Uchaguzi 2020 Uchaguzi tarehe 28; CHADEMA inapoteza kila kitu

Uchaguzi 2020 Uchaguzi tarehe 28; CHADEMA inapoteza kila kitu

Endelea kujitekenya na kucheka mwenuewe! Kama ule wizi uliozoeleka ndo mnaoutegemea ujue mwaka huu mtaula wa chuya!
Nakuhakikishia kama uchaguzi huu utakuwa wa HAKI, Lissu anatua ikulu!
 
Kama ingekuwa hivyo unavyowaza NECCCM Tumeccm Polisiccm wasingekuwa busy kuwahujumu kuidhoofisha chadema wangeacha wananchi waamue wenyewe
CHADEMA wanajijihujumu na kujidhoofisha wenyewe kwa kumuachia Mbowe aibe ruzuku yote badala ya kuzitumia kuendeleza chama. Mnasema mnajuwa kutumia pesa vizuri, mngekuwa mnajuwa kutumia mngetumia pesa ya Ubelgiji kwa kukodisha "chopper".
 
Hoja zako ni mfu.

Ccm inabebwa na mfumo yaani katiba wala si utendaji.
Kama ulivyosema cdm inabebwa na lissu uchaguz huu ila kumbuka Msingi ulijengwa na Watu wengine pia wapo waliopoteza mpaka maisha na bado mbowe Aeiinua mpaka leo UNAITENGENEZEA HOJA HAPA.

Ukizungumzia wabunge kukosa nafasi basi kwa akili yako finyu ndy unajua kinakufa kumbuka UPINZAN WALIGOMEA UCHAGUZ WA MARUDIO ZANZIBAR 2015 NA BADO WATU WAPO WANALIAMSHA DUDE NA NI TISHIO KUBWA TENA.

UCHAGUZ WA MITAA HAWAJASHIRIKI NA MWAKA UMEKATA WANANCHI HAWAONI TOFAUTI SEMBUSE KUKOSA HAO WABUNGE KADHAA.

WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO WASIPOYAONA CCM WANATAFUTA HUKO KWINGINE. UCHAGUZI HUU UNAWEZA KULETA MABADILIKO MAKUBWA SANA HAUTAISHA KAMA ZILE ZA MAMLUKI WA CCM SLAA, MREMA,LOWASA NA LIPUMBA.

Uchaguzi huu umetufanya watanzania kuwajua madalali wanahangaika duniani huko kupigia udalali nchi yetu na rasilimali zetu

Uchaguzi huu umefanya mtanzania ayajue mataifa yenye uchu na tamaa kubwa kuja kujichotea mali zetu kwa matamko yao yaliyojawa jazba na sintofahamu wakiwa wamechanganyikiwa na speed ya maendeleo inayowafanya wahofie kupoteza target

Uchaguzi huu unazidi kuthibitisha kwamba John Pombe Joseph Magufuli ni rais bora duniani anayetetea maslahi ya watu wake. Alitutetea kwenye corona na sasa anatutetea dhidi ya wachuuzi, madalali wanaotaka kututawala kwa nguvu

Tukutane hapa kuanzia tarehe 28 kupeana pole na kupongezana
 
Mbona NEC na polisi umewasahau... mnaenda kutoka kwa shari au kwa heri
 
SABABU 31 ZA KUMKATAA MAGUFULI 28 OKTOBA 2020:

1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5
3. Ameongeza makato HESLB toka 8% to 15%
4. Amefukuza wafanyakazi na hajawapa hata senti tano kisa vyeti feki
5. Kaondoa fao la kujitoa NSSF
6. Kaondoa wanunuzi binafsi wa kahawa waliokuwa wanatoa bei nzuri
7. Karudisha gharama za matibabu kwa watoto na wajawazito
8. Anatoza maiti kodi kuzitoa mochwari
9. Kavunja katiba ya nchi kuzuia wapinzani kufanya mikutano halali ya siasa
10. Katunga sheria kandamizi kukomoa watu
11. Kabambikia kesi watu kwa visasi na chuki
12. Kafilisi wafanyabiashara kwa chuki binafsi
13. Kathibiti mashirika ya kutetea haki za binadamu
14. Kadhibiti na kutisha vyombo vya habari na kuviamrisha vimtangaze yeye tu na chama chake
15. Kavuruga sana mahusiano ya kimataifa
16. Kavuruga demokrasia na anataka wananchi waishi kama mifugo yake kufuata analotaka
17. Kazima bunge live na kulitumia bunge kama muhuri kufanya mambo yake
18. Mahakama imebinywa na imekuwa siyo huru tena
19. Kawadhibiti viongozi wa dini wanaomkosoa na kumwambia ukweli
20. Kanunua ndege bila kufuata sheria ya PPRA
21. Watu wengi wameuwawa na kupotea na kutekwa
22.Amelea na kulinda kikosi kazi cha "watu wasiojulikana"
23. Amepandikiza hofu,ukatili na dhuluma kama nyenzoza siasa mpya za Tanzania na utu umetoweka
24. Kakivuruga chama chake na kukimega vipande vipande
25. Kajenga uwanja wa ndege kwao bila ya approval ya bunge wala cabinet
26. Alisema tutaishi kama MASHETANI.. Kwa madai kuwa tulikuwa tunaishi kama Malaika. Hakika amelitimiza hilo.
27. Kuwa na kundi la watu wasiojulikana awamu hii ya tano na polisi hawajawai

