LGE2024 Uchaguzi serikali za mitaa: Mamia ya wagombea wa upinzani waenguliwa, waapa 'kutosusia shamba'

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Anaitwa docta Akili lkn sijui kama humo kuna Akili. Ulichoandika hakionyeshi Akili TIMAMU.
 
Huyu mama amekuwa bingwa sana wa kutafuta umaarufu ubwete (cheap popularity) kwa kutatua matatizo kwa mdomo wake yaliyotengenezwa na mikono yake.

Ninaiona drama fulani iliandaliwa kuhusu kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani.
 
Huyu mama amekuwa bingwa sana wa kutafuta umaarufu ubwete (cheap popularity) kwa kutatua matatizo kwa mdomo wake yaliyotengenezwa na mikono yake.

Ninaiona drama fulani iliandaliwa kuhusu kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani.
chawa wanafanya yote hayo kisha wanamwambia cha kusema, bora umewapa makavu najua wameona huu uzi.
 
“Mtu yeyote mwenye malalamiko ni vyema akajikita katika kufata sheria, kufuata kanuni, kwani kanuni na sheria zetu hazijaacha ombwe kutokana na jambo lolote linaloweza kuibuka kutokana na uchaguzi huu” amesema Mchengerwa
Lugha kama hii ni kama ya Tlaatlaah; mmoja tuliye naye humu JF.
Inawezekana mtu hyo ni huyu huyu Mchengerwa?
 
Unatengeneza tatizo halafu unaliletea ufumbuzi.. Ili kupata political mileage!? Kisha usifiwe?😡🤔🙇🏿‍♂
Mama ni "Msikivu".

Sijui tuliweza vipi kuwa na viongozi vihiyo kama hawa.

Huyo mama hana chembe ya aibu/soni hata akifanya vioja ambavyo kila mtu anaona ni vioja.
Siyo hivyo tu, Samia ni mtu ambaye wakati mwingine utadhani ni mtu mwenye huruma sana; rejea alivyo kuwa akipapasa mto wa Tundu Lissu pale hospitalini Nairobi, na kujifanya kuwa hata kuondoka hapo anashindwa, kwa jinsi alivyo guswa na mkasa ulio mpata Lissu. Sasa fananisha hali hiyo na haya yanayotokea sasa hivi chini ya utawala wake; watu kupotezwa, kifo cha kikatili kilicho mpata Mzee Ali Kibao. Kwake haya ni "drama", na kwamba "kifo ni kifo tu."

Huyu ndiye kiongozi asiye guswa kabisa na matatizo yanayo wakabili wananchi anao waongoza.
 
Mimu ni mwanaccm na nampenda mama kwa kazi nzuri lakini kwa ujinga huu na upumbavu kama na yeye anahusika ! Mungu ashugulike na yeye na kama ni wa chini yake Mungu ajua? Maana yeye huwezi kumficha kitu!
Andiko lako lilieleweka vizuri huko juu; lakini ukamaliza kwa kujichanganya mwenyewe. Unampenda mama kwa kazi nzuri ipi hasa? Huu ndio unafiki usio kuwa na tija.
 
Ila vyama vya upinzani ni pasua kichwa. Yani chama wagombea wake Asilimia 60 wameenguliwa lakini analazimisha kuwa hawatasusia. Haya bwana.
 
Kama 80% wameenguliwa hakuna maana kushiriki huu uchafuziView attachment 3148867
Sidhani kama kuna mtanzania yoyote ambaye swala la uchaguzi analitilia mkazo sana mpaka apande ghathabu yoyote. Uchaguzi utapita watu wataendelea na shughuli zao mioyo ya watanzania kwenye swala la uchaguzi kwa katiba hii imekufa ganzi. Atakaye fanya fujo ataishia kupokea kipondo na mateso tu yasiyo na sababu, hii ndiyo demokrasia ya kiafrika tangu Enzi za mababu zetu ukitaka kuwa kiongozi lazima uwe mtemi, turudishe tu zile mila natamaduni zetu yaani hakuna sababu ya kupiga kura mtu kama anataka uongozi anachaguliwa wachama hiki na wachama hiki wanawekwa kilingeni wanapigana anaye shinda ndiye anapewa uongozi, tusifuate hizi taratibu za wazungu hatuziwezi.
 
Mimi wala sishangai wapinzani kuenguliwa hata hao waliyo pitishwa kugombea hawatashinda. Cha muhimu wahisika wamalize zoezi lao tuendelee na shughuli nyingine. Wasimamizi wote wauchaguzi ni watu wachama kimoja na wengi wao ni makada, unategemea nini? Huu uchaguzi ni kiini macho tu, wapinzani wao waende wakajilimie tu, hakuna uchaguzi wowote mtajidai mnapigania haki zenu mtaishia kufungwa tu jela, Kipindi cha Chama kimoja uchaguzi ulikuwa unakwenda vizuri sana tena kwenye vituo vya kupiga kura wanafunzi ndiyo walikuwa wanasimamia uchaguzi tukimaliza zoezi tunapewa sh. 5 kila mtu tunarudi nyumbani hakuna sekeseke yoyote. Nishauri turudishe mfumo wa chama kimoja tunaweza tukapata viongozi wazuri kuliko sasa.
 
Acha waongozwe kimabavu hopefully watatia akili.

CCM wamekuwa wabaya kuliko wakoloni.
 
Kama wameondolewa kisheria hana mamlaka kuwarudisha kinyume cha sheria.
 
Sasa na wewe ulienda kusomea ujinga.
Huo wako ndiyo ujinga, sisahishi typo hata siku moja, nasahihisha R na L, upo hapo ulipo kondoo?

Au kama kitu huelewi nakufundisha.

Uislam mwema sana. No complications.
 
Huo wako ndiyo ujinga, sisahishi typo hata siku moja, nasahihisha R na L, upo hapo ulipo kondoo?

Au kama kitu huelewi nakufundisha.

Uislam mwema sana. No complications.
Huna ishu na unakosea mara nyingi unajiona uko mkamilifu, wengine hukosea typing na wewe unawambia kauli mbovu wakati wewe mwenyewe unakosea mda wote. Huna cha kunifundisha.

kama mimi ni kondoo wewe ni Ngurue jike lisilo na ustaarabu. Dini yako ndivyo inavyokufundhisha hizo tabia za kudharau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…