Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Toka mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulipoanza, tumeshuhudia mambo mengi ya hovyo yakifanywa na TAMISEMI, chini ya Waziri Mchengerwa, kuanzia kutunga kanuni mbaya za kusimamia uchaguzi, kama ile ya kuwalinda wasimamizi wa uchaguzi wasishtakiwe wanapofanya makosa hata ya kijinai wakati wa zoezi la uchaguzi; kuandikisha watoto wadogo kuwa wapiga kura, kuwaengua wagombea kupitia vyama vya upinzani kwa karibia 65%, hadi kuanza kuwanyanyasa wapinzani wakati wa mikutano ya kampeni.
Nyakati zote, kati ya watu waliopaza sauti dhidi ya ushetani huu, ni watumishi wa Mungu. Hawa nawaita ni watumishi wa kweli wa Mungu wanaoiishi kweli ya Bwana. Watumishi hawa wa Mungu, kwa ukakamavu na ushujaa wa kiroho, walipaza sauti dhidi ya matendo haya ya kishetani. Tunawapongeza sana viongozi hao walioamua kuviishi viapo vyao vya kuwa wasemaji, wakemeaji na waonyaji dhidi ya vitendo vyote vya kishetani. Lakini nafahamu wazi kuwa hawa wanaotenda huu ushetani hawapendi kabisa wakemewe wala kuonywa, na hivyo watapandisha chuki zao dhidi yao. Lakini nina hakika watumishi hawa wa Mungu, hawawezi kulegea na kufumba vinywa vyao kutokana na kuchukiwa na shetani. Kwa mtumishi wa Mungu, kuchukiwa na shetani na kutenda yaliyo kinyume na mapenzi ya shetani, ni utakatifu mbele za Mungu.
Jukumu kubwa la viongozi wa dini na hata waumini wa dini ni kuwa jasiri dhidi ya uovu wote. Lazima tuuchukie, na kuukemea uovu wote iwe ni uovu wa kisiasa, uovu wa kiuchumi, uovu wa kimaadili au uovu wa kiimani.
Mungu wetu wa huruma, daima ni jasiri, yeye aliuvaa ubinadamu wetu ili atuoneshe tukiwa na mwili huu wa kibinadamu tunatakiwa kusimama vipi dhidi ya mabaya yote. Ipo mifano mingi jinsi watumishi manabii wa Mungu walivyosimama na kunena kwa ujasiri mkuu dhidi ya watawala dhalimu walioutumikia uovu na himaya ya shetani.
Kuwanyima watu nafasi ya kuwachagua viongozi wanaowataka ni ushetani, chama kinachofanya hivyo ni Chama Cha Mashetani, na watu wote wanaounga mkono au kukaa kimya dhidi ya ushetani huu , ni mahalifa wa shetani.
Kuwafumba watu midomo kwa kuwateka, kuwapoteza na kuwaua ili waliobakia waogope kuunena ukweli dhidi ya maovu ya watawala au serikali, ni ushetani.
Watu wachache kujimilikisha nchi na kuwatendea uovu wengine wote, ni ushetani.
Kuujua ukweli wote juu ya uovu uliopo unaotendwa na watawala, serikali au taasisi zake, lakini ukaamua kuwa chawa wa chama kinachosimamia maovu, au watawala waovu ili tu ulinenepeshe tumbo, unakuwa sehemu ya uovu, na huo ni ushetani.
Hima wananchi wote, viongozi wetu wa dini na waumini wa dini zote, tusimame kwa ujasiri dhidi ya ushetani wote, tusimfanye shetani kuwa mshindi katika maisha yetu. Tukiungana tutaishi kwenye kwenye Taifa la haki, lenye neema na baraka za Mungu wetu, kwa sababu tumeyaishi mapenzi yake. Mungu wetu ni Mungu wa haki, hatasimama na wanaoiua haki. Wamelaaniwa wadhulumaji wa haki, Duniani na ahera.
Kwa moyo wa unyenyenyekevu mkuu, pamoja na jitihada zetu, tuombe kwa imani, Mungu azidi kuwajalia yote mema viongozi wetu wanaosimama katika haki, lakini awafedheheshe, kuwatia unyonge na kuwalaani wote wanaosimama upande wa dhuluma zote.