28. Ni mwongo kupindukia – mwaka 2015 wakati anaomba kura aliongopa mengi km kumpa kila mwalimu kompyuta, kukipa kila Kijiji milioni 50 nk. Leo hii tunaingia uchaguzi mwingine, hajatimiza hayo na anaahidi mapya bila aibu.

29. Kudhalilisha akina mama kwenye majukwaa yake ya kisiasa

30. Kula rambirambi za wahanga wa majanga. Rais anayekula rambirambi zilizotolewa na watu mbalimbali ikiwemo nchi rafiki hatufai Watanzania.

31. Kuwakana Watanzania waliopata majanga km Wanakagera wakati wa tetemeko la ardhi.
Malalamiko yako yamekaa kihisia kuliko uhalisia! Ninahisi una mgongano wa kimaslahi, kama siyo vyeti feki uliyeondoshwa kazini, au unataka huduma za jamii za Serikali shule, hospitali ziwe za ovyo ili yako ipendwe, au una magari ya mizigo au mabasi hautaki Treni y JPM ifanye kazi au ni Wakala wa wenye ndege unatamani ATC ife ili wewe ufanye kazi au ni dalali wa mabeberu. Tuchape kazi tuijenge Nchi yetu , haitajengwa kwa maandamano,kucheza pull, malalamiko, kubeti na hakuna wa kutujengea mabeberu ni wavunaji tu tutachiwa mashimo!
 
Wakati CHADEMA wakipoteza kila kitu ambacho kwako wewe ni Urais, Ubunge na Udiwani, sasa kaa ukijua ni muda muafaka kwa CCM kupoteza pia.
Kupoteza kwa CCM kunaeleweka na watu wenye kutumia akili tu na kwa CCM wapo wachache mno ambao hawana sehemu ya kusemea hatari hiyo kwani wamezungukwa na kundi kubwa la vipofu wanaopiga kelele nyingi mno akiwemo wewe.
Msichokijua uchaguzi huu sio mwisho wa uchaguzi au Tanzania kuishi kwenye uso wa dunia. Kama kuna jukwaa zuri kwa upinzani kujipanga basi ni uchaguzi huu mbona kwa kuwa mmeamua kutotumia akili ila nguvu zaidi basi mnaenda kuidhihirishia dunia kuwa nyingi ni maadui wakubwa wa nchi hii.
Kama CCM ingeongozwa na mtu smart basi angewekeza kwenye akili na sio nguvu, sasa Magufuli anaenda kuwaachia CCM ya wajinga wengi na hapo ndio mtatafuta shimo la kuingilia mtalikosa na kile Magufuli alichokipanda ni swala la muda tu atalipia hata akiwa Chato na mkongojo wake.
Uwekezaji wa akili kaufanya JPM ikiwemo kuifanya Elimu Bure ili wanyonge pia wasome, vita vya kiuchumi, uzalendo na utetezi wa raslimali za Nchi!
 
Magufuli anaendelea kuwa Rais kwa muhula wa pili, wapiga kelele wa jamiiforums wengi hawapo hata kwenye daftari la mpiga kura + wanatumia multiple IDs ili kuonesha kuwa Lissu yuko juu!

Rais Magufuli ntampigia kura yangu aendelee kuongoza taifa letu, amefanya mazuri mengi ndani ya mda mfupi. Hawa wafuasi wa Lissu wamejitia upofu na kuungana na Lissu wakijinasibu kumuondoa Rais Magufuli [emoji23][emoji23][emoji23]

Hawawezi! Ushindi mapemaaaaaa[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji1241][emoji1241][emoji1241][emoji123][emoji123][emoji123]
Tupo wengi baba
 
Upinzani ukiendelea na ubishi wa kijinga na kujipa moyo kipumbavu, watapoteza na kukibomoa hata kidogo kilichopo.

