Uchaguzi Rais 2015: Utabiri Wa Mshindi Baina ya CCM na CHADEMA

Uchaguzi Rais 2015: Utabiri Wa Mshindi Baina ya CCM na CHADEMA

Very Constructive Study!! Hata hivyo, ili tuweze kupata minimal erros result ni bora tukiangalia jambo moja la msingi ambalo watu tunashindwa kuliona kwa mapana yake. Jambo ninalopenda kuweka sawa ni kuhusu tafsiri ya neno "ngome ya CHADEMA" na "Ngome ya CCM." Haya yote yana maana sawa lakini uhalisia wake kwa hivi sasa ni tofauti kidogo.

Tunapozungumzia mkoa fulani ni Ngome ya CCM, UHALISIA wake kwamba mkoa huo ni ngome ya CCM kweli kweli kiasi kwamba kwenye mkoa husika CCM inatarajiwa kushinda kwa ushindi wa kishindo unaoweza kufikia hadi 70% na wakati mwingine hata 80%! Kwa kawaida, mikoa ya aina hiyo inakuwa haitoi nafasi yoyote kwa CHADEMA!

Kinyume chake, tunavyozungumzia mkoa fulani ni Ngome ya CHADEMA, UHALISIA wake ni kwamba hapo CHADEMA inapewa nafasi kubwa ya kushinda kuliko CCM ingawaje CCM haiwezi kupuuzwa moja kwa moja! Hivyo basi, inapotokea CHADEMA imeshinda kwenye mkoa husika bado ushindi wake hauwezi kuwa wa kishindo kama vile CCM inavyoshinda kwenye ngome zake. Aidha, hata kama CHADEMA inakuwa inapewa nafasi kubwa ya kushinda, bado CCM nao wanakuwa na nafasi ya kushinda hata kama haiwezi kuwa kubwa kama ile ya CHADEMA.

Asante kwa mawazo yako nasdaz; nadhani ni muhimu sana nikaweka ufafanuzi huo juu ya maana ya Ngome; nitafanya marekebisho haya muhimu muda si mrefu; hivi sasa kuna takwimu naziweka sawa ili nizipandishe; vinginevyo based on your description au definition ya NGOME, mifano miwili nadhani ni mizuri, nayo ni Tanga being GREEN all the way, na Arusha being BLUE all the way....
 
Naingia kichwa kichwa

Vigezo

1. Mahali chama kina strong showing nawapa 70%, kinachofuata 30%, Wengine 10%

2. Mahali chama kina ushindani mkubwa nawapa 50%; 30% 20%

3. Mahali vyama vina ushindani karibu sawa na kuna wa kutopiga kura nawapa 40%, 30%, 30%

4. Mahali kuna ushindani sawa kwa vyama viwili 40%, 40%, 20%

Kwa vigezo hivyo naweka utabiri wangu kama hapo chini unaweza weka wa kwako kwa vigezo na viwango vyako.

