Wakuu,
Kutokana na hoja za wachangiaji mbalimbali kama vile kutoka kwa bongolander, EMT, Zitto, Mimibaba, kwa kutaja wachache tu, kwamba tunahitaji a more realistic approach nimejaribu kutulia and dig out my brian ili kubaini njia nzuri ya kutufikisha tunapokusudia kufika; Nimefanikiwa angalau kukwangua ‘the surface' kwani hatua ya kuchimba shimo bado ipo mbali kidogo; Katika juhudi zangu mbalimbali, nikabaini kwamba matumizi ya takwimu za matokeo ya uchaguzi mkuu 2010 ni jambo lisilo epukika; However, sio takwimu za Urais kwani hizi zina mashaka ya uchakachuaji, bali takwimu za matokeo ya kura kwa wabunge, kwani licha ya mapungufu ya hapa na pale yaliyojitokeza maeneo kama Segera n.k, hizi kwa kiasi kikubwa takwimu za ubunge ni more reliable, na kama kuna tatizo la uchakachuaji, basi zitabadilika kwa Margin ndogo sana; Kabla sijaendelea, ni muhimu nikasema kwamba nimekuja na assumption moja muhimu that that should hold:
Ili kufanikiwa ushindi 2015, ni muhimu kwa Mgombea Urais wa Chadema akabebwa na Wabunge majimboni kwao kuliko kutumia mfumo wa sasa wa CCM ambao ulikuwa more effective chini ya Chama kimja na ambao kwa maajabu makubwa, bado unaendelea leo hii na kuigwa hata na Chadema na vyama vingine, yani - Mgombea Urais ndio mbeba Wabunge Majimboni; Iwapo this assumption holds, basi uchaguzi wa 2015, We should not expect a Discrepancy between kura za mbunge na Rais kama ilivyojitoeza 2010; Ni muhimu yaliyotokea kwa Zitto na Mbowe yasijirudie tena 2015 kwani bila ya hivyo, Chadema itakuwa na wakati mgumu wa kushinda kiti cha Urais;
Uchambuzi wangu wa takwimu za kura za wabunge 2010 umenipa picha ambayo sikuitarajia na ni tishio kwa Chadema tofauti na wengi wanavyodhania; Picha hii imenifanya nibadilishe kabisa mtazamo wangu juu ywa mikoa gani ni GREEN, BLUE na RED; Hoja za baadhi ya wachangiaji humu kwamba mkoa kama vile Dar-es-salaam sio BLUE bali GREEN, kumbe ni hoja yenye mashiko makubwa sana; Mbali ya Dar-e-salaam, Mkoa mwingine ambao wengi wetu hatukudhania ungekuwa GREEN au RED yani ARUSHA, pamoja na takwimu za marudio ya Uchaguzi wa Arumeru Mashariki mwaka huu (2012), bado Arusha sio BLUE bali ni GREEN; Sana sana ni RED, lakini BLUE? HAPANA; Nitajaribu kufafanua nimefikiaje findings hii kubwa na muhimu sana kwetu; Nitatumia mkoa wa Arusha kwa kuanzia na kuomba ridhaa yenu kama mnakubaliana na methodolofy niliyotumia ili kama tunafikia consensus, basi niendelee kwa mikoa iliyobakia ili tuweze kubaini wapi ni GREEN, wapi ni BLUE, wapi ni Sandakalawe;
Bongolander na wengine wachache walijadili hoja muhimu sana kwamba kura za mijini zio kigezo tosha kwamba Mkoa fulani ni ngome ya Chadema au CCM; Tutazame takwimu zifuatazo:
Kwa mujibu wa takwimu za Sensa za mwaka 2002, Arusha ina jumla ya watu 1,288,088; Hizi ni takwimu ya zamani, lakini kwa vile projections za population growth rate Tanzania zimeendelea kuwa takribani 3% kwa mwaka, ifikapo mwaka 2015, Arusha itakuwa na jumla ya wakazi karibia milioni 1.8; Nimepata takwimu hii kwa kuchukua 3% kwa mwaka (out of the 1.28 million population) mara miaka 13 i.e, na iwapo tutajumlishia ongezeko hili kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2015, tutapata takribani watu milioni 1.8 kama wakazi wa Arusha ifikapo 2015; Tofauti na matarajio ya wengi, kumbe Arusha ni mkoa muhimu sana kwani ukitazama jedwali kwenye bandiko namba moja la uzi huu, utaona kwamba Arusha haipo hata katika kumi bora in terms of idadi kubwa ya watu waliojiandikisha kupiga kura 2010, huku Arusha hiyo hiyo ikiwa sio tu kwamba ipo kwenye kumi bora, bali tano bora in terms of idadi ya watu miongoni mwa mikoa yote ya Tanzania;
