni yule "pace maker" mgombea wangu or "joka la mdimu", the bottom line mshindi ni CCM!.

Mara tuu baada ya uchaguzi 2010, nadhani mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza humu kusema point blank kuwa "Chadema Haijajipanga"!, nilitukanwa sana!, leo 2012 matokeo ya kutojipanga, ndio haya yameanza kuonekana! ikiwa ni bado miaka 3 tuu kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwingine ambapo mpaka sasa Chadema bado hawajajipanga!, unless katika kipindi hiki kilichobakia, Chadema sasa wafanye mambo yao kwa kukimbia wakati wenzao wakitembea, vinginevyo 2015 ni kilio kwa wengine na kicheko kwa wengineneo!.
Wasalaam.
Pasco.
 
Naungana na jmushi1. Kujua idadi ya wapiga kura tuu sidhani kama utakuwa umeitendea wema hii thread.

Ingekuwa vizuri pia kama tungejua angalao idadi ya watu ambao waliokuwa eligible kupiga kura. Ngumu kujua of course.

Baada ya hapo unaangalia ni wangapi ambao ni eligible walijiandikisha kupiga kura

Then, ni wangapi ambao walijiandikisha kupiga kura walipiga kura.

Halafu unaangalia kati ya waliopiga kura walikipigia kura chama gani.

Humo ndani ndiyo tunadadavua kwa nini watu hawajiandikishi kupiga kura. Pia hao wanaojiandikisha huwa wanafanya hivyo kwa dhumuni la kupiga kura?

Pia kwa nini wanaodaiwa kujiandikisha kupiga kura wengi wao hawapigi kura? This is the most pressing issue kwa kweli.

Kwa nini katika sehemu fulani watu wanakipigia kura chama fulani?

Ukishapata majibu ya maswali haya na mengine, unaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kufanya a through analysis ya polls, forecast, na hata betting. These will not only teach us something about a particular election, but also about democracy in general.

Through these we can know the outcome of elections weeks before they occur with about the accuracy with which we can know the weather a week before it occurs.

Kwa mfano, katika uchaguzi wa Marekani, polls suggest a Romney popular vote win. So does the best forecasting model. But the betting markets suggest a slight Obama victory on the popular vote and clearer victory in the Electoral College.

What's a betting person to do? Put some money on one horse and just enjoy the race.
 
kwa sasa mikoa mingine imeanzishwa mipya. hukuijumuisha. hata hivyo na hiyo kama dsm kusema ni ngomehakika ya CDM, kwa takwimu za mwaka gani? ukiangalia kati ya chadema ina jimbo la kawe & ubungo (2) . CCM inamajimbo (6) ya kinondoni, ilala,ukonga,segerea,kigamboni,temeke nk. hivyo kusema dsm ni ngome ya uhakika Chadema, kwa kutumia tafiti zipi ?
the same to maeneo mengine ya mikoa mingine. uchambuzi huu hauko realistic.

BADO HATA MAONI YAKO SIO REALISTIC, KWAN UKUMBUKI CCM ALVOCHAKACHUA MATOKEO? ANGALIA SEGEREA, KIGAMBONI, MAJIMBO YOTE AYA YANGEENDA CHADEMA, RIL KWA SASA CDM INA POWER SANA DAR, ILA NIMEKEREKA KWA KUINOTE KAGERA KM NGOME YA CCM NATMAI HAMETUDHALILISHA WAHAYA, TNACHUKIA SANA RUSHWA ZA CCM, KWA UFUPI KNA MAJIMBO KM NKENGE HATKUPIGA KWAKUWA CDM AIKUSMAMISHA MTU, PIA TATIZO MLETA MADA ANATMIA DATA ZA 2010, SHUKA ARDHINI TAFITI KWA SASA MAMBO NI TOFAUTI KABISA, TNATAKA MABADILIKO SANA, NA MBIO ZA URAIS ZTAKUWA TAMU KM MAGAMBA WATABUGI NA KUMSIMAMISHA FISADI EL AMBAE NI WAZI KAWAZID WASHINDAN WAKE KT CHAGUZ ZAO ZA MAJUZ, NATMAI MUNGU ATAKUWA ANAIELEKEZA TANZANIA KT MABADILIKo FR CCM TO CDM
 
Mkuu asante sana kwa takwimu nzuri. Ila usisahau kuwa Raisi atatokana na uwezo wake wa kutoa rushwa. Niamini nalo kuambia. Wananchi kwasasa wamegundua mkichaguliwa manawasahau na kupanda vx mpaka 5years zijazo wakati wao wanabaki na shida zao. Mwenye fedha na uwezo mkubwa wa kuhonga atakua raisi. Sisi watumia CP,Ipad na viwezesha vingine ni wachache sana, wanaoishi milimani kwa kuuza mahindi ndio wengi na ndio wenye kupiga kura.
Silaha PESA mkuu, KISU mzigo.
 