2015 ikiwa ni sahihi ki hivi nigongeeni Like kwa sababu kitufe cha Like kwenye post zangu kimeondolewa
[TABLE="width: 396"]
[TR]
[TD="class: xl65, width: 43, bgcolor: transparent, align: right"][/TD]
[TD="class: xl65, width: 98, bgcolor: transparent, align: center"]MKOA[/TD]
[TD="class: xl66, width: 98, bgcolor: transparent, align: center"]IDADI YA WAPIGA KURA[/TD]
[TD="class: xl65, width: 103, bgcolor: transparent, align: center"]CDM[/TD]
[TD="class: xl65, width: 93, bgcolor: transparent, align: center"]CCM[/TD]
[TD="class: xl65, width: 92, bgcolor: transparent, align: center"]Wengine[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent, align: right"]1[/TD]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent"]ARUSHA[/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 723,874.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 506,711.80 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 144,774.80 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 72,387.40 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent, align: right"]2[/TD]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent"]DAR ES SALAAM[/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 1,912,662.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 956,331.00 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 765,064.80 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 191,266.20 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]3[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]DODOMA[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 849,561.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 339,824.40 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 424,780.50 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 84,956.10 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent, align: right"]4[/TD]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent"]IRINGA[/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 758,262.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 379,131.00 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 303,304.80 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 75,826.20 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]5[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]KAGERA[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 1,048,294.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 419,317.60 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 524,147.00 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 104,829.40 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]6[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]KIGOMA[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 666,114.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 333,057.00 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 266,445.60 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 66,611.40 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent, align: right"]7[/TD]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent"]KILIMANJARO[/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 739,529.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 517,670.30 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 147,905.80 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 73,952.90 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]8[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]LINDI[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 450,620.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 180,248.00 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 225,310.00 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 45,062.00 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent, align: right"]9[/TD]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent"]MANYARA[/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 533,894.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 320,336.40 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 160,168.20 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 53,389.40 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent, align: right"]10[/TD]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent"]MARA[/TD]
[TD="class: xl73, bgcolor: transparent, align: right"] 752,906.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 376,453.00 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 301,162.40 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 75,290.60 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent, align: right"]11[/TD]
[TD="class: xl67, bgcolor: transparent"]MBEYA[/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 1,056,126.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 633,675.60 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 316,837.80 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 105,612.60 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent, align: right"]12[/TD]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent"]MOROGORO[/TD]
[TD="class: xl73, bgcolor: transparent, align: right"] 988,113.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 494,056.50 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 395,245.20 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 98,811.30 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]13[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]MTWARA[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 658,220.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 263,288.00 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 329,110.00 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 65,822.00 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent, align: right"]14[/TD]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent"]MWANZA[/TD]
[TD="class: xl73, bgcolor: transparent, align: right"] 1,586,919.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 952,151.40 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 476,075.70 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 158,691.90 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]15[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]PWANI[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 518,841.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 155,652.30 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 259,420.50 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 103,768.20 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]16[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]RUKWA[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 489,289.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 195,715.60 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 244,644.50 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 48,928.90 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent, align: right"]17[/TD]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent"]RUVUMA[/TD]
[TD="class: xl73, bgcolor: transparent, align: right"] 607,920.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 303,960.00 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 182,376.00 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 121,584.00 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent, align: right"]18[/TD]
[TD="class: xl72, bgcolor: transparent"]SHINYANGA[/TD]
[TD="class: xl73, bgcolor: transparent, align: right"] 1,380,953.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 690,476.50 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 552,381.20 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 138,095.30 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]19[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]SINGIDA[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 545,074.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 218,029.60 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 272,537.00 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 54,507.40 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]20[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]TABORA[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 840,014.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 336,005.60 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 420,007.00 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 84,001.40 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]21[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]TANGA[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 891,942.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 356,776.80 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 445,971.00 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 89,194.20 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent, align: right"]22[/TD]
[TD="class: xl70, bgcolor: transparent"]* ZANZIBAR[/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 15,540.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 1,554.00 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 9,324.00 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 4,662.00 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: xl74, bgcolor: transparent, align: right"][/TD]
[TD="class: xl74, bgcolor: transparent"]JUMLA[/TD]
[TD="class: xl69, bgcolor: transparent, align: right"] 18,014,667.00 [/TD]
[TD="class: xl68, bgcolor: transparent, align: right"] 8,930,422.40 [/TD]
[TD="class: xl71, bgcolor: transparent, align: right"] 7,166,993.80 [/TD]
[TD="class: xl75, bgcolor: transparent, align: right"] 1,917,250.80 [/TD]
[/TR]
[/TABLE]

naona Sheikh Yahya amepata warithi. kwa kuangalia tu matokeo ya udiwani ya juzi unajua tu nani anashinda. chadema wameongeza kata , CCM imeendelea kushinda kata zake na kupoteza 2 kama sikosei. ni dhahiri kuwa CCM ina nguvu. hapo kwenye takwimu zako, kuipa chadema ushindi ni kama kujifariji tu, na kuwapa moyo wachangiaji wanaoipenda Chadema. lakini kiuhalisia Ushindi wa Chadema 2015 utategemea na "upepo" wa usalama wa chaguzi zake za ndani 2014. na pia ni jinsi gani imejikita kutengeneza wanachama. bila kutegemea "undecided voters" ambao hutegemea kampeni. na mikutano. tuwe realistic
 
