LGE2024 Uchaguzi serikali za mitaa: Mamia ya wagombea wa upinzani waenguliwa, waapa 'kutosusia shamba'

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mamia ya wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi wa serikali za mitaa ujao wameenguliwa kushiriki uchaguzi huo.

Chama cha ACT Wazalendo kimeripoti takribani asilimia 60 ya wagombea wake wameenguliwa kushiriki uchaguzi kwa sababu walizozitaja kukosa msingi wa kisheria na kanuni.

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi, tarehe 8 Novemba ilikuwa ni siku ya uteuzi wa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Hata hivyo wagombea wa vyama vya upinzani pekee ndio wameripotiwa kuenguliwa kwasababu ya kukiuka utaratibu au kukosa vigezo mbalimbali.

Soma, Pia;

CHADEMA wanatoa Tamko kuhusu hali ya Kisiasa inayoendelea nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Wakati Chadema ikiendelea kupata orodha kamili ya wagombea wao wote walioenguliwa nchi nzima, jana tawi la chama wilayani Kilosa liliwasilisha barua yenye uthibitisho wa wagombea 242 walioenguliwa katika wilaya ya Kilosa pekee.

Chadema inasema wapo wagombea wengine kutoka jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma ambao si tu wameenguliwa kushiriki uchaguzi bali pia wameshutumiwa kutokuwa raia.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema katika jimbo la Tunduru Kaskazini, wagombea wao 69 wameenguliwa, waliopitishwa ni 23 tu.

Jimbo la Kigoma mjini wagombea wao 63 wameenguliwa na kubakizwa wagombea watano pekee.

Jimbo la Tunduru Kusini, ambalo ACT Wazalendo wanadai kuwa ni moja ya ngome yao kubwa, ni wagombea 13 tu ndio walioteuliwa huku wagombea 34 wakiwa wameenguliwa.

“Maeneo mengi ambayo wameengua wagombea wetu ni maeneo ambayo tulikuwa tunatarajia kushinda.

Wamefanya ‘mapping’ ya kuangalia huyu ana uwezo, ndio wanamuengua.

Kwenye ngome zetu hasa ndio tumeathirika pakubwa kuliko sehemu zingine” amesema Esther Thomas, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Tanzania Bara. Baadhi ya wagombea wa ACT Wazalendo wameambiwa sababu ya kuenguliwa ni kutokuwepo kwa nafasi walizoomba na kujaza fomu vibaya. Chadema wamesema kuna wagombea wao ambao wameenguliwa nje ya muda wa kisheria na pasipo kuwekewa mapingamizi halali.

“Hali ni mbaya sana maana wagombea wetu wameenguliwa hadi usiku, ambapo ni nje ya muda. Watu tu wanaitwa wanapewa barua, wanaambiwa wameenguliwa” amesema Jon Mrema, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema.

Mrema anasema baadhi ya wagombea wameambiwa wameenguliwa kwasababu chama chao cha Chadema hakijasajiliwa. Wagombea wengine kutoka Dar es Salaam wameenguliwa baada ya kujaza katika fomu zao kwamba kazi inayowapatia kipato ni ujasilia mali. “Wasimamizi wanawaengua wanasema ujasiliamali sio kazi. Sasa sisi tunajiuliza, kama ujasiliamali sio kazi halali ilikuwaje serikali ikawapa hadi vitambulisho?” amehoji Mrema.

Vyama vyote vimewasilisha mapingamizi kutaka wagombea wao warudishwe, na wanatarajia kupata majibu kufikia mwisho wa siku leo. Vyama pia vina siku tatu za kukata rufaa ambapo maamuzi ya rufaa zote yatatoka tarehe 13 Novemba. Siku mbili zilizopita, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa alivikumbusha vyama vya siasa , wagombea na wadau wengine wa uchaguzi kwamba muhisika yeyote asiyeridhika na taratibu za uchaguzi ana haki ya kukata rufaa.

“Mtu yeyote mwenye malalamiko ni vyema akajikita katika kufata sheria, kufuata kanuni, kwani kanuni na sheria zetu hazijaacha ombwe kutokana na jambo lolote linaloweza kuibuka kutokana na uchaguzi huu” amesema Mchengerwa.

Siku ya Ijumaa Katibu Mwenezi wa chama tawala Chama Cha Mapinduzi Amos Makalla alitoa wito kwa Wizara ya Tamisemi inayosimamia uchaguzi kuhakikisha inatenda haki kwa vyama vyote huku akisisitiza kwamba CCM haihitaji kubebwa. “CCM hatuhitaji upendeleo wowote, CCM hatuhitaji kubebwa, kwahiyo tuko tayari, tulishajipanga, hatuhitaji mbeleko” alisema Makalla.