Ingekuwa busara wapinzani, hata humu mitandaoni kukubali nguvu ya CCM kisha kusema tutapambana kadiri ya rasilimali na uwanja ukiwa sawa tunaweza kushinda.

Hii ya kujiaminisha kuwa mwaka huu tutashinda, hakuna kuiba kura wala mbinu itakayotushinda. Hii mbaya hii, ukipigwa ukiwa umesema hivyo ndio huaminiki tena, hata visingizio unakosa na unakuwa umepoteza pakubwa!

Ifike mahali upinzani ukubali ukweli ili kujenga upinzani wa 2025. Upumbavu usifanye 2025, mwaka wa uwezekano ikawa kuanza upya tena!
 
Kuna watu humu wanajipa moyo eti CHADEMA hii ya Lissu, Mbowe, Mnyika, Heche, Halima, Bulaya Matiko na Wenzake wanaweza kuishinda CCM ya Magufuli, Bashiru Ali, Mangula, na mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi.

Kama Kuna mtu anawaza hivo na anamanisha na ana amini Mawazo yake hayo yanaweza kuwa uhalisia, basi huyo ana tatizo kubwa sana kifikira.

Uchaguzi huu CDM iliyopalaganyika ikiwa inamtegemea mtu mmoja inakwenda kupambana na:
1. Rais Magufuli
2.Chama Cha Mapinduzi.
3.Watanzania

Tarehe 28 Watanzania bila kujali gharama, bila kujari Lissu anaahidi nini Watamkwepa, watajiepusha naye.
Msisahau hapa sijazungumzia swala la CCM kuwa Chama Dora!!

Nimevaa ngao🤣🤣🤣
Mkuu kajekudya , hapa ulisema kweli...
P
 
Bora sema wewe, tukisema sisi, tutanyooshewa vidole vya Makada!.
P
Mnanyooshewa vidole kwa sababu pamoja na kujua fika figisu wanazofanyiwa wapinzani na CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola, bado mnajifanya kutoa uchambuzi wenu feki as if uwanja wa kisiasa uko sawasawa kwa vyama vyote, kitu ambacho siyo kweli.
 
Mnanyooshewa vidole kwa sababu pamoja na kujua fika figisu wanazofanyiwa wapinzani na CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola, bado mnajifanya kutoa uchambuzi wenu feki as if uwanja wa kisiasa uko sawasawa kwa vyama vyote, kitu ambacho siyo kweli.
Tulia wewe, Watanzania wameamua
 
Hii nayo ni analysis juu ya ushindi wa kishindo.
Disgusting.
 
Kuna watu humu wanajipa moyo eti CHADEMA hii ya Lissu, Mbowe, Mnyika, Heche, Halima, Bulaya Matiko na Wenzake wanaweza kuishinda CCM ya Magufuli, Bashiru Ali, Mangula, na mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi.

Kama Kuna mtu anawaza hivo na anamanisha na ana amini Mawazo yake hayo yanaweza kuwa uhalisia, basi huyo ana tatizo kubwa sana kifikira.

Uchaguzi huu CDM iliyopalaganyika ikiwa inamtegemea mtu mmoja inakwenda kupambana na:
1. Rais Magufuli
2.Chama Cha Mapinduzi.
3.Watanzania

1.Rais Magufuli
Rais Magufuli tangu aingie Madarakani amekuwa akifanya baadhi ya Mambo ambayo yanakuwa reflected Kama ya kwake.Hali hii imemfanya pengine awe maarufu kuliko hata Chama chake. Magufuli amejijengea ufalme wake ndani ya mioyo ya Watanzania, siyo lazima akubalike na wote na hakuna anayetegemea iwe hivo, lakini ukweli umaarufu wake unamfanya yeye Kama yeye apate kura ambazo atapigiwa yeye Kama Magufuli, na nyingi ni zile za wasio na Chama.