Mimibaba bado hayo ni matokeo ya hisia tu hayareflect hali halisi ndiyo maana tunapendekeza tutumie takwimu za uchaguzi wa 2010 kama kigezo hapo tutakua tumeanzia mahali pazuri.
 
naona Sheikh Yahya amepata warithi. kwa kuangalia tu matokeo ya udiwani ya juzi unajua tu nani anashinda. chadema wameongeza kata , CCM imeendelea kushinda kata zake na kupoteza 2 kama sikosei. ni dhahiri kuwa CCM ina nguvu. hapo kwenye takwimu zako, kuipa chadema ushindi ni kama kujifariji tu, na kuwapa moyo wachangiaji wanaoipenda Chadema. lakini kiuhalisia Ushindi wa Chadema 2015 utategemea na "upepo" wa usalama wa chaguzi zake za ndani 2014. na pia ni jinsi gani imejikita kutengeneza wanachama. bila kutegemea "undecided voters" ambao hutegemea kampeni. na mikutano. tuwe realistic

Shehe Yahaya alikuwa anatumia vitabu na majini mimi natumia takwimu za Mchambuzi na upepo unavyovuma. Nilitegemea ukosoe kuhusu chanzo cha takwimu za Mchambuzi maana kina mapungufu.

La kwanza hakutoa asilimia ya wasiopiga kura kulingana na uchaguzi uliopita na kwa nini hawakupiga kura.

La pili kuna wapiga kura wapya hata kabla ya 2015 ambao hatma ya kuingizwa kwenye daftari haiojulikani.

Tatu kiwango cha kujinasi kwa rushwa kwa CCM ni kwa kwenda mbele ambacho ni chanzo kikubwa cha mgawanyiko wa wapiga kura wake mahafidhina.

Nne CCM ijitakari na ichukue hatua za kujirekebisha kwa kubadili sera yake ya KUTAWALA MILELE na ijielekeze kuwasikiliza wapiga kura.

Tano jitihada za CCM kuondoa umasikini na ujinga wa elimu ya uraia zianze

Sita M4C ikijitathmini kujitafakari na kuchukua hatua, elimu ya uraia itaongezeka, wapiga kura watakuwa na sababu za msingi za kuchagua chama kwa ulinganisho makini. CDM wajiwekee mtandao wa maana vijijini kama wanavyofanya.

Saba vyama viache kutegemea kudra ya Mungu, rushwa, ujinga na umaskini kupata kura bali vifanye kisayansi na viaonekane kwa matendo vina dhamira nzuri

Nane tuombe Mungu majanga yasiwepo pamoja hasa kwa wanasiasa wetu kuto kuathirika na majanga hayo.

Tisa pamoja na ugumu wa maisha sisi wananchi tusiotegemea ajira bali hali ya hewa tunaweza kupata chakula na kuitazama nchi yetu kwa jicho la huruma.

Mwisho mchakato wa Katiba uende salama kwa kuvunja muungano au kuwa na aina tofauti ya muungano.

Kwa takwimu za kuanzia, inatosha kupiga ramli pamoja na kwamba utabiri wangu ni kuwa huo ushindi wa CDM unaweza kuongezeka zaidi kama hata wewe utafanya uchaguzi kwa vigezo vyenye mantiki kwa kuepuka mazoea.
 
