Utaratibu wa kuwekana na kuondoana madarakani kwa kura ni wa wazungu lakini hata sisi waafrika pamoja na uduni wetu unaonekana ndio utaratibu sahihi na unatufaa. Hii ni kwa sababu utaratibu mbadala ni kuwa na mfumo wa kifalme ambapo kwa sasa ni ngumu ku-implement.
Kama mamlaka zinafikiri zinaweza kupata madaraka bila ridhaa ya wananchi basi wabuni mfumo sahihi na sio hivi viini macho maana sasa watu ni waelewa. Mbali na hapo wakitokea miongoni mwetu wakakubali kwamba mfumo wa upigianaji kura umefeli na kuamua kubuni wa kwao basi tumuombe Mungu wasije wakabuni kitu kibaya kitakacho haribu hata kidogo tulichokwisha kijenga. Tukumbuke miongo mitatu iliyopita Somalia ilikuwa nchi imara.
Maneno kuwa Haki huinu taifa hakuna hata mmoja wetu mwenye akili timamnu anayeyakataa!