Uchaguzi Serikali za Mitaa ufutwe

Uchaguzi Serikali za Mitaa ufutwe

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Hakuna kuendelea na taratibu za Uchaguzi ambao umejaa hujuma na maigizo ya kisanii.Tuziombe taasisi zote za haki za binadamu,asasi za kiraria na vyama vya siasa waungane kushinikiza serikali kuondoa tarehe iliyopangwa Uchaguzi kufanyika na kupanga upya zoezi lianze upya.

Hatuwezi kuingia kwenye Uchaguzi ambao madhala yake tunayaona siku za usoni. Amani ya nchi yetu inavurugwa makusudi na watu waliojaa ghilba, tamaa za madaraka,chuki na uonevu mkubwa. Uchaguzi huu ufutwe na kisha urejewe upya kwa taratibu za awali.
Haiwezekani nchi nzima wapinzani pekee ndio wenye matatizo na ujazaji fomu za kugombea. Hii sio haki ni uonevu wa hali yajuu. Wananchi wasikubaliane na mambo ya hovyo namna hii.

Waziri Suleiman Jafo atambue kua yeye ndiye mwenye dhamana na mambo haya asiache tufikie tusikopataka, asije akajikuta katika mtihani wa kujibia hili. Tatizo ni kubwa na lipo wazi, hii haijawahi kutokea tangu nchi yetu ipate Uhuru na hatutakubaliana nalo. Acheni ushindani ufanyike kwa haki kwani bado ni mapema sana.

Tusijivunie kuwaonea raia wa vyama vya upinzani kwa kujivunia vyombo vya usalama kuwadhibiti, Tutambue kua raia ndio waliotunga Sheria kuhusu uwepo wa vyombo hivi. Raia wote ndio taifa na sio watu wachache kujimilikisha taifa. Huatwezi kufika mambo ya namna hii

= = = = = = = = = = = = = =

Ushauri kutoka kwa Mystery

Kutokana na Waziri Suleiman Jafo, kutangaza kuyarudisha majina yote yaliyokuwa yamekatwa hapo awali na kuyarudisha kwenye uchaguzi, ni bora yakafanyika mawazo ya busara na kuufuta huu uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu na kipangwa tarehe nyingine mbele na usimamiwe na Tume ya uchaguzi ya Taifa.iliyo huru,kwani ni dhahiri hawa wasimamizi wa uchaguzi huu, ambao ni makada wa CCM, waliosababisha uchaguzu huu uvurugike,hawafai tena kuendelea kusimamia uchaguzi huo

Naiomba sana serikali ifuate ushauri kwa kuwa inapaswa kuona zoezi zima LA kuchagua viongozi wa serikali za mitaa ni mitaa ni LAZIMA liwe huru, kwa kuwa wananchi wenyewe ndiyo wanaopaswa kuwachagua viongozi watakaowawakilisha.

Ili kurejesha ari ya wapiga kura, ni vyema zoezi zima la kuanzia kujiandikisha wapiga kura, uchukuaji wa fomu kwa wagombea likaanza upya kabisa, chini ya wasimamizi wapya, Tume ya uchaguzi ya Taifa

Kwa kuwa zoezi zima la uchaguzi huru na wa haki lina umuhimu mkubwa na kama mjuavyo wasimamizi hao wamethibitisha pasipo shaka yoyote, kupendekea chama cha CCM, hawafai tena kupewa hukumu hili la kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki

Niwape mfano mmoja tu, mathalani kuna mechi ya mpira baina ya watani wa jadi baina ya Simba na Yanga, itokee refa na washika vibendera wote 2 wawe ni wanachama wa timu mojawapo kati ya hizo 2, utegemee ile timu nyingine, ipeleke timu uwanjani??

Ni dhahiri hiyo timu pinzani, haitapeleka timu uwanjani na haiwezi laumiwa na uamuzi huo, wa kutopeleka timu uwanjani

Vivyo hivyo katika uchaguzi huu, iwapo serikali hii ina nia ya dhati kabisa ya kuuendesha uchaguzi huu uwe wa huru na wa haki, ni lazima wahusishe wapinzani, hususani wa vyama vikuu vya uoinzsni nchini vya Chadema na ACT wazakendo, katika zoezi zima la uchaguzi na kusiwe na kificho cha aina yoyote, ili zoezi hilo lihesabike kuwa huru na la haki
 
Mkuu kwani kuna uchaguzi wa kuchagua nini?tuendelee kusubiri always MUDA ni hakimu mwema ,its only 6yrs to go,then upepo utabadilika na kuvuma kutokea upande mwingine au yaliyotokea na yanayotokea Chile,Hong Kong,Venuzuera,Malawi,unafikiri yanaweza tokea hapa kwetu ????again TIME will tell.
 
Wewe na wenzako ni wajinga sana, mlikuwa mnahamasishana humu kususia kujiandikisha, sasa ivi mnalialia mnataka uchaguzi!
 