Chadema wamefananisha kile kinachoendelea sasa na yale yaliyotokea mwaka 2019 ambapo wagombea wa vyama vya upinzani karibu kote nchi walienguliwa kushiriki katika uchaguzi.

“Awali tulidhani kwamba baada ya serikali na Rais Samia Suluhu Hassan kusema uchaguzi utakuwa uhuru na wa haki, tukadhani yale yam waka 2019 hatutarudi kule. Lakini ghafla tunaona tunarejeshwa mwaka 2019, na imekuwa ghafla mno. Na tulianza kuona dalili hizi pale wakati wa zoezi la uandikishwaji ambapo hadi Watoto ambao hawajafikisha miaka18 waliandikishwa” amesema Mrema.

Hata hivyo vyama vyote viwili Chadema na ACT Wazalendo vimesisitiza kwamba havitajitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na malalamiko ya dhulma wanazotendewa wagombea wao.

“Wanachokitafuta ni kutuchokoza, kutupa sababu tuseme kwamba tunasusa.

Tumeshasema hatutasusa hata tukibaki na Kijiji kimoja, tutaendelea kushiriki kwasababu kushinda mtaa mmoja ni ushindi wa maana kwasababu sasa hatuna mtaa hata mmoja nchi hii tunaouongoza kati ya mitaa takribani elfu 5 iliyopo. Kati ya vitongoji elfu 64 vilivyopo katika nchi hii hatuongozi kitongoji hata kimoja. Kwahivyo hata tukibaki na kitongoji kimoja na tukashinda, maana yake ni kwamba tuna ushindi wa asilimia 100,” amesema Mrema.

“Siku zote sisi hatususii shamba. Maana ukisusia shamba, litaliwa lote litaisha. Kwahiyo tunapambana huku tukishiriki, na tunashiriki huku tukipambana” amesema Thomas.

Credit: BBC Swahili

Soma:

ACT wazalendo: Wagombea wetu Kigogo, Dar es salaam hawajateuliwa

John Mrema aanika madudu ya TAMISEMI, waongeza sifuri na herufi kuwakosesha sifa Wagombea
 
Waliulizwa lugha wanazo zijua ukijubu zote kiswahili na kimombo unaenguliwa, (unatakiwa uwe mbumbumbu)
 
Nchii hii inavituko sana,hivi ni kweli waliopewa dhamana wanaitakia hii nchi mwema?
Siku tatu za kukata rufaa ni kiini macho,hata wazisikilize hizo rufaa kwa masaa24 hawataweza kuzimaliza,
Hata hivyo huo ni mkakati wa chama na serikali.
Kwa maana hiyo suala la rufaa sio mwarobaini wa tatizo hilo.
Na kwa mtazamo wangu hata uelewa kwa wasimamizi ni mdogo kwa sababu kila mmoja ana kununi zake binafsi.
 
Rufaa zao vipi?? Zimesikilizwa???
 
Kama 80% wameenguliwa hakuna maana kushiriki huu uchafuziView attachment 3148867
 

Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
    420.8 KB · Views: 5
  • 20240907_095744 (1).jpg
    116.1 KB · Views: 6
  • IMG-20200726-WA0000.jpg
    43.7 KB · Views: 4
  • 5810871-156c33252d331784831e630b50148deb.mp4
    2 MB
  • 5811523-6041f5af6e2b5c7600d07027005d6658.mp4
    3.7 MB
Kanuni za sheria ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa zinasema:

1. Umri wa mgombea ni kuanzia miaka miaka 21. Chadema inateua wagombea wa umri wa miaka 18 hadi 20.

2. Mgombea awe anajua kusoma na kuandika kiswahili na kiingereza. Chadema inaweka wagombea ambao hawawezi hata kuandika majina yao kwa usahihi.

3.Mgombea hatakiwi kuwa na ugonjwa wa akili. Chadema inaweka wagombea wenye akili zilizoathiriwa na madawa ya kulevya, bangi, viroba, wenye mafaili Mirembe, C1 etc

4. Mgombea lazima awe na kazi rasimu inayomupatia kipato cha uhakika cha kuendeshea maisha yake. Chadema inaweka wagombea ambao ni jobless, wapiga debe, matapeli, panya roads, waganga njaa, wasio na uhakika kama kesho watakula, wazururaji, machangudoa etc

5. Mgombea lazima awe ni mwanachama hai wa chama chake. Chadema inaweka wagombea ambao hawana hata kadi ya uanachama wa chadema.