Mimibaba bado hayo ni matokeo ya hisia tu hayareflect hali halisi ndiyo maana tunapendekeza tutumie takwimu za uchaguzi wa 2010 kama kigezo hapo tutakua tumeanzia mahali pazuri.

"ningependa kuwasilisha takwimu za idadi ya wapiga kura kwa kila mkoa Tanzania kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi (NEC); Ni dhahiri takwimu hizi zitaendelea kubadilika jinsi tunavyo karibia mwaka 2015, lakini halitakuwa tatizo kwani tutaendelea kufanya marekebisho accordingly"

Namnukuu Mchambuzi aliyeleta takwimu tuzijadili na mimi naona zinafaa kujadiliwa kama "initial sample". Unapokuwa na takwimu hakuna suala la hisia takwimu hizi kulingana na Mchambuzi ni takwimu za uchaguzi wa 2010; lakini pia angalia post yangu #64 .

Nimeona tukipata madaraka na uhuru toka kwa wakoloni, nimeona nchi kiuchumi tuliyoachiwa na wakoloni, nimekuwa mtumishi wa serikali kwa awmu zote nne. Experience hii ya utawala wa chama tawala ni chungu SIITAKI mimi na wala siitaki kwa wajukuu wangu kwa kukosekana mwelekeo thabiti. Ila kwa kulinganisha takwimu na hali ya mambo nakiri viwango vya vigezo vyangu vinaweza kuwa na kosoro lakini ni sahihi kwa asilimia 60 ingawaje ningependa ningekuwa na usahihi unaozidi asilimia 70 ambao si rahisi kuupata.
 
Bongolander,

Ni kweli suala la poll limekaa complicated kidogo, halitatupa kitu tunachotafuta, ndio maana mimi naona ni vizuri sana tukianza na raw data ambazo ndio nimeziweka, then kama alivyoshauri jmushi1, niweke matokeo ya 2010 kwa kila mkoa n akila chama, ingawa katika hili kuna baadhi ya watu wanajenga hoja kwamba takwimu za 2010 sio legit kwa sababu ya uchakachuaji uliotokea (allegedly); Hiyo ramani yako imekaa vizuri, source yake nini? nadhani itasaidia sana kuweka things into perspective katika mjadala wetu; naweka takwimu fulani sawa halafu nitarudi;

Mkuu hiyo ramani nimechorachora mwenyewe si official nilikuwa najaribu tu kuweka input kutokana na kumbukumnbu za uchaguzi uliopita. Nakubaliana na Jmushi1 kuhusu takwimu za 2010 si za kweli. Ukipata zile raw zitakuwa ni za kweli, lakini zilizotangazwa na NEC zilichakachuliwa sana. Redet walifanya polls ambazo zilireflect matokea yale yaliyochakachuliwa, ukipata zile itakuwa msingi mzuri wa kujadili na kuangalia hali ya 2015 inaweza kuwa vipi.
 
Mkuu hiyo ramani nimechorachora mwenyewe si official nilikuwa najaribu tu kuweka input kutokana na kumbukumnbu za uchaguzi uliopita. Nakubaliana na Jmushi1 kuhusu takwimu za 2010 si za kweli. Ukipata zile raw zitakuwa ni za kweli, lakini zilizotangazwa na NEC zilichakachuliwa sana. Redet walifanya polls ambazo zilireflect matokea yale yaliyochakachuliwa, ukipata zile itakuwa msingi mzuri wa kujadili na kuangalia hali ya 2015 inaweza kuwa vipi.

Siwezi kupata data ambazo sio rasmi kwa mujibu wa NEC; alichosema jmushi1 ni kwamba tutumie takwimu zilizopo NEC, hata kama zilichakachuliwa, then humo humo tuajua tusonge vipi mbele, je unakubaliana na hoja hiyo? Vinginevyo inabidi tutengeneze picha yetu wenyewe kama nilivyoweka kwenye bandiko namba moja kuhusu wapi ni ngome ya nani, kama ulivyofanya na ramani yako ambayo its very useful;
 
Kigoma, sio ngome ya CCM kabisa, ninaifahamu KG ninatokea kule.

