Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

Maafisa watendaji wanasadifu maakida na majumbe enzi za utawala wa wajerumani. Viongozi wa kuchaguliwa hawana issue awamu hii. Ndo maana ma Dc na RC ndio kila kitu. Mbunge diwani au mea anaweza tu kuswekwa ndani kwa amri ya wateule hawa.
This is typical German Direct Rule. Bado tu kichapa viboko
 
Huyo ni maskini wa kila kitu. Ila umasikini mbaya ni wa akili
Ohoooo we ndo mmoja wa wale maskini wa akili na mali. Hv kwa akili ya kawaida mgombea anaeza kosea kuandika mwaka wake wa kuzaliwa kizembe hvyo??.
 
Uchaguzi huu utathibitisha ukweli kuwa Tanzania haina wapinzani na hawa waliopo ni Wajasiriasiasa......wanasaka fursa tu wapate kuishi!
Kivipi, wakati hawatakiwi kushiriki, sasa kwa akili yako unataka wafanye nini.
 
Naona kinachofanywa na utawala uliopo ni kujikweza kutaka kuwaonesha watu nje ya nchi kuwa wanakubalika kwa wananchi.
Ila kiuhalisia ni wanavunja katiba ili kuyapitisha wanayoyataka
 
WALE WANAOLALAMIKA WAMEONEWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WAMEZINGATIA HAYA?
1 . Kama majina yake yatatofautiana kati ya majina aliyojaza kwenye fomu na majina aliyojiandikisha kwenye daftari. Angalia kanuni ya 13 (e) Uk. 152

2. Endapo mdhamini hataandika majina matatu na cheo ktk vyama. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (d) Uk. 10-11

3. Jina alilojaza wakati anachukua fomu lifanane na lililopo kwenye fomu ( dispatch book vs forms). Angalia kanuni ya 17 (1) Uk. 153

4. Mgombea arejeshe fomu mwenyewe na kusaini. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153

5. Majina ya mdhaminiwa yafanane na ya mgombea yaliyojazwa kwenye fomu. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (a-d) Uk. 10-11

6. Fomu ya kiapo iwe halisi iliyotolewa na msimamizi msaidizi na ishuhudiwe na msimamizi msaidizi ngaz husuka. Angalia kanuni ya 16 (e) Uk. 152

7. Fomu zijazwe na mhusika lazima ziwe zimesainiwa. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (e&f) Uk. 10-11

8. Fomu zishuhudiwe na ngazi ya chini ya chama itakayobainishwa na chama. Angalia mwongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.1 & 14.2 (a) Uk. 10-11

9. Ambaye hajajiandikisha hana sifa ya kuwa mgombea. Angalia kanuni ya 13 (e)Uk. 152, ilinganishe na Kanuni ya 16 (d) Uk. 152 na Kanuni ya 14 (a) Uk. 152

10. Aliyejiandikisha mara mbili atakuwa amepoteza sifa ya kugombea au kupiga kura. Angalia kanuni ya 14 (b)Uk. 152
11. Lazima aeleze shughuli halali inayomwingizia kipato na endapo atabainika kudanganya atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (d)Uk. 152
12. Atakayeomba nafasi zaidi ya moja kwenye fomu moja atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 17 (1) & (5) Uk. 152-153
13. Nafasi anayoomba ionekane mpaka kwenye fomu ya kiapo. Angalia kanuni ya 17 (1)Uk. 153 isome sambamba na Kanuni ya 16 (e) Uk. 153
14. Fomu zijazwe kwa ukamilifu. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153
15. Eneo la uraia ajaze uraia siyo nchi mfano: Mtanzania na siyo Tanzania. Angalia kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154
16. Usahihi wa maeneo kwa mujibu wa GN mfano chankobe akiandika chakobe atakuwa amepoteza sifa maana eneo hilo litakuwa halipo ktk GN. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152 & Kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154.

17. Mwombaji aeleze anaomba nafasi ipi na wapi mfano nafasi anayoomba mwenyekiti wa Kijiji cha Kagera vinginevyo atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152

18. Fomu ijazwe taarifa inayohitajika tu, kuwepo kwa maandishi au michoro isiyohitajika hilo ni kosa. Angalia kanuni ya 17 (5) Uk. 154

19. Mgombea arejeshe fomu zote mbili kinyume na hapo hana sifa. Angalia kanuni ya 17 (2), (3) na (4) Uk. 153-154

20. Kama mgombea ameomba nafasi mbili unaweza kumteua nafasi moja. Angalia kanuni ya 17 (1)& (5) Uk. 153-154

21. Mgombea akiwa na ajira, wadhifa au uteuzi wowote katika mihimili ya Serikali atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Anagalia kanuni ya 16 (f)Uk. 153

22. Ikiwa Mgombea alichukua fomu na hakurejesha atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia Kanuni ya 17 (2), (3) na (4)

23. Mgombea ambaye hatadhaminiwa na ngazi ya chini ya Chama chakeatakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia mwongozo wa uchaguzi sehemu 14.1 na 14.2 (a)

Kabla ya kulalamika kukatwa majina,Jiridhisheni kwa kila hatua kama mmekidhi vigezo na masharti sio kulalama...
 
Hizo fomu za CHADEMA mtazisomea wapi wakati walipotaka kurejesha mlifunga milango ya ofisi?
 
Kumbe mmeambiwa mjaze fomu hizo kwa makosa ili itokee kilichotokea. Nia na madhumuni kuwaaminisha wananchi pamoja na mabeberu kuwa mnaonewa na serikali ya Rais Magufuli. Tumewastukia.
 
Hawa jamaa zangu hawakujiandaa vyema kwani nikichukulia mfano wa wilaya ya longido ni wagombea wawili tu ambao walichukua fomu kupitia chadema kugombea .
Tukisema hawakujipanga mtachukia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…