Umenena vyema Sana mtoa hoja ila ingekuwa vizuri ungetuwekea data za kutosha kuhusu hoja zako ili tukuelewe zaidi,kwani kusema Tu bila ushaidi ni ngumu kukuamini

Je wapinzani wamekataa kweli kwa kuonewa au ni mpango wao? Nadhani waliokuwa wanajaza walikuwa na kopi za hizo karatasi watuonyeshe hayo pia
 
Safari hii chini ya utawala wa Naibu Rais Daud Bashite na mtukufu magufuli hakuna uchaguzi bali kuna Mbinu za kurejesha mfumo wa chama kimoja wapate kutawala milele na milele kama China Cameroon Uganda cuba
 
hivi mbona chadema ilihamasisha watu wasijiandikishe what has just happned??[emoji3][emoji3]
 
Uchaguzi wote tu ufutwe
Wabaki wao tu Tujue moja

Ova
 
Kama hamtaki uchagzi wa serikli za mitaa kubalini iwe nchi ya chama kimoja na muache kulalama
 
Wapinzani wakishiriki uchaguzi huu kura yangu nawapa ccm,gomeeni uchaguzi
Nalog off
 
Niliwahi kushauri humu sometimes back kuwa uchaguzi kama huu wa serikali za mitaa usihusishe vyama vya siasa.

Vyama vya siasa vibaki kwa uchaguzi mkuu tu yani madiwani, wabunge na rais. Period.

Uchaguzi wa serikali za mitaa kuhusisha vyama haina mantiki na ni kuleta tu tension na uhasama bila sababu na kuwagawa wananchi.

Mtu kama m/kiti wa kitongoji, kijiji au mtaa kutokana na chama nini faida yake haswa. It's totally illogical and without rationale.
 
Mkuu uchaguzi utaendelea kama ulivyopangwa. Mligomea kujiandikisha, Watanzania wenye sifa wakajiandikisha. Baada ya kuaibika huko, mmenda kichwakichwa kuchukua fomu za kugombea hata taratibu hamzijui na hamkujiandaa. Mmefutwa. Sasa eti uchaguzi ufutwe. Haufutwi ng'ooo!
 
[emoji30][emoji30][emoji30]
Screenshot_20191016-224559-picsay.jpeg
 
Kutokana na Waziri Suleiman Jafo, kutangaza kuyarudisha majina yote yaliyokuwa yamekatwa hapo awali na kuyarudisha kwenye uchaguzi, ni bora yakafanyika mawazo ya busara na kuufuta huu uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu na kipangwa tarehe nyingine mbele na usimamiwe na Tume ya uchaguzi ya Taifa.iliyo huru,kwani ni dhahiri hawa wasimamizi wa uchaguzi huu, ambao ni makada wa CCM, waliosababisha uchaguzu huu uvurugike,hawafai tena kuendelea kusimamia uchaguzi huo

Naiomba sana serikali ifuate ushauri hiu, kwa kuwa inapaswa kuhakikisha zoezi zima la kuchagua viongozi wa serikali za mitaa ni LAZIMA liwe huru, kwa kuwa wananchi wenyewe ndiyo wanaopaswa kuwachagua viongozi watakaowawakilisha.

Ili kurejesha ari ya wapiga kura, ni vyema zoezi zima la kuanzia kujiandikisha wapiga kura, uchukuaji wa fomu kwa wagombea likaanza upya kabisa, chini ya wasimamizi wapya, Tume ya uchaguzi ya Taifa

Kwa kuwa zoezi zima la uchaguzi huru na wa haki lina umuhimu mkubwa ns kama mjuavyo wasimamizi hao wamethibitisha pasipo shaka yoyote, kupendelea chama cha CCM, hawafai tena kupewa jukumu hili la kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki

Niwape mfano mmoja tu, mathalani kuna mechi ya mpira baina ya watani wa jadi baina ya Simba na Yanga, itokee refa na washika vibendera wote 2 wawe ni wanachama wa timu mojawapo kati ya hizo 2, utegemee ile timu nyingine, ipeleke timu uwanjani??

Ni dhahiri hiyo timu pinzani, haitapeleka timu uwanjani na haiwezi laumiwa na uamuzi huo, wa kutopeleka timu uwanjani

Vivyo hivyo katika uchaguzi huu, iwapo serikali hii ina nia ya dhati kabisa ya kuuendesha uchaguzi huu uwe wa huru na wa haki, ni lazima wahusishe wapinzani, hususani wa vyama vikuu vya uoinzani nchini vya Chadema na ACT wazalendo, katika zoezi zima la uchaguzi na kusiwe na kificho cha aina yoyote, ili zoezi hilo lihesabike kuwa huru na la haki
 
Kama Taifa hatuwezi kuandaa uchaguzi wa kihuni wa aina hii, ni lazima pia tufahamu kuwa tunajidanganya kwa kudhani kuwa uchaguzi huu ni wa ndani ya nchi kwa hiyo mataifa ya nje hayapaawi kuuingilia

Tutambue kuwa dunia nzima inatushangaa hivi sasa, kwa kuendesha kitu tunachokiita Uchaguzi wakati katika uhalisia tunachoendesha ni UCHAFUZI wa hali ya juu sana!
 
Umenena vyema Sana mtoa hoja ila ingekuwa vizuri ungetuwekea data za kutosha kuhusu hoja zako ili tukuelewe zaidi,kwani kusema Tu bila ushaidi ni ngumu kukuamini

Je wapinzani wamekataa kweli kwa kuonewa au ni mpango wao? Nadhani waliokuwa wanajaza walikuwa na kopi za hizo karatasi watuonyeshe hayo pia
Upumbavu huu.. jafo kasema wameonewa warudishwe.
 
Back
Top Bottom