Kwa maneno ya haraka Kigoma ni ngome ya upinzani, kwa hiyo ni bora uiwekee alama nyekundu kuliko hiyo kijani. Naomba ubadilishe haraka maana hiyo kijani uliyoweka kwenye kigoma inanikera sana mimi.
 
Mchambuzi,

Hizo Green,Blue,Red zitategemea na CCM watamsimamisha nani kugombea nafasi. Zinaweza kubadilika kidogo.
 
Kigoma, sio ngome ya CCM kabisa, ninaifahamu KG ninatokea kule.

Kwa maneno ya haraka Kigoma ni ngome ya upinzani, kwa hiyo ni bora uiwekee alama nyekundu kuliko hiyo kijani. Naomba ubadilishe haraka maana hiyo kijani uliyoweka kwenye kigoma inanikera sana mimi.

KIgoma ni ngome ya wapinzani kwenye ubunge sio urais.
 
Akiteuliwa Lowassa hizo Blue za Kilimanjaro na Arusha zinakuwa Green while other Greens remain Green. :becky: (I'm just guessing)
 
Mkuu Mchambuzi,kwanza nadhani thread hii itatumika na vyama vyote kuwasaidia waelewe ni wapi panahitajika kupafanyia kazi kuelekea uchaguzi mkuu 2015.

However nilikuwa na ombi moja;je kuna uwezekano wa kutuwekea rekodi za kura zilizopatikana kwa kila chama kwenye hiyo mikoa ambayo inaelekea kuwa ni ngome zao?


Mwisho,nadhani hapo kwenye "toss up",ni "sadakalawe" na si "sandakalawe"



Record za nyuma za kura zisitumike kutabiri mshindi ni nani 2015. Kwa sababu ninategema mazingira tofauti ya uchaguzi tofauti na kipindi kilichopita

1. Katiba tofauti
2. Tume ya uchaguzi tofauti
3. Tawala za mikoa kutojihusisha na uchaguzi moja kwa moja (eg. Mkurugenz, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa N.k)
4. Daftari/Orodha ya wapiga kura; kuandikwa wapya na kuhakiki wa zamani
5. n.k



Unapofanya mchanganuo kama huu kwa maana ya kutabiri kitu, lazima ujiwekee mipaka na assumptions

Kwa maoni yangu mimi, kama kila kitu hapo juu kitabaki kama ilivyo sasa (status quo) hata hili zowezi itakuwa ni kujisumbua tu, kwa maana kwamba CCM watashinda kiti cha uraisi.

Ila kama kitabadilika angalau kimoja wapo hapo juu, hasa katiba ambayo italazimisha mabadiliko ya vingine, kutakuwa na mazingira tofauti sana ya kiuchaguzi ambayo hayahusiana na takwimu za 2010 na kurudi nyuma.

Believe you me, Tatizo letu kubwa ni mfumo wa kiuchaguzi, vinginevyo tutakuwa tunatabiri kitu ambacho tunajua jibu.

Wana wa Shinyanga hawatasahau pale walipojua mbunge wa Chadema ameshashinda, wakawa wanashangilia mtaani, wakasikia mambo yamebadilika ghafla, CCM wameshinda kwa kura 1.
 
KIgoma ni ngome ya wapinzani kwenye ubunge sio urais.

Hapana mkuu, najua unaangalia kura zilizopigwa miaka ya nyuma, hasa 2010; Kwa upande wa kigoma kuna tatizo kubwa sana lilifanyika juu ya kumnadi mgombea wa upinzani kwa nafasi ya urais; kwa mfano mtu ambaye Chadema walimtegemea sana amnadi mgombea wao wa uraisi kule kigoma ni ZZK, lakini huyu jamaa alikuwa busy kujinadi yeye mwenyewe kwa nafasi ya ubunge wake na ni mara chache sana aliweka msisitizo kwenye kumnadi Dr. Slaa. Fuatilia hotuba zake nyingi wakati wa kampeni utagundua hilo, alifikia hatua ya kujinadi yeye kwa nafasi ya uraisi 2015.