This is a very important finding for vyama vyote vya siasa kwani takwimu za NEC zinaweza kuchuza, na kufanya vyama vya siasa viweke priority kwenye mikoa mingine na kupoteza ushindi; Finding hii emphasizes umuhimu wa chama kama Chadema kupitia m4c kuhakikisha kinajikita zaidi katika kuandikisha wapiga kura wapya badala ya kupoteza muda kugeuza wanachama wa CCM wahamie Chadema; Ukweli utaendelea kubakia kwamba – jumla ya wanachama wa CCM na Chadema haitafikia hata nusu ya jumla ya wapiga kura wa nchi nzima ifikapo 2015; Vinginevyo, mkoa kama Arusha utakuwa ni moja na mikoa muhimu sana kutupatia Rais mwaka 2015, hasa iwapo tuta acha kuchukulia takwimu za NEC juu ya idadi ya waliojiandikisha kupiga kura kama ndio takwimu mama; Ni muhimu kwa vyama vya upinzani kuhimiza wananchi wajiandikishe kupiga kura, na vyama hivi viweke malengo/targets kwa mizi sita/mwaka juu ya idadi ya wapiga kura wapya n.k, huku wakihakikisha wanalinda kura za wale wote wanaojiandikisha kuelekea 2015;
Takwimu nyingine muhimu kwa mkoa wa Arusha ni ile ya eligible voters ambayo EMT alijadili na kuniamsha kidogo juu ya umuhimu wa hili; Sasa naelewa kwanini EMT alijenga hoja kwamba Takwimu hii ni muhimu kuliko hata ile ya waliojiandikisha kupiga kura; Kwa mujibu wa findings zangu, 55% ya wakazi wa Arusha ni eligible voters, kwa maana kwamba wana umri kuanzia Miaka 15 na kuendelea (65+); tukumbuke kwamba watanzania wengi uanza kupiga kura wakiwa na umri wa miaka 15, licha ya sheria kutamka miaka 18; Kwa maana hii, ilipofika mwaka 2010, ambapo Arusha ilikuwa na idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura 723,874 kwa mujibu wa NEC, eligible voters ARUSHA walikuwa ni takriban 878,476 (nimepata takwimu hii kwa kutmia projections za 3% population growth per annum); Hii ina maana kwamba wakazi wa Arusha karibia 154,602 hawakujiandikisha kupiga kura 2010 licha ya kuwa eligible voters; Hii ni idadi kubwa sana, hasa ukizingatia kanuni ya sasa ya uchaguzi kwamba: MSHINDI NI MSHINDI;
Vile vile, kufikia Mwaka 2010, 41% ya eligible voters Arusha walikuwa na umri kati ya 15 na 39, huku 14% wakiwa na umri wa miaka 40 na kuendelea (65+); kwa maana hii, eligible voters chini ya miaka 40 walikuwa takribani 543,959, ambayo ni sawa na 75% ya idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura mkoani Arusha 2010, na eligible voters wenye umri wa miaka 40 na kuendelea (60+) walikuwa ni 185,742, ambayo ni sawa na 25% watu waliojiandikisha kupiga kura Mkoani Arusha; Kwahiyo, ifikapo 2015, karibia 75% ya wapiga kura watakuwa hawajavuka umri wa miaka 40; Takwimu hii inaendana na takwimu nyingine nyingi kwenye tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi;
Tumalizie kwa kuangalia takwimu mbili za mwisho ambazo ni muhimu sana: Kwanza ni idadi ya watu kwa majimbo mkoani Arusha, na vile vile idadi ya watu katika majimbo ya CCM na Chadema;
Kati ya jumla ya majimbo SABA ya mkoa wa Arusha, CCM ina majimbo manne, na Chadema ina majimbo matatu; Tukianza na Majimbo ya CCM:
Wilaya Ya Monduli ambayo kiutawala imechanganywa na Longido, ina 15% ya total population ya mkoa wa Arusha; Ngorongoro ambayo pia ni Jimbo na wilaya, ina 11% ya total population ya Mkoa wa Arusha; Arumeru KIUTAWALA ni Wilaya, hivyo ina utata kidogo kwani ina majimbo mawili, huku kila chama (CCM na Chadema), kikishikilia jimbo moja; Nimejaribu kutatua utata huu kwa kufanya roundup/estimates; Arumeru kama wilaya ina takribani 42% ya wakazi wote wa Mkoa wa Arusha; Kwa vile jimbo moja la Arumeru (Arumeru Magharibi) ni la CCM huku lingine ni la Chadema, ili kurahisisha hesabu, tukigawanya 42% kwa majimbo mawili, ina maana kwamba kwa kukisia, Arumeru Mashariki na Magharibi kila moja ina takribani 21% ya jumla ya idadi ya wakazi wa mkoa mzima wa Arusha; Takwimu hii haipo mbali sana na ukweli kwani majimbo mawili ya Arumeru yote na karibia usawa in terms of maeneo ya urban, peri-urban and rural characteristics; Kwa maana hii, tukianza na majimbo ya CCM:
CCM inashikilia majimbo yenye karibia 47% ya wakazi wote wa Mkoa wa Arusha – Longido, Ngorongoro, Arumeru Magharibi na Monduli;
Na kwa Chadema:
Kwa maana hii, Chadema inashikilia Majimbo yenye karibia 53% ya wakazi wote wa Mkoa wa Arusha ambayo ni Arusha mjini, Karatu na Arumeru Magharibi; Swali linalofuatia ni Je, kwa maana hii Arusha ni Ngome ya uhakika ya Chadema?
Kwa mtazamo wa haraka haraka, hii inatosha ku conclude kwamba Arusha ni Ngome ya Chadema; Lakini picha hii inabadilika iwapo tutaangalia jumla ya idadi ya kura kwenye majimbo kwa CCM na Chadema;
Kwanza tutazame Jumla ya Kura za Ubunge katika Mkoa Mzima wa Arusha:
Kwa mujibu wa takwimu za NEC, jumla ya KURA zilizopigwa ngazi ya ubunge katika majimbo yote saba ya mkoa wa Arusha ni kura 368,128; takwimu hii ni inclusive na wapiga kura wapya katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki (2012), ambapo waliongezeka ingawa kwa idadi ndogo sana - kutoka 55,698 mwaka 2010 hadi 60,038 mwaka 2012;
Sasa ebu tutazame kila chama kilipata kura ngapi za ubunge mkoa mzima:
Tukianza na CCM, Jumla ya KURA ilikuwa ni 191,933 kati ya KURA 368,128 (sawa na 52%) ya kura za mkoa mzima wa Arusha, ngazi ya ubunge;
Kwa upande wa Chadema, jumla ya KURA ilikuwa ni 166,056 kati ya KURA 368,128 (sawa na 48%) ya kura za mkoa mzima wa Arusha ngazi, ya ubunge;
Swali linalofuatia ni je: ARUSHA NI NGOME YA CHADEMA?
Iwapo wengi wenu mnakubaliana na uchambuzi wangu, ARUSHA ni aidha GREEN au SANDAKALAWE;
Naombeni mawazo yenu juu ya methodology hii iwapo inafaa kutusaidia kubaini wapi ni GREEN, BLUE & RED, ili tuingia kwenye hatua zinazofuatia;
Pia naombeni mawazo yenu juu ya kigezo cha kutumia (in terms of percentage) kutaja kwamba hii au ile ni RED, BLUE au GREEN; Kuna wachangiaji wachache walikuja na namba hizo, lakini nadhani kigezo hiki kinaweza badilika, hasa kutokana na uchambuzi wangu huu;
Cc:jmushi1, blueray, companero, zitto, mwanamutapa, pasco, zenmoster, nguruvi3, jokakuu, jasusi, director, Africa-spring, for2015, MC, nasdaz, bongolander, EMT, kinenekejo, kagosaki, jujuman, gedeli, remmy; hawa ni wachangiaji ambao niliwasoma kabla ya kuingia mitamboni kuandaa bandiko hili; inawezekana wengine nimewasahau lakini haikuwa kwa nia mbaya;
Zitto, awali ulijenga hoja juu ya umuhimu wa kuja na scientific approach on this phenomenon, nimejaribu angalau to scratch the surface towards that end, nahitaji mawazo yenu katika kuboresha hili, ili tukifikia a consensus juu ya methodology, tutazame mikoa mingine kama Kigoma, Mwanza, n.k ambayo kwa mtazamo wa wengi, mikoa hii sio Green (CCM);
Nawasilisha;