MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Hakuna kuendelea na taratibu za Uchaguzi ambao umejaa hujuma na maigizo ya kisanii.Tuziombe taasisi zote za haki za binadamu,asasi za kiraria na vyama vya siasa waungane kushinikiza serikali kuondoa tarehe iliyopangwa Uchaguzi kufanyika na kupanga upya zoezi lianze upya.
Hatuwezi kuingia kwenye Uchaguzi ambao madhala yake tunayaona siku za usoni. Amani ya nchi yetu inavurugwa makusudi na watu waliojaa ghilba, tamaa za madaraka,chuki na uonevu mkubwa. Uchaguzi huu ufutwe na kisha urejewe upya kwa taratibu za awali.
Haiwezekani nchi nzima wapinzani pekee ndio wenye matatizo na ujazaji fomu za kugombea. Hii sio haki ni uonevu wa hali yajuu. Wananchi wasikubaliane na mambo ya hovyo namna hii.
Waziri Suleiman Jafo atambue kua yeye ndiye mwenye dhamana na mambo haya asiache tufikie tusikopataka, asije akajikuta katika mtihani wa kujibia hili. Tatizo ni kubwa na lipo wazi, hii haijawahi kutokea tangu nchi yetu ipate Uhuru na hatutakubaliana nalo. Acheni ushindani ufanyike kwa haki kwani bado ni mapema sana.
Tusijivunie kuwaonea raia wa vyama vya upinzani kwa kujivunia vyombo vya usalama kuwadhibiti, Tutambue kua raia ndio waliotunga Sheria kuhusu uwepo wa vyombo hivi. Raia wote ndio taifa na sio watu wachache kujimilikisha taifa. Huatwezi kufika mambo ya namna hii
= = = = = = = = = = = = = =
Ushauri kutoka kwa Mystery
Kutokana na Waziri Suleiman Jafo, kutangaza kuyarudisha majina yote yaliyokuwa yamekatwa hapo awali na kuyarudisha kwenye uchaguzi, ni bora yakafanyika mawazo ya busara na kuufuta huu uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu na kipangwa tarehe nyingine mbele na usimamiwe na Tume ya uchaguzi ya Taifa.iliyo huru,kwani ni dhahiri hawa wasimamizi wa uchaguzi huu, ambao ni makada wa CCM, waliosababisha uchaguzu huu uvurugike,hawafai tena kuendelea kusimamia uchaguzi huo
Naiomba sana serikali ifuate ushauri kwa kuwa inapaswa kuona zoezi zima LA kuchagua viongozi wa serikali za mitaa ni mitaa ni LAZIMA liwe huru, kwa kuwa wananchi wenyewe ndiyo wanaopaswa kuwachagua viongozi watakaowawakilisha.
Ili kurejesha ari ya wapiga kura, ni vyema zoezi zima la kuanzia kujiandikisha wapiga kura, uchukuaji wa fomu kwa wagombea likaanza upya kabisa, chini ya wasimamizi wapya, Tume ya uchaguzi ya Taifa
Kwa kuwa zoezi zima la uchaguzi huru na wa haki lina umuhimu mkubwa na kama mjuavyo wasimamizi hao wamethibitisha pasipo shaka yoyote, kupendekea chama cha CCM, hawafai tena kupewa hukumu hili la kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki
Niwape mfano mmoja tu, mathalani kuna mechi ya mpira baina ya watani wa jadi baina ya Simba na Yanga, itokee refa na washika vibendera wote 2 wawe ni wanachama wa timu mojawapo kati ya hizo 2, utegemee ile timu nyingine, ipeleke timu uwanjani??
Ni dhahiri hiyo timu pinzani, haitapeleka timu uwanjani na haiwezi laumiwa na uamuzi huo, wa kutopeleka timu uwanjani
Vivyo hivyo katika uchaguzi huu, iwapo serikali hii ina nia ya dhati kabisa ya kuuendesha uchaguzi huu uwe wa huru na wa haki, ni lazima wahusishe wapinzani, hususani wa vyama vikuu vya uoinzsni nchini vya Chadema na ACT wazakendo, katika zoezi zima la uchaguzi na kusiwe na kificho cha aina yoyote, ili zoezi hilo lihesabike kuwa huru na la haki