Swala la watu kumuunga mkono mbunge wa chama flani na si mgombea Uraisi ni kweli inatokea, lakini hii huwa ni katika level ya Jimbo kwa sababu flani flani, na si kwa Mkoa mzima wenye majimbo zaidi ya matano.
 
Record za nyuma za kura zisitumike kutabiri mshindi ni nani 2015. Kwa sababu ninategema mazingira tofauti ya uchaguzi tofauti na kipindi kilichopita

1. Katiba tofauti
2. Tume ya uchaguzi tofauti
3. Tawala za mikoa kutojihusisha na uchaguzi moja kwa moja (eg. Mkurugenz, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa N.k)
4. Daftari/Orodha ya wapiga kura; kuandikwa wapya na kuhakiki wa zamani
5. n.k



Unapofanya mchanganuo kama huu kwa maana ya kutabiri kitu, lazima ujiwekee mipaka na assumptions

Kwa maoni yangu mimi, kama kila kitu hapo juu kitabaki kama ilivyo sasa (status quo) hata hili zowezi itakuwa ni kujisumbua tu, kwa maana kwamba CCM watashinda kiti cha uraisi.


Ila kama kitabadilika angalau kimoja wapo hapo juu, hasa katiba ambayo italazimisha mabadiliko ya vingine, kutakuwa na mazingira tofauti sana ya kiuchaguzi ambayo hayahusiana na takwimu za 2010 na kurudi nyuma.

Believe you me, Tatizo letu kubwa ni mfumo wa kiuchaguzi, vinginevyo tutakuwa tunatabiri kitu ambacho tunajua jibu.

Wana wa Shinyanga hawatasahau pale walipojua mbunge wa Chadema ameshashinda, wakawa wanashangilia mtaani, wakasikia mambo yamebadilika ghafla, CCM wameshinda kwa kura 1.

Mkuu MC nakubaliana sana na wewe, kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki kikweli, uwezekano wa CCM kushinda ni mdogo sana. Unless wafanye kampeni kubwa kupindukia, kitu ambacho kimsingi hakiwezekani. Hayo unayosema, kwa maoni yangu, sioni kama kweli CCM itakubali kuyabadilisha. Hata kama ni mimi nigekuwa madarakani nimeshika polisi, jeshi, mahakama, tume ya Uchaguzi, above all usalama wa taifa, nisingekubali kuachia.

Ukumbuke pia kuwa bado CCM wanadhibiti idara zinazoamua na zinazotangaza mshindi. Kwa maana hiyo hata kama opposition wakishinda (kwa mazingira kama ya sasa) hali itakuwa kama 2010. Kwa hiyo kilichopo ni kuwa CUF na CDM ambao ndio victims wakubwa wa uchakachuaji wachukue hatua haraka sana katika miezi hii 36. Kwenye uchaguzi wa 2010 wananchi walionesha kuitikia sana kutaka mabadiliko, wapiga kura played their part kuhakikisha kuwa hawaibiwi tena.

Kama 2015 Chadema na CUF hawatafanya juhudi za kuleta foreign observer wengi na kuwaweka katika kila kituo cha kupigia kura, mchezo utakuwa ni ule ule wa kuchakachua kwenye kuhesabu kura na kutangaza mshindi. Kama kukiwa na foreign obsever katika kila kituo, na foreign observer kila mkoa hadi ngazi ya taifa, uchaguzi unaweza kuwa fair. Hii ndio naona option pekee kama mazingira yakiwa kama ya 2010.

Tukiendelea kuleta observers na wanakwenda Dar, Arusha, Dodoma na Zanzibar na kupiga picha mbili tatu, tutakuwa tunaendelea kujidanganya, ni kama tutakuwa tunaita wageni kuja kuhalalisha stolen elections. Kwa hiyo mkuu MC naona muhimu hapa ni kuangalia uwanja wenyewe wa 2015.
 
