Uchaguzi 2020 Uchaguzi tarehe 28; CHADEMA inapoteza kila kitu

Uchaguzi 2020 Uchaguzi tarehe 28; CHADEMA inapoteza kila kitu

Bora sema wewe, tukisema sisi, tutanyooshewa vidole vya Makada!.
P

..Tundu Lissu ana kipaji cha siasa kumzidi Magufuli.

..Na matumizi ya Tundu Lissu ktk kampeni siyo makubwa kama ya Magufuli / CCM.

..Chadema wanaonekana kufanya kampeni na siasa kutokana na wito, wakati CCM wanaonekana kusukumwa na uchu wa madaraka.

..CCM wanacheza rafu nyingi za kisiasa kwa kutumia taasisi mbalimbali za dola, wakati Chadema wamejiegemeza kwa wananchi.
 
Yaani chadema Kama chama kikuu Cha upinzani kimepoteza muelekeo, huwezi kuwaaminisha watu eti utashinda urais na wakati wagombea ubunge na madiwani hawana muelekeo, utashinda vipi Kama si bangi hizo? Hata Kama ukishinda bado Hawa wenye wabunge wengi watawapelekesha tuuu kiufupi vyama vya upinzani mnatimiza wajibuu Hapo.
 
Yaani chadema Kama chama kikuu Cha upinzani kimepoteza muelekeo,huwezi kuwaaminisha watu eti utashinda urais na wakati wagombea ubunge na madiwani hawana muelekeo,utashinda vp Kama cibangi hizo? Hata Kama ukishinda bado Hawa wenye wabunge wengi watawapelekesha tuuu kiufupi vyama vya upinzani mnatimiza wajibuu Hapo.
Kama ingekuwa hivyo unavyowaza NECCCM Tumeccm Polisiccm wasingekuwa busy kuwahujumu kuidhoofisha chadema wangeacha wananchi waamue wenyewe
 
Kuna watu humu wanajipa moyo eti CDM hii ya Lissu, Mbowe, Mnyika, Heche, Halima, Bulaya Matiko na Wenzake wanaweza kuishinda CCM ya Magufuli, Bashiru Ali, Mangula, na mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi...
Ni bora pole pole achukue posho yake aliyokulipa maana utumbo uliouandika hata wewe huuamini!!!

Kama Tundu Lissu hawashindi msingehangaika nae kuzuia kampeni zake na mikutane yake, msingehangaika kukataa kuwaapisha mawakala wa Chadema na wala msingezuia vyombo vya Habari kurusha Habari zake.

Ccm jiandaeni tu kuwa wapinzani rasmi 2020-2025 maana mtake msitake Tundu Antiphas Lissu ndo Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025
 
Lawyer umeandika pumba sana, hebu tufafanulie ni kundi gani la kijamii ambalo CCM ina uhakika wa kura zao? Tuanze wanafunzi, watumishi wa umma, watumishi wa sekta binafsi, wafanyabiashara wakubwa, wa kati, wadogo, machinga? Wasiokuwa na ajira, waliachishwa ajira zao kwa sababu mbalimbali za kiuchumi au za chuki, wana CCM wa zamani, wanaCCM mpya, wagombea, wateuliwa, walioula kipindi hiki cha 2015-2020 (kikazi au kibiashara) of which hali ya biashara wote tunaijua awamu hii, uchawi wa biashara upo kwenye mzunguko wa pesa kama hakuna mzunguko?

Haya, tuongeze kundi la wale wasiojielewa, kwanza hawaelewi kwanini wanapiga kura, ni bendera fuata upepo, na kundi la wajinga wachache/wengi kwa kadri uonavyo wewe wakati huu una wajinga wengi au wachache? Eennhee nikasau kundi la wakulima wadogo na wakubwa. Hebu tuchambulie kura zinatoka wapi hapa.....
 
Hatutaki Rais dikteta ,sauti za wananchi kuzizima, bunge letu kuwa kibogoyo, Radio zote kutangaza habari za ccm,magazeti yote kutangaza habari za ccm,watu kupigwa risasi ovyo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ,kulagai wakulima kuwa nitanunua mazao lakini ndio kwanza mazao yamekufa ,korosho hola,alizeti hola,mpunga hola,kahawa hola biashara nyingi zimefungwa sasa serikali ya namna hii ni ya nini huyu ni Idd Amini wa Tanzania hafai hata kwa kulumagia
We wasema!
 
Back
Top Bottom