6. Mgombea asiwe alishawahi kuhukumiwa na kufungwa jela kwa zaidi ya miezi 6 kwa kosa la jinai. Chadema inaweka wagombea ambao walishawahi kufungwa jela kwa makosa ya ujambazi, wizi, ubakaji, ukabaji, utekaji na kadhalika.

7. Mgombea lazima awe ni raia wa Tanzania. Chadema wanaweka wagombea ambao hawa kadi au namba ya NIDA.

8. Mgombea lazima awe ameshajiandikisha kwenye daftari la uchaguzi wa serikali za mitaa. Chadema inaweka wagombea ambao hawakujiandikisha kwenye daftari hilo.

10. Na kadhalika. Yaani vyama vya upinzani kwa kujua au lutojua havizingatii sheria na kanuni za kuteua wagombea wa uongozi wa serikali za mitaa. Vimekuwa ni makokoro ya mtu yo yote kuwa mgombea. Hili haliwezi kukubalika. Lazima hao wasio na sifa za kisheria waenguliwe.
 
Pumbavu
 
Upuuzi mtupu! Mnachokifanya kwa wapinzani, mnatafuta machafuko! Msifikiri watu ni wajinga kama machawa wa ccm! Matokeo ya mnayo yafanya mtayaona! Hamkujifunza kwa magufuli bado mnaendeleza upumbafu na ulimbukeni wa madaraka mnaona ni sifa! Na mnategemea uchaguzi wa amani??? Mashetani ninyi! Upinzani wamewakosea nini! Hakuna mwanaccm kamili anayependa upumbavu huu mnaoufanya, wote wanaofanya ujinga huu awe mkurugezi, au nani ni watu wajinga haijalishi ana cheo gani huyo ni shetani ambaye ana ngozi ya binadamu! Inawezekanaje upinzani tu ndio wanaokosea????? Alafu mnatuambia tuwaombee ninyi??? Ety Tanzania ni kisiwa cha amani kwa upumbavu huu mapigo ya Mungu yatashuka! Magufuli alitaka kujimilikisha tanzania iwe ya chama kimoja alafu bila unqfiki akaenda kuinua biblia anaapa na anajua ujinga alioufanya akafikiri Mungu ni mpumbavu kama yeye! Kilichompata kasome kisa cha herode! Mungu hadhihakiwi unachokipanda utakivuna msifikiri Mungu hayupo, matokeo yake hakufaidi hata mwaka mmoja na maccm wenzake walioingia kwa dhuluma! Na kwa taarifa zenu wale wote walioshiriki uharamia wa 2020 uwe mkurugezi, waziri, sijui nani polisi, wengi wamekufa vifo vya ajabu, na waliobaki ni kwa huruma za Mungu na wasifikiri kwamba wana akili sana ni neema ya Mungu tu anawasubiri watubu! Kwa nini nyie viongozi msitende haki mmeapa kwa kuinua misaafu na biblia kuitetea katiba, mbona nyie ni wanafiki sana mnafikiri Mungu ni mjinga????? Mnajali matumbo yenu ila kujali wezenu ambao ni vyama vya upinzani mnawaona kama ni maadui zenu????? Upumbavu huu magufuli aliounzisha na kujaza makada wenye njaa kwenye uongozi ndio matokeo ya tunayoyaona! Sasa badala ya kuwaombea tutaomba Mungu ashugulike na kila anayefanya kinyume na alichoapa kukitenda! Hatuwezi kuendelea kuishi maisha ya namna hii! Chadema sio watu????? Kwa nini msiwaelimishe na kurekebisha hayo makosa madogo mnayoyasema kama kweli wewe kiongozi una upendo mbona kipindi cha kikwete ujinga huu haukuepo??? Acha kutufanya watanzania wote kuwa ni wajinga! Mimu ni mwanaccm na nampenda mama kwa kazi nzuri lakini kwa ujinga huu na upumbavu kama na yeye anahusika ! Mungu ashugulike na yeye na kama ni wa chini yake Mungu ajua? Maana yeye huwezi kumficha kitu!
 

Angalia huyo ni wenu na uangalie alivyojaza.
 
Hivi wewe akili yakwako imehama au basi ni mgonjwa!!
 
Mambo ya siasa waachie wanasiasa. Kila mwanaume anapopambana kumpata msichana, hutumia mbinu chafu, kuhonga, kumdhuru mshindani na kila mbinu zote ili mradi tu afanikiwe..
 
Umeenguliwa nini? Maana si povu hilo.

Majanga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…