  • Thanks
Reactions: MC
mchambuzi umekosea mwanza.... mwanza ni blue kabisa... ni kati ya ngome kubwa ya chadema na kura nyingi zilitoka mwanza za chadema.. hapo panahitajika kurekebishwa..

Mkuu mwanza ni blue kutoka mjini mpaka vijijini
 
Wakuu,

Nimeupenda mjadala huu. siasa za Tanzania zinabadirika sana. kuna rafiki yangu Diwani chama fulani aliniambia hivi'sism niwajanja.

hakasems mtaji wao ni pesa na propaganda chafu. nimi nimeliona hilo. Hila ninachojua M4C imekuwa mwiba kwao kwasababu inagusa watu wao-ignorant citizens. Ushauri wangu, kama nilivyoshauri pia kwenye threads zenye mlengo kama huu, nguvu yam4c izidishwe mara dufu kuelekea red na green no matter what kind of resistance you gone face.
 
Mchambuzi,

Hongera sana kwa kuleta hii mada. Mimi nadhani kama vyama vya upinzani wataitumia hii mada vizuri itawasaidia sana katika uchaguzi comes 2015. Nashindwa kuelewa kwa nini miji mikubwa kama Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza idadi ya waliojiandikisha kupiga kura na idadi ya watu haviendani. Ni muhimu kwa vyama vya upinzani kuanza kuhamasisha watu wajiandikishe kupiga kura na kuanza kuliangalia hili daftari kwa kutumia magnifed lenses. Kitu kingine, CDM na CUF waanze kufikiria ni kwa jinsi gani wanaweza kuweka tofauti zao pembeni, na kuangalia jinsi ya kushirikiana; kwani, ukiweka CUF katika hiyo equation mikoa mingi ya pwani inakuwa sandakalawe....
 
Nadhani ungeweka idadi ya waliopiga kura kwa kila chama kwenye hiyo mikoa,halafu maybe tuangalie na idadi ya wabunge na madiwani,then tunaweza kusema ipi ni ngome ya chama kipi.Hilo litasadia badala ya kukisia tu.Especially kama lengo ni kutabiri ushindi wa uchaguzi wa rais 2015 baina ya chadema na ccm.

Mkuu, heshima mbele na Mchambuzi kwa mada hii. Kumekuwa na hoja kuwa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi hayatafaa kwa uchambuzi maana yalikuwa na uchakachuzi. File nililoattach lina matokeo ambayo yanasadikiwa kuwa sahihi kama ambavyo lilivyokuwa likisambazwa muda kidogo baada ya uchaguzi ikiwa ni sehemu ya tathmini ya matokeo ya uchaguzi ule. Siwezi kusema kwa uhakika kuwa ndo matokeo ambayo hayajachakachuliwa maana sijacompile mie, lakini kwa madai ya wengi haya ndo yalikuwa matokeo sahihi. Kwa dhumuni la utabiri huu, matokeo haya yanaweza kutupa mwanga zaidi katika kujua ngome za wagombea watarajiwa.
 

Attachments

Lifuatalo ni zoezi la utabiri juu ya mshindi Urais uchaguzi Mkuu 2015 baina ya CCM na Chadema; Lakini kabla hatujaenda kwenye hatua nyingine yoyote, ningependa kuwasilisha takwimu za idadi ya wapiga kura kwa kila mkoa Tanzania kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi (NEC); Ni dhahiri takwimu hizi zitaendelea kubadilika jinsi tunavyo karibia mwaka 2015, lakini...

Kwanza hapo kwa Dar es salaam umekosea sana aisee, hakuna ngome yenye nguvu kwa ccm km hii, Dar es salaam ina wenyewe mkuu, wengine wote wakuja tu.
 
Back
Top Bottom