Hizi kelele za mitandaoni dhidi ya JPM ukizifatilia ni za wale wale, hata thread humu ukiangalia wale wale ndio wanakoment, lakini waulize je Mama zao, Dada zao, wajomba zao, shangazi zao, Babu zao na Bibi zao wanaijua Facebook, wanaijua JF, wanaijua tweeter au Instagram. Jibu wanalo, je hoja ya Uhuru na maendeleo ya vitu inaeleweka kwa Hawa watu. Mtu ambaye hakuwahi kuona umeme( sizungumzii Maria Sarungi Wala Fatuma Katume, na Hawa hawafiki hata 5000) leo kauona umeme unaweza kumueleza asimchague Magufuli eti kwakuwa amemnyima Uhuru wakati anaenda kanisani, anapiga simu, anaenda sokoni anaenda shambani Bila wasiwasi akakuelewa?.

2. Chama Cha Mapinduzi
Dubwasha linalotisha, Dude hatari Barani Africa, dude ambalo Lina historia ya kuwaweka viongozi kadhaa wa Afrika Madarakani. Hili dude Lina vichwa, Lina Consultants, lina rasilimali watu na fedha za kutosha, Lina uzoefu wa kutosha katika anga hii ya siasa. Halafu Kuna mtu anawaza linaweza kushindwa na mtu anaitwa Tundu Lissu.

Hebu angalia muundo was CCM kuanzia hapo kwenye mtaa unaoishi, angalia kwa sasa kwenye eneo lako la nyumbani kumi muundo wa CCM, angalia WanaCCM hao katika muundo huo katika eneo Hilo la nyumba kumi walivyojipanga na wanavyoendelea kuzisanya kura kwa ajiri ya CCM. Sasa unaona, Kuna kura za Magufuli ambazo atazipata yeye na kura ambazo Chama Cha Mapinduzi kitazipata. Hali hii iliwahi kutokea mwaka 2005 ambapo Jakaya Mrisho Kikwete yeye Kama yeye alipigiwa kura na CCM nayo ikapata kura zilivyounganishwa mkwere akapiga 80%. Lakini 2010 watu wakawa hawana hamu naye, lakini Chama Cha Mapinduzi kikamtafutia kura. Akapiga 61% Kama sikosei, hizi zilikuwa za Chama.

Najua wengi mmejaa kwenye Social Media, hamupo field, hamuoni huo muundo ulivyo hatari. CDM is no where, katika level hizi, CDM ipo mgongoni kwa Lissu. Upande mwingine Kuna CCM Kuna Magufuli na Kuna CCM.

Sasa ukiangalia hali ilivo Sasa unaona kabisa atapigiwa parefu, lakini bahati mbaya hata upande wa Wabunge Mambo ni magumu mno. Majimbo ambayo siku za nyuma yalikuwa ni hoja isiyobishaniwa Sasa mwaka huu ni hoja nzito, Pale Mbeya Sugu amekamatwa Ke....nde, na Dr. Tulia, Lema ameshikwa Pu....bu, na Gambo, hapo Arusha, Mbowe jasho linatirtika hadi kwenye meno, Mzee wa Kondoo wa bwana anapumulia Kisogo Cha Halima. CDM ni Kama wapo kwenye furushi ambalo tarehe 28 linadondoka.

3. Watanzania
Sisi tunayo Kariba ambayo tumejengewa na Mzee Baba mwenyewe, Mchonga, Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere. Ni Kariba ambayo unaweza iita utakavyo kulinga a na muono wako, Njema sana, Mbaya, woga, au uungwana.

Watanzania tunapenda Amani Bila kujali gharama yake, Watanzania ni wavumilivu bila kujali gharama, Watanzania tunapenda uungwana sana, hatupendi Shari, lakini mbaya zaidi tunayo Imani Kali kuwa Mabeberu ni watu hatari, na watu wabaya sana. Lakini sisi ni wanafiki, Watanzania ukiwa na sisi tutakueleza hivi, ukitoka tunafanya tofauti, Tunakutanguliza halafu tunasikilizia, upepo ukibadilika tunaingia mitini!

Watanzania ukishaonyesha dalili za ushari, dalili za kuleta uvunjifu wa Amani au ukajinasibisha na Mababeru, au ukasingiziwa Mambo hayo, basi sisi Watanzania tunachofanya, tunakukwepa.

Tarehe 28 Watanzania bila kujali gharama, bila kujari Lissu anaahidi nini Watamkwepa, watajiepusha naye.
Msisahau hapa sijazungumzia swala la CCM kuwa Chama Dora!!

Nimevaa ngao🤣🤣🤣
Mkuu ulisema ukweli mtupu wakabeza sasa nafikiri wanaweza kukubali wameshapigwa!
 
Back
Top Bottom