Ahsante sana Mkuu, that's a very critical projection. Mimi naamini Mikoa ya Mara, Kagera, Kigoma, Mtwara, Pwani na Zanzibar ni Sandakarawe. Kagera ni kati kwa kati CHADEMA na CCM,, Kigoma ni kati ya CHADEMA,CCM na NCCR,,,Mtwara na Zanzibar huwaambii kitu kuhusiana na CUF,,,,najua hapa target ni CHADEMA na CCM lakini kama ni Sandakarawe basi iwe ivyo.

Naendelea kuamini kuwa 2015 mambo mengi yatabadilika na hasa idadi ya wapiga kura itaongezeka sana kwani tutakuwa na vijana wengi wengi, mabadiliko haya yataathiri hata Ngome za uhakika za vyama hivi na hasa CCM
 
Nilidhania Mwanza Blue ila sikuwa na uhakika sana niiweke wapi; Lakini nadhani upo sahihi; ngoja tuone wadau wengine wanasemaje, ila ningependa ufafanue kidogo kwanini unadhani mwanza ni blue, nafanya hivyo ili kuepuka wajinga wa CCM wakija humu waanze kutaja tu fulani kijani kwa hoja za ovyo; Kuhusu Kigoma, pia nakubaliana na wewe, lakini kati ya nyekundu na blue for NCCR, imelalia zaidi wapi kwa mtazamo wako?

Mwanza ni buluu kutokana na yaliyomkumba Tony na Lau licha ya mamlaka yao ya kidola n.k.
Kigoma imelalia bluu zaidi kama tunajumuisha bluu ya NCCR na upinzani katika ujumla wake
 
Mwanza ni buluu kutokana na yaliyomkumba Tony na Lau licha ya mamlaka yao ya kidola n.k.
Kigoma imelalia bluu zaidi kama tunajumuisha bluu ya NCCR na upinzani katika ujumla wake
Vigezo gani mnatumia kupanga mikoa? Hili ndio jambo la kwanza. Maana naona mnachangia tu bila kujua vigezo. Inawezekanaje Kigoma ikawa kijani na Kilimanjaro blue? Kigoma ilitoa Kura Kwa chadema kwenye Urais 45% Mara mbili ya national avarage. Arusha? Kilimanjaro? Dar ES Salaam?
Kigoma ina majimbo 8, majimbo 5 yapo upinzani na 3 CCM. Hawa NCCR wote isipokuwa mmoja Ni CDM rebels tu na watu wa Kigoma walichagua watu hao Kwa hasira na sio NCCR iliyochaguliwa na ndio maana CDM ilipata Kura nyingi za Urais na madiwani wengi sana mkoa Mzima.

Wekeni vigezo vya kisayansi na sio hisia tu. companero wewe mwanasayansi, saidia kuweka vigezo ili mjadala uwe na maana.

Kigoma has never been CCM toka mfumo wa vyama vingi uanze and it will never been CCM. Unawezaje kuweka Iringa blue na Kigoma au Kagera kijani?
 
Mkuu nakubaliana na wewe'unafikiri nini kifanyike ili tuweze kuharibu huo mpango mpya wa ccm?

.....

Mkuu director1, kitu cha kufanyika ni kidogo tuu, nacho ni "Chadema Ijipange" "kimipango mkakati" (strategies) na kuanza "to do things right" on top of doing "the right thing"!.
P.
 
Vigezo gani mnatumia kupanga mikoa? Hili ndio jambo la kwanza. Maana naona mnachangia tu bila kujua vigezo. Inawezekanaje Kigoma ikawa kijani na Kilimanjaro blue? Kigoma ilitoa Kura Kwa chadema kwenye Urais 45% Mara mbili ya national avarage. Arusha? Kilimanjaro? Dar ES Salaam?

Kigoma ina majimbo 8, majimbo 5 yapo upinzani na 3 CCM. Hawa NCCR wote isipokuwa mmoja Ni CDM rebels tu na watu wa Kigoma walichagua watu hao Kwa hasira na sio NCCR iliyochaguliwa na ndio maana CDM ilipata Kura nyingi za Urais na madiwani wengi sana mkoa Mzima.

Wekeni vigezo vya kisayansi na sio hisia tu. companero wewe mwanasayansi, saidia kuweka vigezo ili mjadala uwe na maana.

Kigoma has never been CCM toka mfumo wa vyama vingi uanze and it will never been CCM. Unawezaje kuweka Iringa blue na Kigoma au Kagera kijani?.......

Muanzishaji wa mada kasema huu ni mwanzo, anajipanga kuandaa hivyo vigezo vya kisayansi kwa msaada wa huu mjadala wa awali - ila hisia nazo ni vigezo pia kwenye siasa ndio maana sasa kuna kukubaliana kuhusu ubluu wa Kigoma (rejea jibu la Mchambuzi kuhusu kukubaliana na hoja ya Companero kwamba Kigoma inapaswa kuwa bluu).
 
Back
Top Bottom